Monday, March 2, 2015

MBOWE AZINDUA KIKOSI CHA RED BRIGADE MKOANI MWANZA.

Mkurugenzi wa masuala ya usalama wa CHADEMA ndg. Wilfred Lwakatare akimwongoza mwenyekiti wa CHADEMA kuvikagua na kutoa kiapo maalum kwa kikosi cha ulinzi cha CHADEMA almaarumfu kama Red Brigade katika mkoa wa Mwanza

Mwenyekiti wa CHADEMA akipokea viapo utiifu na uaminifu  vya walinzi maalum wa CHADEMA. 

Kikosi cha CHADEMA kikiwa kwenye mstari wa gwaride

Kikosi cha CHADEMA cha Red Brigade kilichopo Mwanza kikionyesha ukakamavu wao. Na wakionyesha kwa vitendo salamu ya" peoples power" inayotumiwa sana na CHADEMA. Kuanzishwa kwa vikosi vya ulinzi vya CHADEMA ni sehemu ya mkakati wao na malengo kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015. Vikosi hivi vina jukumu maalum la kulinda kura zisiibwe na aina yoyote ya rafu itakayochezwa na vyombo vya serikali dhidi ya CHADEMA , watendaji wa CHADEMA, rasilimali za CHADEMA na wanachama  pamoja na wanaoitakia mema CHADEMA na ulinzi kwa  viongozi wa CHADEMA kwa ujumla wake.

No comments: