Monday, March 2, 2015

HIFIKEPUNYE POHAMBA: MSHINDI TUZO YA MO IBRAHIM.Mheshimiwa Hifikepunye Pohamba rais wa Namibia aliyemaliza muda wake.Na Baraka Mfunguo,

Rais wa Namibia  anayemaliza muda wake Hifikepunye Pohamba amenyakua tuzo maarufu ya MO Ibrahim. Rais Pohamba  ametajwa kuwa mshindi kutoka katika mmoja wa mwanajopo aliyeshiriki mchakato wa kumpata kiongozi bora anayestahili tuzo hiyo, ndg. Salim. A. Salim jijini Nairobi. Misingi muhimu inayozingatiwa katika utwaaji wa tuzo hiyo ni Utawala Bora, Mapambano dhidi ya rushwa, utawala wa sharia, majadiliano na utawala wa demokrasia pamoja na haki za binadamu.


Kwa mujibu wa utaratibu wa Taasisi ya MO Ibrahim mshindi wa zawadi hii atanyakua kitita cha dola milioni tano kwa miaka kumi na dola laki mbili katika kipindi cha maisha yake. Komredi Pohamba ni mmoja wa wapambanaji katika ukombozi wa kusini mwa Afrika katika nchi ya Namibia iliyokuwa ikitawaliwa na Afrika ya Kusini kupitia chama cha SWAPO. Na amehudumu katika urais katika misimu /mihula miwili mwaka 2004 na 2009. Mrithi wake anatajwa kuwa ni ndg. Hage Geingob. Tangu  uhuru wa nchi ya Namibia mwaka 1990, chama cha SWAPO kimekuwa kikitawala na kuongoza katika siasa za nchi hiyo ambayo hufuata utawala wa vyama vingi.Pohamba ametajwa kuwa mshindi wa tuzo  ya MO Ibrahim kwa mwaka 2014 katika hafla iliyofanyika jijini Nairobi. MO Ibrahim ni Mwingereza mwenye asili ya Sudan , mjasiriamali na mmiliki wa makampuni yanayojihusisha na mawasiliano na mtu anayejitoa katika masuala ya kijamii katika kutatua changamoto mbalimbali. Alizindua tuzo hii kama hamasa kwa viongozi wa Ki Afrika katika kuzingatia utawala bora wa sharia unaozingatia na kuheshimu haki za binadamu, demokrasia na uwajibikaji. 

Tuzo ya kwanza ilitolewa mwaka 2007 kwa Joachim Chissano  rais wa zamani wa Msumbiji. Natumaini kuwa Rais Jakaya Mrisho wa Tanzania atashinda tuzo ya MO Ibrahim awe kiongozi wa kwanza katika historia ya Tanzania kwani ana vigezo na anastahili.

No comments: