Wednesday, February 18, 2015

MING'OKO: CHAKULA KIKUU MIKOA YA MTWARA NA LINDI

Ming'oko pichani ikiwa inachuuzwa rejareja mitaani mkoa wa Mtwara.


Na Baraka Mfunguo,

Kuna msemo usemao kuwa ukiwa kwa Mrumi  ama Roma ufanye kama yale ayafanyayo kwani ndio utaratibu wake na utamaduni wake. Wengi wetu tumekuwa tukisikia hadithi nyingi kuhusu vyakula vya mikoa ya kusini hususan  chikandanga, korosho, mihogo/makopa, ng'onda na "Samaki nchanga, ama wasudan ama mkanda nje" na majina mengine kede kede. Hadithi hizo ni za kweli isipokuwa tu samaki nchanga sio wale wa majumbani ni wale wa maporini. Na sio wote wanaokula samaki nchanga. Imani ya kiislamu mathalan, hairuhusu kuliwa kwa samaki nchanga. Samaki nchanga ni maarufu sana maeneo ya Masasi, Nanyumbu, Nachingwea, Ruangwa, Nanganga na maeneo ya viunga vya Ndanda.

Leo nazungumzia Ming'oko, ming'oko ni aina ya kiazi kikuu ambacho hakilimwi bali hujiotea chenyewe na huchimbwa maporini. Ni chakula kinachoheshimiwa na ukitaka uchukiwe na watu mmnyime mng'oko. Ni utamaduni ambao umezoeleka na wala sio suala la kuuliza kwa nini. Ming'oko ina faida nyingi kiafya na inaelezwa inajenga kinga mwili za binadamu dhidi ya magonjwa. Pia inaelezwa kuwa ni zao ambalo linaaminika kiimani kitamaduni miongoni mwa wanakusini.. Hivyo ukikaribishwa mng'oko usikatae. Ming'oko huweza kuliwa na chochote vile upendavyo waweza kukifanya kama staftahi, chakula cha mchana ama mlo wa kawaida wa kutoa hamu.

No comments: