Monday, March 2, 2015

SHUGHULI YA KUMUAGA KAPTENI JOHN KOMBA KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE.Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima zake za mwisho mbele ya mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapt. John Komba

Mwili wa Kapteni John Damian Komba ukiwasili katika viwanja vya Karimjee

Askari Maalum wa Bunge wanaojulikana kama Sergeant et Arms wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa hayati Kapteni John Komba

Mwili wa John Komba ukiwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo

Mwili wa Kapteni John Komba ulipofikishwa nyumbani kwake Mbezi Beach kwa Komba asubuhi ya leo.DONDOO MUHIMU ZA MTIRIRIKO WA MATUKIO YA KUMUAGA HAYATI KAPTENI JOHN DAMIAN KOMBA  • Shughuli zimeendelea kwa viongozi wa kitaifa, serikali, Bunge na vyama vya siasa kutoa salam  zao za rambi rambi

  • Viongozi wa dini kuongoza kwa sala

  • Wasanii mbalimbali kuimba nyimbo maalum za kumkumbuka Hayati  Kapteni John Damian Komba

  • Utaratibu wa kuaga kwa viongozi, wanasiasa, wananchi wa kawaida

  • Familia yamuaga rasmi

  • Safari ya kwenda Uwanja wa ndege Terminal One unaanza. Kutakuwa na ndege mbili moja itakayoubeba mwili wa Kapteni John Komba na watu wa karibu na familia yake. Nyingine itakayowabeba viongozi wa serikali, wabunge wote kutoka mkoa wa Ruvuma, wabunge walioteuliwa na spika, ndugu, jamaa, familia na marafiki.

  • Mwili utaagwa leo jioni katika viwanja wa majimaji mjini Songea mara utakapowasili.

  • Kesho ni maziko katika vijiji vya Lituhi mkoani Ruvuma.No comments: