Sunday, March 1, 2015

TAARIFA YA JESHI LA WANANCHI: AJALI YA NDEGEVITA YA JESHI LA WANANCHI MWANZAJESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA


Makao Makuu ya Jeshi

Simu ya Upepo:“N G O M E”

Sanduku la Posta 9203, DSM

Simu ya Mdomo : 22150463


Telex        : 41051  


Tele Fax   : 2153426

27, FEB15


                   
                                       
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto.

Hata hivyo, rubani wa ndgevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu.

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,  
Dar es Salaam, 
Tanzania.


Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963

No comments: