Tuesday, February 24, 2015

VURUGU IRINGA: POLISI NA WANANCHI KUFUATIA KUUAWA KWA MAMA NTILIE


Na Baraka Mfunguo, 

(Kwa hisani ya vyanzo mbalimbali vya habari)

WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi Ilula na kuvunja milango , kuchoma moto kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili pia yameteketea kwa moto.


Kituo hicho  cha polisi cha Ilula mkoani Iringa, kimechomwa na wananchi wenye hasira kufuatia polisi kumuua mwanamke mmoja mfanyabiashara ya mama ntilie kufuatia msako maalum ulioendeshwa na jeshi la polisi dhidi ya wafanyabiashara wanaofanya biashara ya pombe za kienyeji na mama ntilie katika Manispaa ya Iringa .Inaelezwa  wakati wa purukushani za kukimbia, ndipo polisi mmoja alimchota mtama huyo mama wakati anakimbia na kusababisha mama wa watu kuanguka na kufariki hapo hapo marehemu ametambulika kwa jina la Mwanne Ally.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.

Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.
Gari  zilizosheheni  mabomu za kikosi cha kutuliza ghasia FFU zimewasili   mabomu ya machozi yanapigwa mfululizo, wanasafisha barabara kwa kuzima moto na kutoa matairi njiani.


No comments: