Sunday, March 1, 2015

RATIBA NA UTARATIBU WA KUMUAGA KAPTENI JOHN KOMBA
TANZIA- TAARIFA ZAIDI / RATIBA MSIBA WA KAPTENI JOHN KOMBA

Ratiba ya kusafirisha mwili wa marehemu Mhe. Capt. John Komba itakuwa kama ifuatavyo:

Kesho tarehe 02/3/2015 saa 1 asubuhi kutakuwa na  misa ya kumuombea Marehemu Kapteni John Damian Komba katika parokia ya Mt. Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni  lililopo mbezi Beach.
  •  Saa 4 asubuhi mwili utaelekea Karimjee kwa ajili ya kuagwa.  
  • Saa 8 mchana mwili utaelekea airport tayari kwa safari ya kuelekea Songea. 

Mazishi yatafanyika tarehe 3/3/2015 kijijini kwake Lituhi.
Kufuatia Msiba huu shughuli za kamati za Bunge hazitakuwepo kwa kesho tarehe 2/3/2015. 

Ukipata taarifa hii tafadhali mjulishe na mwingine.


IMETOLEWA NA;
OFISI  YA  KATIBU WA BUNGE

1.3.2015

No comments: