Tuesday, February 24, 2015

TAARIFA YA MAANDAMANO YA AMANI KUPINGA MAUAJI YA ALBINO TANZANIA
Na Zitto Kabwe, 
(Kwa hisani ya ukurasa wake wa Facebook)

Taarifa rasmi kutoka kwa Tanzania Albinism Society,kuhusiana na Maandamano ya amani ya kupinga mauaji ya Albino- kutoka kwa Mohammed Chanzi (Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Ulemavu wa Ngozi) ni kama ifuatayo:

Tarehe na Siku ya Maandamano: Tarehe 2 mwezi wa 3 (02/03/2015) Jumatatu

Mahala pa kukutania: Viwanja vya baharini vya Ocean Road Hospital (Nyuma ya hospitali ya ocean road upande wa baharini)

Muda wa kukutana: Saa Nane Mchana

Mavazi: Nguo Nyeusi (Pendekezo: Tshirt Nyeusi)

LENGO KUU: Kufikisha ujumbe kwa mheshimiwa Rais kuhusiana na simaziiliyokumba watanzania juu ya mlipuko upya wa mauuaji ya Albino, Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunasimamia haki na tunayalinda maisha ya wenzetu, Maandamano haya yameidhibishwa na Polisi kanda maaum ya Dar-es-salaam na ni ya amani.
RAI- Asasi zote za kijamii, za kiserikali na zisizo za kiserikali. wanaharakati wote, wapenda amani na wapigania haki wote wanaombwa sana kushiriki kikamilifu katika maandamano haya yatakayoanzia hapo viwanja vya Ocean Road mpaka Ikulu kupitia mtaa wa Lithuli.


Hii Inatuhusu wote, wanajamii, Watanzania. mjulishe na mwezako, njoo ujiunge na wenzako wanaopambania maisha ya wenzetu.

No comments: