Saturday, March 7, 2015

AINA YA VIONGOZI TUNAOWAPANDIKIZA.

Pichani rais wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini akimpiga mmoja wa mwanachama na mfuasi wake. Tafrani hiyo ilizuka wakati walipokuwa wamekwenda kumwona rais kumweleza kilio chao cha muda mrefu kuhusu usalama wao kutokana na matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika maeneo ya kanda ya ziwa kwa imani za kishirikina. Kiongozi huyu hana tofauti na viongozi wetu tunaowachagua ama wanaochakachua matokeo na kubaki madarakani. Matokeo yake wananchi wakidai haki zao wanapigwa mabomu, wanapigwa risasi, wanauliwa wamachinga wanadhulumiwa mali zao. Hii ndio demonstration ya viongozi tulio nao sasa. Na kuna msemo ule unaosema" shukrani ya punda ni mateke". Na hii ndio shukrani ya viongozi wetu tuliopandikiziwa .

No comments: