Siku kama ya Leo tarehe 7 mwezi februari 2008 nchi yetu ilikuwa katika hali ya sintofahamu katika kile kilichoitwa sakata la Richmond. Sasa ni miaka saba imepita zipo siri nzito zimejificha nyuma yake lakini siku hadi siku tunayaona mabadiliko na kukua kwa Imani ya Watanzania.

Baada ya Alhamis ile ambayo naiweza kuiita ni Alhamisi ya ushindi wa mahafidhina walio jaa damu ya watanzania kwa Maneno mafupi naweza sema kwa Lugha ya kiingereza (You can win a battle but you loose a war) mambo kadhaa sasa yamewekwa hadharani juu ya hayo na kupoteza mwelekeo wa taifa.

UKWELI WA SERIKALI KUSHINDWA KESI DHIDI YA RICHMOND.
Katika shauri la serikali lilofunguliwa dhidi ya iliyoitwa kampuni hewa ya Richmond, kama ilivyo njia fupi ya mfitini baada ya maelezo marefu ya kifitina ya Tume ya mwakyembe serikali iliishtaki Richmond kwa kupata mkataba kwa ulaghai , Richmond walijieleza mahakamani kwa vielezo vyote na kushinda kesi na hata serikali ilipo kata rufani ilishindwa tena , hii siri mahafidhina hawaitaki kuizungumza sababu mahakama ilithibitisha mkataba kuwa ulipatikana kihalali.

SIRI YA SERIKALI KUTOLIPA HATA SENT TANO KWA RICHMOND HADI LOWASSA ANAJIUZULU.
Lowassa aliamua kujiondoa katika serikali huku serikali ikiwa haijapata hasara hata ya sent moja kwani binafsi Edward Lowassa alijijua ni mtu safi na amejiuzulu kwa sababu ya tatizo la uwaziri Mkuu, Kwani malipo kwa Richmond yalisimamishwa hadi pale walipo shinda kesi mahakamani.

SIRI KUHUSU MITAMBO YA KUZALISHA UMEME YA DOWANS INAYO TUMIKA HADI LEO.
Mahafidhina wale wale kwa kutumia bunge la Samwel Sita walisema mitambo ile ya Richmond haiwezi kununuliwa na serikali kutoka Symbion kwani haiwashi kibatari huku Dr Rashidi akiwa amewaita wakaguzi huru kutoka Ujerumani na wakauthiditisha kuwa ipo imara, wakasababisha kujiuzuru kwa Dr Rashid na kuumbuliwa na Hillary Clinton na Obama kwa kuikubali walipo itembelea. laitani wangeinunua kama Dr Rashidi alivyo shauri tungelikuwa tunaokoa garama za capacity charge Toka kwa DOWANS.

KUSHUKA KWA UFAULU MARA KADHAA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI.
Wasomi na wataalamu mbali mbali wanao amini katika Vision au Creativity huamini njia pekee ya kufikia lengo la aliebudini ni kuwa mmoja ya watekelezaji , Edward Lowassa ni mmoja ya walio kuwa na dhamira ya dhati ya Elimu ,alisimamia shule za kata kujengwa nchi nzima takribani shule elfu moja toka 2006 hadi 2008, Kujiuzulu kwake kuna siri nzito ya Serikali ya kushindwa kujenga vyumba vitatu vya maabara,hili tunafichwa kuwa serikali imeshindwa kufikia lengo.

KUONGEZEKA KWA WIZI SERIKALINI NA UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA.
Hapa ndipo ilipo siri nzito ya takribani miaka saba sasa, Edward Lowassa alikataa kushiriki michezo michafu, mahafidhina waliozoea kula kwa takribani miaka miwili ya Uwaziri Mkuu mianya ya Rushwa ilizibwa na kiasi cha kufanya waunde na waandae zengwe la kumtoa katika nafasi, na wote walio shiriki katika kumng'oa Lowassa madarakani wanahusika katika masakata ya wizi hivi karibuni kuanzia ,Pesa za Congo kwa watu kuchukua pesa na kuwapeleka wanajeshi wetu vitani, Escrow, Nguzo za Kinyerezi, Vitambulisho vya taifa NIDA, Bandari na Vibali vya sukari.

MWISHO.
Watanzania wenzangu hebu tufumbuke macho, mtanzania mwenzetu anahatarisha maisha yake, furaha yake ya kuwa Tanzania , anapambana Siku zote kuufuta umasikini. Tutafakari siku ya Leo Tar 7/02 /2015 kwa maisha ya watanzania kwa maisha na mustakabali Wa Taifa . Ni imani yangu siku ya Leo itaonyesha tashwira ya taifa hili kuelekea Maamuzi na Matumaini Mapya na Edward Lowassa 2015. Lowassa ndiye atakayeweza kutatua migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji hivi sasa pamoja na wawekezaji kwa ujumla. Lowassa ana uthubutu wa dhati na dhamira njema kwa watanzania.