Sunday, February 22, 2015

WAHITIMU WA JKT WALIOPEWA AHADI FEKI YA AJIRA NA SERIKALI WAMTEMBELEA MWENYEKITI WAO MUHIMBILI.
Update:
 Katibu wa umoja wa wahitimu wa JKT walioahidiwa ajira hewa na serikali amekamatwa kwa kosa la kupanga njama ya kufanya maandamano bila kibali. Mwenyekiti wa  wanafunzi wahitimu JKT walioahidiwa ahadi hewa na serikali ya kuajiriwa baada ya mafunzo ya JKT,ndg. George Mgoba akiwa wodini akiugulia baada ya kutekwa na watu wasiojulikana .

Baadhi ya wanafunzi wahitimu wa JKT walioahidiwa ajira hewa na serikali  wakiingia hospitalini.

Baadhi ya wanafunzi wahitimu wa JKT walioahidiwa ajira hewa na serikali  wakiingia hospitalini Muhimbili kwenda kumuona mwenyekiti wao aliyetekwa na watu wasiojulikana.

Baadhi ya wanafunzi wahitimu wa JKT walioahidiwa ajira hewa na serikali  wakiingia hospitalini Muhimbili kwenda kumuona mwenyekiti wao aliyetekwa na watu wasio julikana.

Polisi wakionyesha uwepo wao kwa kigezo cha kuimarisha usalama

PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS


Na Baraka Mfunguo,

Vijana wahitimu  waliopata mafunzo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kupewa ahadi feki na serikali pindi watakapomaliza mafunzo yao kwamba watapatiwa ajira, leo wamekutana katika eneo la Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, kisha kuelekea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kumjulia hali mwenyekiti wao George Mgoba ambaye alitekwa na watu wasiojulikana.

Askari walikuwepo katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuimarisha usalama ambao hata hivyo hawakuwa na umuhimu kwani wahusika walikuwa wamekwenda kumuona mwenyekiti wao aliyetekwa na kuteswa na watu wasiojulikana. Kutokana na ulinzi mkali uliowekwa ilikuwa ngumu kwa baadhi ya wadau wa habari kuweza kupata picha ya mwenyekiti huyo.


Matukio ya  utekwaji nyara kwa watu wanaojitoa mhanga kudai haki zao yamekuwa sio mageni nchini. Hususan tukio la kutekwa na kuteswa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya madaktari iliyokuwa ikitafuta suluhu na serikali dhidi ya madai ya madaktari nchi nzima ndg. Steven Ulimboka, kutekwa kwa baadhi ya wananchi waliokuwa wakihoji uhalali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam na matukio  mengine mengi ambayo yamekuwa hayazungumzwi kwenye vyombo vya habari kutokana na wahanga kufumbwa midomo/vinywa na mkono  mrefu wa serikali. 

Kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Tanzania pamoja na kuwa na utitiri  mashirika ya kudai haki za binadamu, matatizo hayo  yamekuwa ama yakifumbiwa macho na wadau   ama mashirika hayo kutokuwa na meno ya kutosha kuweza kukabiliana na serikali kutokana na mfumo mbovu wa usimamizi na utoaji haki katika ngazi zote, urasimu na suala la rushwa, na kukubali kuburuzwa na serikali.

1 comment:

Mbele said...

Serikali isiwe inatoa ahadi bila kutafakari uwezo wa kuzitekeleza. Hii ni enzi ya kuwafundisha na kuwawezesha vijana katika ujasiriamali na, kujiajiri kuliko kuwaaminisha kuwa serkali itawapa ajira.

Serikali ifunguke macho, sio kuwa usingizini kama vile tuko katika miaka ya sitini na kitu.