Monday, March 2, 2015

UJUMBE WA VITALI MAEMBE KWA WANASIASA.
Na Vitali Maembe,

Waziri ametuomba wasanii tuivunje Demokrasia!
Ametuomba tujidharaulishe sisi na kazi yetu!
Ametuomba tutembee watupu hadharani!
Haya sikuambiwa, nimeona kwa macho yangu, nimesikia kwa masikio yangu!

Alianza kwa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kuwa anatazama, anasikiliza na kuzisoma kazi zetu za sanaa. Huu sio kweli, kama kiongozi huyu DKT. FENELLA MUKANGARA na walio mteua wangekuwa wanafanya hivyo nchi hii ingekuwa mbali! Sera ya yetu ingekuwepo!
Rais na Mawaziri hawaitazami michoro yetu wala hawasikilizi nyimbo zetu, na kama wanafanya hivyo basi ni kwa bahati mbaya au nia tofauti.

Wasanii wenzangu, mlioamua kuwa wasanii, mliojikuta ni wasanii na nyie mlioambiwa muingie kwenye sanaa kutafuta tonge tu nisikilizeni.

'Sanaa ni Demokrasia tosha, Sanaa ina miiko ambayo inasisitizia Usawa na haki na wajibu. Kushawishi na kudanganya sio kazi ya sanaa, Sanaa ni kuonya, kuelimisha, kuburudisha na kumuacha mtu aamue kulingana na sanaa ilivyomfunulia mambo! wala sio kuamulia mtu au kuingilia Uhuru wa Mtu. Wasanii na watu wengine wanapaswa kusisitiziana kujiandikisha na kupeana Elimu ya kupiga kura, kamwe si kuilazimisha jamii kuikubali au kuikataa Katiba.

'Hivi mnatutakia nini sisi nyinyi Wanasiasa? Mmetutumia vibaya wasanii na wanahabari Kwanza mmetuvua nguo, hali mnajua tupo uchi mnatupapasa tuwaeleweje, mnataka kutuibia au mnataka kutubaka?


Tumewalisha sana, tumeandaa chakula tule wote, nyinyi mnakula kidogo mnajifanya mnatujali sisi wenye njaa sana, kumbe usiku mnaenda kufukua Makaburi mnakula nyama za ndugu zetu....' endeleeni!

No comments: