Saturday, November 22, 2014

SINEMA YA ESCROW INAENDELEA...............

HABARI HIZI HAZIJATHIBITISHWA RASMI. BLOGU HAIHUSIKI KWA NAMNA YOYOTE NA MITAZAMO AMA ITIKADI ZA WATOA TAARIFA HIZI. NA HAIEGEMEI UPANDE WOWOTE WA SIASA ZA NCHI.


Mtazamo: Waswahili wanasema "Lisemwalo Lipo kama halipo basi laja". Tutayasikia mengi sana katika hili sakata. Wananchi wanastahili kupata taarifa sahihi kwa wakati sahihi na kupitia njia sahihi inayostahili na kueleweka na wote. Kukaa kimya  kwa serikali kutaweza kuleta matatizo na mtafaruku mkubwa. 

Katika Ulimwengu wa utandawazi, kila mtu ni mtoa taarifa, haijalishi taarifa hiyo kama ina utafiti ama makusudio yake ni nini katika hadhira iliyolengwa. 

Wapo wale werevu watakaong'amua pumba na mchele na kuchambua pumba na kuchukua mchele, wapo wale ambao  wataona ni kama uchafu tu kisha kupuuza, na wapo wale ambao ni wengi watajumuisha pumba na mchele na kuwa kitu kimoja. Kufanya hivi hatutatengeneza . Tunaumba janga.

- Baraka Mfunguo

UPDATE Nov 29/11/2014

KIKAO CHA BUNGE CHA JIONI
Maazimio nane yamepitishwa baina ya kamati za maridhiano kwa utekelezaji.

Waziri Mkuu aahidi kuyasimamia maazimio yote.

Sinema ya Escrow imekwisha rasmiKIKAO CHA BUNGE CHA ASUBUHI

Kikao cha Bunge kitaendelea mara baada ya kamati iliyoundwa kupitia mapendekezo kusimamia maridhiano baina ya Wabunge wa UKAWA na wa Chama cha Mapinduzi kufikia muafaka na maazimio hayo kusomwa Bungeni  majira ya saa kumi jioni.

 Baada ya maridhiano yatatolewa mapendekezo ya maazimio "formulation" dhidi ya wote waliohusika na sakata hili la miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow ili yapigiwe kura na bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.Update Nov 28/11/2014

VITHIBITISHO VYA ALIYEKUWA KATIBU/MWANASHERIA WA TANESCO.DONDOO MUHIMU KIKAO CHA 28/11/2014 JIONI(kwa hisani ya JAMII FORUMS)

Kigwangalla: Sijawahi kuona Profesa muongo kama Muhongo
Kigwangalla: Toka lini pesa za watu binafsi zikawekwa Benki Kuu?

Mpina: Ni bahati mbaya tuna Profesa muongo kama Muhongo ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini
Mpina: Pesa zilizotolewa hazijalipwa kwa mmiliki halali wa IPTL, PAP sio wamiliki halali!
Mpina: Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliingilia majukumu ya TRA ktk kukusanya kodi

Zitto: Nimekuwa na mgogoro na chama changu lkn kwenye hili wameniunga mkono, kwa mara ya kwanza nimehudhuria kikao cha UKAWA
Zitto: Kuna baadhi ya wajumbe wanadai tumetumwa na Uingereza. Hakuna kinachonituma kufanya haya, ni uzalendo kwa nchi yangu
Zitto: Mahakama ilikiri kuwa kweli tulikuwa overcharged; ikaamriwa yafanywe mahesabu upya!
Zitto: Prof. Muhongo alisema anaheshimu mahakama za ndani. Jaji utamwa hakuwa anaamua kesi ya Escrow wala Capacity Charges
Zitto: Jaji hakusema kokote kuwa toeni hela mkawape IPTL. Hakuna sehemu alikotaja kitu kama hicho
Zitto: Kama TANESCO ina madeni makubwa na haina hela; Tanzania ina deni kiasi gani la Taifa? Basi tumeshauzwa!
Zitto: Muhongo alikuta TANESCO ikiwa na hasara ya Bil 43. Sasa TANESCO ina deni la zaidi mara 4!
Zitto: TRA wamegundua fraud kwamba nyaraka za PAP zilikuwa forged! Nchemba ameonesha ukomavu ktk hili
Zitto: Hivi watanzania tumefikia hatua ya kuukata utanzania kabisakabisa?
Zitto: Prof. Muhongo anadai yeye hahusiki na mambo ya makampuni. Sheria iliyotungwa mwaka 2012 haisemi hivyo!

Umeme umekatika Bungeni, wabunge wanashangilia!
Zitto: Kijana aliyesema Singh ni tapeli ametengenezewa kesi ya mauaji. Alifukuzwa kazi! Naomba apatiwe ulinzi
Zitto: Prof. Tibaijuka aliniandikia mchango wake wa maandishi kuelezea alivyopata fedha; tunawaachua Kamati ya Maadili
Zitto: System ili-collapse wakati wa mchakato wa uhamishaji wa mabilioni haya
Zitto: Tuhuma zikiachwa bila kufanyiwa uchunguzi watu huziamini. Naomba tuhuma za Lusinde kwangu zifanyiwe uchunguzi
Zitto: Naomba wanaonishughulikia wanishughulikie mimi; mwacheni mamangu apumzike (anatokwa machozi)

Kafulila: Tusiache kujadili kifo cha Waziri Mgimwa kisa mwanae hataki; kuna siku Rais atakufa na mwanae atataka tusichunguze

Chenge: Naomba neno KUFA listumike bali litumike neno KUFARIKI linakuwa na staha kidogo
Pendekezo la Serikali kumkamata Harbinder Singh Sethi kwa money laundering limekataliwa na Serikali hadi kesi iliyopo iishe

Lissu: Sethi akamatwe. Shauri lililopo mahakamani ni shauri la baadae! Akamatwe kwa sababu jinai kubwa imefanyika
Lissu: Pendekezo hili la serikali naomba wabunge wasilikubali; mtu huyu ahukumiwe kwa jinai
Simbachawene anapendekeza Sethi asikamatwe kama ilivyopendelezwa na Serikali; wabunge wanazomea

Mdee: Si ajabu kwa mtu mmoja kuwa na kesi ya jinai na kesi ya madai. Huyu Sethi afunguliwe kesi ya jinai
Halima Mdee: Kilicholetwa na Serikali ni ovyo, kinalinda wezi (kutaka Sethi asikamatwe mara moja)
Pindi Chana: Wa kukamatwa si Sethi peke yake; vyombo vya dola vifanye uchunguzi kwanza kubaini jinai iliyofanywa

Zitto: PCCB na TRA wameshafanya uchunguzi; mnataka vyombo gani vingine vifanye uchunguzi?

Werema: Eneo hili ndo litaleta mgongano mkubwa kati ya Bunge na Mahakama. Kwa sasa ni vigumu kusema "mkamate"

Makinda: Mnaposema akamatwe mnakosea, sisi siyo mahakama, tutafute njia nyingine na tuweke lugha ya kwetu siyo ya mahakama

MAAZIMIO

Pendekezo la kwanza la kumkamata na kumfilisi bwana Seth lina marekebisho ya serikali, naibu waziri wa Sheria anasema haiwezekani

Pendekezo la pili kuhusu Rugemalira, serikali imeweka marekebisho kuhusu uhalali wa pesa za Rugemalira alizogawa


Azimio la TATU limerekebishwa kuwa waliopokea pesa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua mahususi kwa mujibu wa sheria

Pendekezo la NNE. Kamati inazitaka mamlaka kuzitangaza benki za Mkombozi na Stanbic kama asasi za utakatishaji fedha
Azimio la 4 limepita kwamba Kamati inazitaka mamlaka husika ikiwemo benki kuu kuchukua hatua dhidi ya benki zote zilizohusika

Azimio la TANO: Serikali ipitie upya mikataba yote ya umeme na kutoa taarifa kabla ya kumalizika kwa Bunge la bajeti lijalo

Azimio la SITA: kuhusu Bodi ya TANESCO kuvunjwa kwa kusababisha pesa kuchotwa na hasara, serikali imekataa, mjadala unaendelea
Kingwangala: Kanuni zetu zinataka mtu yoyote anayetaka mabadiliko ya maazimio lazima awe amekawasilisha kabla

Kafulila: Kwa mujibu wa mkataba wa IPTL, maamuzi ya mwisho yanafanywa na mahakama ya London, bodi walikuwa na maamuzi hayo na haikuwajibika na maamuzi ya mahakama za ndani ya nchi

Majibu: ISCD ilisharidhia injuction ya mahakama ya Tanzania na ikaijulisha standard charted hivyo si sahihi kusema ISCD ina mamlaka ya mwisho, IPTL pia ilipata injuction kwenye mahakama za Tanzania
IPTL sio kampuni ya kimataifa tena bali kampuni ya ndani

Mdee: Bodi ya TANESCO, napendekeza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi vitendo vya jinai na kuchukua hatua kwa bodi ya TANESCO

Mbowe: Kazi yote hii pengine tusingefika hapa kama bodi ingekua makini, bodi ya TANESCO haiwezi kukwepa lawama hii. Bodi ya TANESCO iwajibishwe

Lissu: Maneno ya Mdee yanahusu jinai, ishu ni bodi ya TANESCO, (Anapendekeza bunge livunje bodi ya TANESCO ivunjwe na iundwe upya kuongeze ufanisi.

Shekifu: Tusifike mahala bunge likatoa amri lakini kutekeleza shughuli pia tuna mihimili mitatu, bunge linaishauri tu serikali na bunge haliwezi kuivunja bodi ya TANESCO
Azimio hili ni la bunge hivyo tuepuke kuvunja katiba

Zitto: Bunge linaelekeza kwamba bodi ya TENESCO liundwe upya maana taasisi zote zimeshachunguza kama TAKUKURU na nyinginezo

Maelekezo ya Lissu yanapitishwa na wabunge

Azimio la Saba: Kamati imethibitisha katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini amefanya uzembe pia amesaidia pesa za Escrow akaunti kulipwa kwa asiyestahili, kamati inashauri uteuzi wake utenguliwe mara moja.

Waziri: Maswala yote yatachukuliwa hatua baada ya uchunguzi.

Kafulila: Halina mabadiliko na kama ni uchunguzi umeshafanywa na CAG na TAKUKURU, bunge kama chombo kinachoisamamia serikali libaki na meno yake ya kuisamamia serikali.

Simbachawene: Katibu mkuu ni mtumishi wa umma, na mwenye mamlaka nae ni raisi wa jamhuri hivyo bunge haliwezi.
Nagu: Nakubalianana uzito wa jambo, watendaji wa serikali wanawajibika kweli lakini wana haki zao, mamlaka husika waangalie na wachukue hatua.

Sendeka: Kamati inapendekeza uteuzi utenguliwe na TAKUKURU wamfikisha mahakamani, sisi tumeshauri na watu ambao tuna mamlaka nao ni waziri mkuu na raisi.

Zitto: Taarifa kwa waziri, taarifa hii inaweza kutumiwa na vyombo vya sheria.

Sakaya: Sio ikithibitika kwani kwa taarifa zilizopo imeshabitika

Suzan Lymo: Kwa uchunguzi ambao umeshafanyika, katibu mkuu huyu ana matatizo kwa sababu PAC na CAG ameshaonyesha

Vyombo vya kiuchunguzi viendelee kufanye uchunguzi

Lissu: Bunge litofautishe maswala la kijinai na mendine sio ya kijinai kama kutengua uteuzi. Wapo wanaolindwa na sheria, lakini wapo wanaoserve kwa mamlaka ya raisi hauwezi ukasema wana protection ya kisheria. Tunaomba nipendekeze bunge linaazima na sio kupendekeza.

Zitto anapendekeza katibu mkuu asimamishwe kupisha uchunguzi.
Wasira: Lazima tukubali nchi inaendeshwa na mihimili mitatu, juzi tulipata tatizo la mahakama kuzuia bunge na sisi pia bunge tusiingilie serikali.

Mchangiaji: Uchunguzi utafanyikaje wakati watu wako kazini?

Werema: Mimi ndiye niliyemshauri Katibu Mkuu Maswi kushughulikia fedha, ninambeba hivyo shughulikeni na mimi

Imeshindikana kupita kwa azimio la saba, Spika kaamua waendelee na azimio la nane, watarudi kupiga kura mwishoni.

Azimio la nane: Bunge limemuondoa Naibu Waziri wa Nishati Masele kwenye mapendekezo kwa kuwa hana hatia ya kuadhibiwa

Azimio la tisa: Linajadiliwa kuhusu kutengua uteuzi wa Waziri Prof Muhongo lakini upande wa serikali imekataa

Bunge halina mamlaka ya kumwambia raisi atengue baada ya Lissu kulitaka bunge kutengua uwaziri wa Muhongo.

Mbaruku: Bunge kazi yake ni kushauri na bunge haliwezi kuwa messenger. (Anashauri anavyoona)
Muhongo ameshutumiwa amedanganya bunge lakini hamna popote iliposemwa fedha hizi ni za umma moja kwa moja. Hivyo nashauri versin ya muheshimiwa Chenge.


Shaha: Tunachohitaji ni lugha nzuri bila kudharau muhimili mwingine. Tuhoji na tumalize na tuulize wanaoafiki Lissu au Chenge.

Zitto: Akili yangu imechoka kidogo hivyo sina pendekezo.

Mbowe: Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi.

Baadhi ya wabunge wanasema wezi waondoke...

Sendeka: Naomba tukae na tujenge hoja, (Kelele zinaendelea)


SPIKA ANAAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE MPAKA WASHAURIANE TENA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AKAUNTI YA VIP ENGINEERING AND MARKETING ILIYOPO KATIKA BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI

Utangulizi


Taarifa hii inatolewa kwa umma kutokana na ripoti mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mitandao ya kijamii na taarifa iliyotolewa kwenye mjadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ufunguzi wa akaunti ya VIP engineering and Marketing (VIP)

Kampuni ya VIP engineering and Marketing ni kampuni ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kampuni hii ilifungua akaunti katika benki ya biashara ya Mkombozi na hivyo kuwa moja kati ya wateja wa benki. Benki ilijiridhisha na ilizingatia taratibu zote za ufunguzi wa akaunti husika kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni zinazozitaka benki kupata nyaraka muhimu kutoka kwa mteja wakati wa ufunguzi wa akaunti hiyo.
Nyaraka hizo ni pamoja na kuwepo kwa cheti cha usajili wa kampuni, kanuni za kampuni, idhinisho la kampuni kumruhusu moja kati ya wanahisa wake kuendesha akaunti pamoja na picha na hati ya kusafiria ya mhusika wa kuendesha akaunti hiyo.

2.0 Mauzo ya hisa za VIP

Kampuni ya VIP ilileta mkataba kwenye benki ya Mkombozi wa mauziano ya hisa za asilimia 30 baina ya VIP na kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP) ambazo inamiliki katika kampuni ya IPTL. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 19 Ogasti, 2013. Bei ya asilimia 30 ya hisa hizo ilikuwa ni dola za Marekani milioni 75. Katika kifungu namba 2.4 cha mkataba wao kinaelekeza fedha za mauzo ya hisa zilipwe kwenye akaunti ya VIP iliyopo benki ya Mkombozi. Mkataba huo wa mauziano ya hisa baina ya kampuni hizi mbili ulitambuliwa na hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa na Jaji J.H.K Utamwa tarehe 5 Septemba, 2013.
3. Mchakato wa kulipa kodi ya serikali

Benki ilitambua kwamba katika mauziano hayo ya hisa ni lazima kodi ya Serikali ilipwe na hivyo iliizishauri pande zote mbili kupeleka mkataba husika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufanyiwa makadirio ya kodi husika. Tarehe 20 Januari, 2014 TRA iliiandikia barua kampuni ya VIP na nakala ya barua hiyo kuletwa kwenye benki ya Mkombozi. Katika barua hiyo TRA iliitaarifu kampuni ya VIP kuwa makadirio ya kodi yatokanayo na mauzo ya hisa ni shilingi 38,186,584,322.00 ikiwa ni kodi ya mauzo ya hisa ya asilimia 30 za mauzo ya hisa kutoka VIP kwenda kwa PAP.(Capital gains and stamp duty).

TRA pia iliiagiza benki ya Mkombozi kuhakikisha kuwa inalipa kodi hiyo kwa niaba ya VIP mara tu fedha zitakapoingia kwenye akaunti yake.

Malipo ya kodi ya shilingi 38,186,584,322.00 yalilipwa TRA kwenye akaunti 11120100 iliyopo katika Benki Kuu ya Tanzania na TRA ilikiri kupokea kodi hiyo kwa barua yake yenye kumbukumbu namba 3-4/100/100/223/4 ya tarehe 24 Januari, 2014.
4. Ufafanuzi wa mambo mbalimbali

4.1 Benki ya mkombozi kuhusika katika kusafisha fedha chafu
Fedha zote zilizoingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo kwenye benki ya Mkombozi zilitokana na mauziano ya hisa kati ya VIP na PAP kwa mkataba uliotambuliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Chanzo cha malipo hayo ni kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya PAP iliyopo katika benki ya Stanbic na kuingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo katika benki ya Mkombozi.

Fedha hizo zilihamishwa katika mafungu mawili. Fungu la kwanza ilikuwa ni shilingi 73,573,500,000.00 zilihamishwa kwa njia ya TISS kwa kumbukumbu namba 000000050720 ya tarehe 23 Januari, 2014 na fungu la pili ni dola za Kimarekani 22,000,000.00 zilihamishwa kwa TISS kwa kumbukumbu namba 000000050812 ya tarehe 23 Januari, 2014. Malipo mengine ya asilimia kumi ya mauzo ya hisa yalilipwa kwenye akaunti ya Mkombozi iliyopo Benki Kuu ya Tanzania. Kutokana na mchakato huo benki ya Mkombozi ilijiridhisha kuwa fedha hizo ni malipo halali na siyo fedha chafu.

Benki ya Mkombozi haijihusishi na utakasishaji wa fedha chafu na haramu katika uchumi wa Tanzania.
4.2 Malipo yatokanayo na akaunti ya VIP

Malipo toka kwenye akaunti ya mteja hufanywa kutokana na maelekezo ya mteja. Benki ikishajiridhisha kuwa fedha ya mteja ni halali na ipo kwa mujibu wa sheria na hamna zuio lolote toka katika mahakama hapa nchini hutekeleza malipo kwenye akaunti ya mteja kutokana na maelekezo yake.

Benki ilijiridhisha kuwa malipo yote yaliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya VIP ni halali kwa kuwa chanzo cha pesa hizo ilikuwa ni halali kutokana na mauzo ya hisa na ulipwaji wa kodi ya Serikali kama ilinyoelezwa hapo juu. Kutokana na sababu hiyo benki haikuwa na shaka juu ya malipo hayo.

4.3 Malipo taslimu kwa wateja na kubeba fedha kwenye viroba, mifuko ya rambo na magunia

Benki inatoa tamko kuwa malipo yote yaliyofanywa katika akaunti ya VIP yalilipwa kupitia akaunti za walipwaji. Hakuna fedha zilizolipwa taslimu kwa wateja na kubebwa kwenye viroba au magunia kama ilivyoripotiwa Bungeni. Pesa iliyotoka kwenye akaunti ya VIP tarehe 6 Februari, 2014 kiasi cha shilingi 3,314,850,000.00 ililipwa kwenye akaunti nane za wateja tofauti na siyo kubebwa kwenye viroba au magunia.

Na zile zilizotoka toka benki ya Stanbic zilizotajwa hapo juu zilitumwa kwa njia ya TISS na siyo kubeba kwenye magunia au viroba.
4.2 Malipo yatokanayo na akaunti ya VIP

Malipo toka kwenye akaunti ya mteja hufanywa kutokana na maelekezo ya mteja. Benki ikishajiridhisha kuwa fedha ya mteja ni halali na ipo kwa mujibu wa sheria na hamna zuio lolote toka katika mahakama hapa nchini hutekeleza malipo kwenye akaunti ya mteja kutokana na maelekezo yake.

Benki ilijiridhisha kuwa malipo yote yaliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya VIP ni halali kwa kuwa chanzo cha pesa hizo ilikuwa ni halali kutokana na mauzo ya hisa na ulipwaji wa kodi ya Serikali kama ilinyoelezwa hapo juu. Kutokana na sababu hiyo benki haikuwa na shaka juu ya malipo hayo.

4.3 Malipo taslimu kwa wateja na kubeba fedha kwenye viroba, mifuko ya rambo na magunia

Benki inatoa tamko kuwa malipo yote yaliyofanywa katika akaunti ya VIP yalilipwa kupitia akaunti za walipwaji. Hakuna fedha zilizolipwa taslimu kwa wateja na kubebwa kwenye viroba au magunia kama ilivyoripotiwa Bungeni. Pesa iliyotoka kwenye akaunti ya VIP tarehe 6 Februari, 2014 kiasi cha shilingi 3,314,850,000.00 ililipwa kwenye akaunti nane za wateja tofauti na siyo kubebwa kwenye viroba au magunia.

Na zile zilizotoka toka benki ya Stanbic zilizotajwa hapo juu zilitumwa kwa njia ya TISS na siyo kubeba kwenye magunia au viroba.
Wito kwa umma
Benki ya Mkombozi inachukua fursa hii kuwatarifu wateja wake na umma kutopotoshwa na taarifa au tuhumma zilizofafanuliwa hapo juu na kuwataka wateja wake wote kutokuwa na hofu yeyote kwani benki ipo imara na inafanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania. Benki inawataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kutoyumbishwa na tuhumma hizo ambazo hazina ukweli ndani yake na badala yake waitumie benki yao kwa shughuli za maendeleo ya nchi yetu.

Pamoja tunajenga nchi na uchumi wa nchi yetu.
Hitimisho

Benki ya biashara ya Mkombozi haijihusishi na haitajihusisha na utakasishaji wa fedha chafu.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI

KIKAO CHA CCM
Kikao cha CCM kimeitishwa mchana huu baada ya mapumziko ya bunge.

Tayari makamu wa rais ameshafika na viongozi waambata wote wa CCM, kinafanyika ukumbi wa White House.

Jambo la kuhashiria kuwa huenda jioni kukawa na breaking news ni kuwa tayari gari binafsi ya waziri mkuu yenye namba za usajiri T 164 AKF aina ya range rover imeshawasili eneo hili sambamba na familia yake.

Habari zilizozagaa toka kwa wabunge hapa ni kuwa jaribio la jana la kuwatuliza wabunge wa CCM limekwama kulingana na michango ya wabunge asubuhi, Sasa wamepanga mbinu mbili, moja ni kushinikiza bunge liiagize serikali ifanye uchunguzi kupitia ripoti ya CAG, PCCB na mapendekezo ya PAC na kisha bunge lijalo mwakani Feb 2015 serikali ije na majibu.

Na mbinu ya pili ni kukubali yaishe watu wawajibike leo leo.

Update Nov 27/11/2014


MAELEZO YA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA “ESCROW” YA TEGETA PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL

 Historia ya Mradi

Mheshimiwa Spika, Katika miaka ya tisini (1990s), Tanzania ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hali iliyopelekea kuwepo kwa upungufu wa umeme na kuathiri shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali ilichukua hatua za dharura za kuanzisha mradi wa kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha Megawati (MW) 100.

Upatikanaji wa IPTL
Mheshimiwa Spika, Mwaka 1994 Serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni za VIP Engineering and Marketing Ltd ya Tanzania iliyokuwa na  Asilimia 30 na MECHMAR Corporation ya Malaysia (MECHMAR) iliyokuwa na Asilimia 70. Kampuni ya IPTL ilipewa leseni ya kujenga, kumiliki na kuendesha (Build-Own-Operate) Mtambo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 100 kwa kutumia mafuta mazito eneo la Tegeta-Salasala, Dar Es Salaam.

Katika Ukurasa wa 52 Aya ya 2, ya Taarifa ya PAC, Kamati imependekeza Mtambo huo utaifishwe.

Ufafanuzi:
Mheshimiwa Spika, Kulingana na Mkataba wa PPA kati ya TANESCO na IPTL, majukumu ya IPTL yalikuwa ni kujenga, kumiliki na kuendesha (Build, Own and Operate – BOO). Hivyo, kutaifisha Mtambo huo ni kukiuka makubaliano katika Mkataba wa PPA wa tarehe 26 Mei 1995, ukiukwaji wa aina hii ukitokea unaweza kuingiza Serikali katika mgogoro mkubwa ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwenye Mahakama za kibiashara za kimataifa. Aidha utaifishaji wa miradi ya uwekezaji binafsi  itakuwa ni njia ya kufukuza wawekezaji  binafsi
Mheshimiwa Spika, Tarehe 26 Mei, 1995, TANESCO na IPTL walisaini Mkataba wa PPA kwa muda wa miaka ishirini (20), kwa ajili ya kununua umeme utakaozalishwa na IPTL. Kwa mujibu wa Mkataba huo, IPTL ilitakiwa kuiuzia TANESCO umeme usiopungua Asilimia 85 ya uwezo wa Mtambo (minimum off take). Hata hivyo, uzalishaji wa umeme haukuanza mara moja kutokana na mgogoro uliotokea kati ya TANESCO na IPTL kuhusu gharama halisi za uwekezaji na namna ya kukokotoa Capacity Charges. Hivyo, IPTL ilianza kuzalisha umeme tarehe 15 Januari, 2002. Kutokana na hali hiyo muda wa miaka 20 ya Mkataba ulianza kuhesabiwa tarehe 15 Januari, 2002 baada ya kuanza uzalishaji (Commercial Operation Date).

Mheshimiwa Spika, Pamoja na mambo mengine muhimu yaliyokuwemo katika PPA, Kifungu Na. 6 cha Mkataba huo kinaipa TANESCO wajibu wa kulipa malipo yaliyotajwa hapo juu na kwamba endapo kutakuwa na mgogoro wowote kuhusiana na malipo hayo (Disputed Amount), itafunguliwa Akaunti maalum (Escrow Account) ya kuhifadhi fedha hizo hadi pale pande mbili zitakapokubaliana juu ya uhalali wa malipo yanayobishaniwa. Aidha, chini ya PPA, migogoro yote kuhusiana na masuala ya utekelezaji wa Mkataba huo ilitakiwa kuwasilishwa na kuamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) ya London. Hivyo, ilikuwa ni jukumu la kila mhusika katika Mkataba huu kuwasilisha malalamiko yake ICSID yanapotokea.
Katika Ukurasa wa 8 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa mwaka 2004 TANESCO ilifungua shauri la ICSID 2 kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya Capacity Charge.

Ufafanuzi

Mheshimiwa Spika, Taarifa hiyo siyo kweli. TANESCO haijawahi kufungua shauri lolote ICSID ya London au Mahakama yo yote dhidi ya IPTL kupinga kiasi kikubwa cha Capacity Charge kama inavyoelezwa katika Taarifa ya PAC. Shauri la ICSID 2 lilifunguliwa tarehe 31 Oktoba 2010 na Standard Chatered Bank Hong Kong (SCBHK) kwa ajili ya kudai malipo ya deni ililonunua kutokana na mkopo uliotolewa na mabenki ya ushirika ya Malaysia kwa IPTL.  Wahusika katika Shauri hilo la ICSID 2 ni SCBHK na TANESCO na wala siyo TANESCO na IPTL.

Mheshimiwa Spika, tarehe 12 Februari, 2014 ICSID ilitoa uamuzi kuhusiana na Shauri la SCBHK na TANESCO na kuwashauri wakae kukokotoa upya malipo ya Capacity Charge. Hata hivyo, ilikuwa vigumu kwa pande hizo kutekeleza uamuzi huo kutokana na pande hizo kutokuwa na Mkataba wa kibiashara baina yao. Vile vile, kupitia Shauri la Madai Na. 60/2014, lililofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania na IPTL tarehe 4 Aprili, 2014 ilizuia utekelezaji wa maelekezo hayo.
Mgogoro kati ya IPTL na TANESCO

Mheshimiwa Spika, Migogoro kati ya TANESCO na IPTL ilianza muda mfupi baada ya PPA kusainiwa tarehe 26 Mei, 1995. IPTL waliitaka TANESCO wakubaliane bei za kununua umeme kwa kuzingatia gharama za uwekezaji. Pande hizo mbili zilishindwa kukubaliana gharama za Capacity Charge kwa vile TANESCO walidai kuwa gharama zilizoainishwa na IPTL ni kubwa kuliko gharama halisi za uwekezaji. Mwaka 1998, TANESCO iliajiri Kampuni ya Mawakili ya Mkono & Co. Advocates kutoa huduma za kisheria kwa kushirikiana na Huntons & Williams ya Marekani. Kutokana na tofauti za gharama za Uwekezaji, Mawakili hawa waliishauri TANESCO ifungue Kesi ICSID nchini Uingereza dhidi ya IPTL ili kupinga gharama hizo.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia ushauri huo wa Mawakili, TANESCO ilifungua Kesi Na.ARB/98/8 ya Mwezi Agosti, 1998 ikidai kuwa gharama halisi za uwekezaji ni Dola za Marekani milioni 90 na siyo milioni 163.53 kama ilivyodaiwa na IPTL. Aidha, IPTL ilidai kuwa kiwango cha marejesho ya uwekezaji (Internal Rate of Return-IRR) ni Asilimia 23.10 ambacho pia kilipingwa na TANESCO.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 12 Julai, 2001, ICSID ilitoa uamuzi wa Kesi hiyo pamoja na mambo mengine kwamba:-

Gharama halisi za uwekezaji zikiwemo Mtambo na nyumba za wafanyakazi wa IPTL zilizoainishwa katika hesabu ya IPTL zilikuwa ni Dola za Marekani milioni 163.53 lakini ICSID iliona kuwa gharama halisi ni Dola za Marekani milioni 127.20;
Mgogoro kati ya IPTL na TANESCO

Mheshimiwa Spika, Migogoro kati ya TANESCO na IPTL ilianza muda mfupi baada ya PPA kusainiwa tarehe 26 Mei, 1995. IPTL waliitaka TANESCO wakubaliane bei za kununua umeme kwa kuzingatia gharama za uwekezaji. Pande hizo mbili zilishindwa kukubaliana gharama za Capacity Charge kwa vile TANESCO walidai kuwa gharama zilizoainishwa na IPTL ni kubwa kuliko gharama halisi za uwekezaji. Mwaka 1998, TANESCO iliajiri Kampuni ya Mawakili ya Mkono & Co. Advocates kutoa huduma za kisheria kwa kushirikiana na Huntons & Williams ya Marekani. Kutokana na tofauti za gharama za Uwekezaji, Mawakili hawa waliishauri TANESCO ifungue Kesi ICSID nchini Uingereza dhidi ya IPTL ili kupinga gharama hizo.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia ushauri huo wa Mawakili, TANESCO ilifungua Kesi Na.ARB/98/8 ya Mwezi Agosti, 1998 ikidai kuwa gharama halisi za uwekezaji ni Dola za Marekani milioni 90 na siyo milioni 163.53 kama ilivyodaiwa na IPTL. Aidha, IPTL ilidai kuwa kiwango cha marejesho ya uwekezaji (Internal Rate of Return-IRR) ni Asilimia 23.10 ambacho pia kilipingwa na TANESCO.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 12 Julai, 2001, ICSID ilitoa uamuzi wa Kesi hiyo pamoja na mambo mengine kwamba:-

     Gharama halisi za uwekezaji zikiwemo Mtambo na nyumba za wafanyakazi wa IPTL zilizoainishwa katika hesabu ya IPTL zilikuwa ni Dola za Marekani milioni 163.53 lakini ICSID iliona kuwa gharama halisi ni Dola za Marekani milioni 127.20;
Katika Ukurasa wa 11 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC, imeelezwa kuwa mtaji wa uwekezaji katika Mtambo wa IPTL ni Shilingi 50,000/= na kwamba huo ndio ungetumika kukokotoa Capacity Charges ili kulipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa.

Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, Maelezo hayo siyo sahihi. Ukweli ni kwamba kutokana na maamuzi ya ICSID 1 ya tarehe 12 Julai, 2001, gharama za ujenzi wa Mtambo wa Tegeta ni Dola za Marekani 127.20 kama ilivyoelezwa katika Ukurasa wa 47 Aya ya 4 ya Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Katika Taarifa hiyo, pia imeelezwa kuwa ilikubalika kuwa uwiano wa deni na mtaji utakuwa 70:30. Hii ikiwa na maana kwamba, deni ni Dola za Marekani milioni 89.04 na mtaji ni Dola za Marekani milioni 38.16. Uamuzi huo haujabadilishwa na Mahakama yo yote au mtu ye yote.

Mheshimiwa Spika, tunakubaliana kwamba fedha iliyopokelewa kutoka Mabenki ya Ushirika ya Malaysia kama mkopo ni Dola za Marekani milioni 85.86. Kati ya Dola za Marekani milioni 105 zilizokuwa zimeidhinishwa. Swali la kujiuliza, je Mtambo huo ulikamilikaje kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 85.86, huku gharama halisi ya ujenzi wa Mtambo wa Tegeta ikawa Dola za Marekani milioni 127.20?

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba kuna matumizi ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 38.16 ambazo pia zimetumika kwenye uwekezaji. Taarifa ya Kamati ya PAC haikuonesha fedha hiyo kuwa sehemu ya uwekezaji.
Mheshimiwa Spika, Tarehe 30 Juni, 2004, Kampuni ya Mawakili iliyokuwa ikiiwakilisha TANESCO katika kesi ya kwanza ya usuluhishi, Kampuni ya Mkono & Co Advocates, iliishauri TANESCO iendelee kupinga kiwango cha malipo ya Capacity Charge kilichokuwa kimeafikiwa tarehe 12 Julai, 2001 na pande hizi mbili katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID) ya London. Hii ilikuwa ni miaka miwili tu baada ya usuluhishi uliochukua miaka minne kukamilika na Mtambo kuanza kuzalisha umeme tarehe 15 Januari, 2002.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, baada ya ushauri huu, Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates) hawakuishauri TANESCO ifungue kesi katika Mahakama za Tanzania wala katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kimataifa (ICSID) ya London.

Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia tarehe 5 Septemba, 2013 wakati Mheshimiwa Jaji Utamwa anatoa hukumu yake juu ya mgogoro wa WanaHisa wa IPTL hapakuwepo na kesi yo yote  kwenye Mahakama yo yote ya kupinga gharama za Capacity Charge kati ya TANESCO na IPTL, iwe katika Mahakama za ndani au za nje. Kwa kutokuwepo Msuluhishi (Broker) katika suala hili, madai yo yote ya TANESCO yanakuwa ni madai ya upande mmoja ambayo kisheria hayawezi kuchukuliwa kuwa ndiyo madai halisi.  Kwa sababu hiyo haikuwepo formula rasmi ya kuutatua mgogoro huo zaidi ya majadiliano na maafikiano kati ya pande mbili (TANESCO na IPTL).
 
Uuzaji wa Hisa za VIP
Mheshimiwa Spika, Kutokana na VIP Engineering and Marketing Limited (VIP) kuona kuwa hainufaiki na ubia wake katika IPTL, ilikusudia kuuza Hisa zake kwa MECHMAR. Hata hivyo, MECHMAR haikuweza kununua Hisa hizo kwa sababu ilitaka thamani ya Hisa za VIP zitokane na ripoti ya ukaguzi ya mwaka (Audited Financial Report) na taratibu za kihasibu za kimataifa (International Accounting Rules), VIP haikukubaliana na utaratibu huo.
Mheshimiwa Spika, Kutokana na kutokubaliana, MECHMAR iliishauri VIP ifungue Shauri la madai hayo kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Uingereza (LCIA) kulingana na Mkataba wa Wanahisa wa IPTL. Hata hivyo, VIP haikufungua Shauri katika Mahakama ya usuluhishi kama ilivyoshauriwa na MECHMAR badala yake tarehe 25 Februari, 2002 VIP ikafungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Miscellaneous Civil Application No. 49/2002) ikiomba Kampuni ya IPTL ifilisiwe ikiwa ni mwezi mmoja tangu kuanza uzalishaji.

Uamuzi kuhusu Ufilisi wa IPTL
Mheshimiwa Spika, Shauri lililofunguliwa na VIP tarehe 25 Februari, 2002 liliendelea kuwa Mahakamani hadi ilipofika tarehe 16 Desemba, 2008. Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jaji Oriyo, J ilitoa uamuzi wa kuiweka IPTL katika Ufilisi wa Muda (Provisional Liquidation) chini ya Kabidhi Wasii Mkuu (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini - RITA). Mfilisi wa Muda alipewa majukumu maalum yafuatayo:
Kulinda mali zote za IPTL katika kipindi chote cha Ufilisi wa Muda; na

 Kufanya uchunguzi wa tuhuma zote zilizotolewa na VIP dhidi ya MECHMAR na kutoa ripoti za uchunguzi huo ili Mahakama iweze kutoa uamuzi.
Mheshimiwa Spika, Tarehe 15 Julai, 2011, Mahakama Kuu ya Tanzania (Kaijage, J) ilitoa uamuzi kwamba, IPTL iwekwe kwenye Ufilisi Kamili (Full Liquidation) na RITA ilithibitishwa kuwa Mfilisi wa IPTL.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Standard Chartered Bank Hong Kong (SCBHK) iliyokuwa imenunua deni la IPTL kutoka kwa DANHARTA, ilipinga na kuiomba Mahakama ya Rufaa ifanye mapitio ya uamuzi wa Mahakama Kuu (Application for Revision – Civil Revision No. 1/2012) ikiainisha dosari katika uamuzi wa Mahakama Kuu ulioamuru kufilisiwa kwa IPTL. SCBHK ilibainisha dosari za maombi ya kutaka IPTL kufilisiwa kwa kuwa maombi ya SCBHK ya kutaka Mahakama iteue msimamizi (Administrator) wa kuisimamia IPTL (kwa niaba ya SCBHK) yalikuwa hayajasikilizwa.
Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilikubaliana na hoja za SCBHK na hivyo kuamuru shauri hilo lirejeshwe Mahakama Kuu ili IPTL irudi mikononi mwa Mfilisi wa Muda (Provisional Liquidator) ambaye alipewa majukumu yafuatayo:-

    Kukusanya mali na madeni yote ya IPTL;

Kupokea na kusajili madeni yote dhidi ya IPTL;

Kusuluhisha migogoro kati ya wanahisa wa IPTL; na    Kusimamia na kuendesha Mtambo wa kuzalisha umeme wa IPTL kwa niaba ya IPTL.

Mheshimiwa Spika, Baada ya kuteuliwa, Mfilisi wa Muda (Provisional Liquidator) alifanya juhudi ya kumaliza mgogoro huo wa IPTL nje ya Mahakama kwa kushirikisha wadau mbalimbali (Stakeholders) wa IPTL kupitia kikao chake cha tarehe 9 Novemba, 2011. (Kiambatisho Na.1). Juhudi hizo hazikufanikiwa na ikalazimu shauri liendelee Mahakamani.

 Uhalali wa uhamishwaji wa Asilimia 70 za Hisa za
MECHMAR kwenda PAP
Mheshimiwa Spika, Suala la uhalali wa umiliki wa Hisa katika Kampuni hizi linahusu wanahisa wa Kampuni wenyewe. Serikali haiwajibiki kuingilia mahusiano ya kibiashara ya wanahisa katika Kampuni Binafsi. Hata hivyo, kulingana na Sheria za nchi ikiwa ni pamoja na Kifungu cha 172 cha Sheria ya Makampuni (Sura 212), mauziano ya Hisa yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu, endapo usajili wa Hisa hizo utafanyika hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa za BRELA za tarehe 31 Desemba, 2013, zinaonesha kuwa uhamishaji wa Hisa 7 za MECHMAR katika IPTL kwenda PAP ulisajiliwa hapa nchini. Kwa maana hiyo, PAP ni mmiliki wa Asilimia 70 za IPTL.

Katika ukurasa wa 44 Aya ya 1 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa PAP siyo mmiliki halali wa Hisa 7 za MECHMAR katika IPTL.

Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, katika maelezo ya Kamati ukurasa wa 30, Kamati imethibitisha kwamba nyaraka za mauziano kati ya MECHMAR na Piper Link zilipokelewa na Harbinder Singh Sethi ambaye pia ndiye mmiliki wa PAP. Kwa uthibitisho huo, Kamati inakubali kuwa Hisa za MECHMAR katika IPTL zinamilikiwa na PAP.
Katika Ukurasa wa 25 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa hakuna ushahidi wa PAP kumiliki Asilimia 70 ya Hisa zilizokuwa zikimilikiwa na MECHMAR katika IPTL.

Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa umiliki wa Hisa 7 za IPTL unatambuliwa hata na SCBHK ambayo ilisaini makubaliano tarehe 25 Novemba, 2011 na PAP ya kulipwa deni la mkopo wa fedha za kununua deni la ujenzi wa Mtambo wa Tegeta. Kiambatisho Na 2.

Majadiliano ya mikopo ya IPTL na Wadai
Mheshimiwa Spika, Kutokana na Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa tarehe 5 Septemba, 2013, Kampuni ya PAP ilijadiliana na wadai halali wa mikopo ya IPTL na kuingia Mkataba wa kuwalipa wadai wote wa IPTL. SCBHK inayodai kuidai IPTL mikopo katika ujenzi wa Mtambo wa Tegeta haikuwasilisha madai ya aina yo yote ili iweze kulipwa.

Mheshimiwa Spika, Ukweli ni kwamba, SCBHK iliyokuwa ikiidai IPTL fedha ilizotumia kununua deni lililotokana na kufilisiwa kwa MECHMAR kule Malaysia (siyo Tanzania) haijawahi kujadiliana na IPTL kuhusu malipo ya mkopo wake kama upo. Mvutano huu unaendelea ICSID kati ya TANESCO na SCBHK, ukiitaka TANESCO ilipe gharama za kununua umeme ikijumuisha deni la IPTL. Madai ya SCBHK dhidi ya TANESCO yanatokana na madai ya kuwepo kwa Deed of Assignment ya MECHMAR kuhusiana na Mkopo wa IPTL ambapo Mtambo wa IPTL uliwekwa kama dhamana ya Mkopo.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo Deed of Assignment hiyo haikuwahi kusajiliwa hapa nchini kama inavyotakiwa katika Kifungu Na. 172 cha Sheria za Makampuni Sura. 212 zinavyoelekeza. Kutokana na kutokusajili Assignment Deed hiyo, SCBHK ilikosa sifa za kufungua madai yake hapa nchini badala yake ilifungua madai haya ICSID nchini Uingereza. Kitendo hicho kinaonesha kudharau Mahakama zetu na PAC inataka tuziamini Mahakama za nje kuliko za kwetu.

Jitihada za Makampuni mbali mbali kununua Hisa za VIP

Mheshimiwa Spika, Kutokana na tofauti zilizokuwepo kati ya MECHMAR na VIP kuanzia mwanzo wa mradi, VIP iliamua kuuza Hisa zake zilizoko IPTL kwa makampuni mbalimbali kwa nyakati tofauti ikiwemo MECHMAR kama mwanahisa mwenzake,  NSSF, Camel Oil, Great White Shark Opportunity Fund pamoja na SYMBION lakini haikuwezekana kutokana na kutoafikiana katika bei.

Mheshimiwa Spika, Baadaye VIP chini ya usuluhishi ya RITA, iliuza Hisa zake kwa PAP kwa thamani ya Dola za Marekani milioni sabini na tano (US$ 75,000,000/=). Ununuzi wa Hisa Asilimia 30 za VIP uliofanywa na PAP ndiyo uliyomaliza mgogoro wa Wanahisa uliyokuwa Mahakamani na kuufanya Mtambo wa IPTL kumilikiwa na PAP kwa kuwa ndiyo iliyomiliki Hisa zote Asilimia 100 za IPTL.
Taarifa ya PAC: Katika ukurasa wa 58 wa Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye aliyekuwa Dalali Mkuu aliyewakutanisha Bw. Harbinder Sethi na Bw James Rugemalira

Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, Taarifa hii siyo sahihi kwa kuwa tangu tarehe 9 Novemba, 2011, RITA aliitisha mkutano na kuwakutanisha wadau wote wa IPTL. Wakati huo, Waziri wa Nishati na Madini aliyeko sasa alikuwa bado hajateuliwa kwenye wadhifa huo.

   Kufungua ESCROW Akaunti

Mheshimiwa Spika, Tarehe 30 Juni, 2004, TANESCO kwa ushauri wa Mkono & Co Advocates walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme zilikokotolewa kwa kutumia IRR ya Asilimia 23.10 na makadirio ya gharama za mtaji wa Asilimia 30 ambao ni Dola za Marekani milioni 38.16, wakati mtaji halisi (equity) wa IPTL ni chini ya Dola za Marekani 100. Hivyo, TANESCO walikuwa wakitoa notisi (Dispute Notice) kwa kila Ankara ya malipo kupinga gharama hiyo kulingana na Kifungu Na. 6.8 cha Mkataba wa PPA. Kifungu hicho kinaeleza kuwa ikiwa upande wote haukubaliani na usahihi wa malipo katika Ankara zilizowasilishwa kwa ajili ya malipo ya gharama za umeme wanatakiwa watoe notisi (Invoice Dispute Notice) kwa upande mwingine. Vile vile, Mawakili wa TANESCO (Mkono & Co Advocates) walishauri kwamba kutokana na pingamizi hilo, ifunguliwe Akaunti Maalum (Escrow Account) kwa ajili ya kuhifadhi fedha ambazo zilitokana na Ankara zilizokuwa zinapingwa.
Mheshimiwa Spika, kutokana na ushauri wa Mkono Co. & Advocates tarehe 5 Julai, 2006, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilisaini Mkataba wa kufungua Akaunti Maalum (Escrow Account) kwa ajili ya kuweka fedha zote za Ankara zilizopaswa kulipwa kwa IPTL.
Mmiliki wa Fedha za Akaunti ya Escrow:

Mheshimiwa Spika, katika Taarifa ya Kamati ya PAC ukurasa wa 22 imeelezwa kuwa Akaunti ya Escrow ilipaswa kuwa na Shilingi bilioni 306.70 ambazo zingekuwa zimewekwa na TANESCO. Hata hivyo, katika mapendekezo ya Kamati ya PAC ukurasa wa 50, Kamati imeeleza kwamba imethibitisha bila chembe ya mashaka kwamba mchakato mzima wa kutoa fedha katika Akaunti ya Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kwamba Mfumo mzima wa Serikali ulipata ganzi ili kuwezesha zaidi ya Shilingi bilioni 306 kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kutakatishwa kupitia benki mbili hapa nchini.

Tahadhari iliyochukuliwa na Serikali wakati wa kutoa fedha kwenye akaunti ya Escrow

Mheshimiwa Spika, kwa kuelewa kwamba kunaweza kukatokea madai kwa IPTL, na kwa kuwa Serikali ilitoa dhamana kwa TANESCO ya kununua umeme wa IPTL, Serikali ilihakikisha inachukua KINGA (Indemnity) kutoka IPTL katika maeneo yote muhimu. Kwa mujibu wa KINGA hiyo, kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika. Ikumbukwe kuwa kabla ya kusaini, KINGA hiyo ilipitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuthibitisha kwamba inakidhi matakwa ya kulinda maslahi ya Taifa. KINGA hii ilitolewa tarehe 27 Oktoba, 2013. Inasema, nanukuu:
“IPTL do hereby agree to INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all present and future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or all losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the Tegeta Escrow Account or part thereof to IPTL pursuant to the Agreement for Delivery of Funds”.

KatikaUkurasa wa 48 wa Taarifa ya PAC, imeelezwa kuwa Serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha dhidi ya madai mengine yanayoweza kujitokeza kabla ya kutolewa kwa fedha kutoka akaunti ya Escrow.

Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, KINGA iliyochukuliwa inakidhi matakwa ya kisheria na imezingatia athari yo yote ambayo ingeweza kutokea baadaye kutokana na kutolewa kwa fedha katika Akaunti ya Escrow. Kwa hiyo siyo kweli kwamba Serikali haikuchukua tahadhari kama ilivyodaiwa na PAC.
. Dhana ya Madai ya Shilingi Bilioni 321

Mheshimiwa Spika, Madai ya kwamba TANESCO inaidai IPTL Shilingi bilioni 321 msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Shilingi za Tanzania 50,000/- kwa wakati huo. Dhana hii ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani milion 38.16 ziliwekezwa kwenye mradi wa Tegeta. Aidha, Bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai hayo ya Shilingi bilioni 321. Kimsingi hata Vitabu vya Hesabu vya TANESCO ambavyo vimekuwa vikikaguliwa na CAG, havioneshi kuwepo kwa deni hilo.

Mheshimiwa Spika, Madai ya Shilingi bilioni 321 yaliyowasilishwa kwa Mfilisi na Mwanasheria wa TANESCO (Mkono & Co. Advocates) ulihitaji kuhakikiwa kabla ya kukubaliwa na Mfilisi kama madai halali. Hata hivyo, uhakiki huo haukufanyika kwa sababu ya Hukumu ya Mahakama ya Rufaa katika Civil Revision No. 1 ya Mwaka 2012, ambayo ilifuta maamuzi ya Mahakama Kuu ya kuiweka IPTL katika Ufilisi na kuirudisha kwenye Ufilisi wa Muda. Hivyo, madai hayo ya Shilingi bilioni 321 na kiapo chake ambacho hakitambuliwi na Bodi ya TANESCO hayakuwa tena na uhalali wo wote.
Kamati ya PAC: Katika ukurasa wa 47 Aya ya 2 Kamati imejiridhisha kuwa madai ya TANESCO ya Shilingi Billioni 321 yana uhalali japo usahihi wake utapatikana baada ya kutekelezwa kwa uamuzi wa ICSID 2 na TANESCO na IPTL kukubaliana kiwango sahihi cha Capacity Charge.


Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, Madai ya kwamba TANESCO inaidai IPTL Shilingi bilioni 321 msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Shilingi za Tanzania 50,000/- kwa wakati huo. Dhana hii ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani milion 38.16 ziliwekezwa kwenye mradi wa Tegeta. Aidha, Bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai hayo ya Shilingi bilioni 321. Kimsingi hata Vitabu vya Hesabu vya TANESCO ambavyo vimekuwa vikikaguliwa na CAG, havioneshi kuwepo kwa deni hilo.

TANESCO na IPTL kufanya Reconcillation ya fedha iliyokuwa kwenye Akaunti ya Escrow

Mheshimiwa Spika, TANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki (reconciliation) tarehe 9 Oktoba, 2013 ili kujua madai halali ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Takwimu za Mfilisi wa Muda wa IPTL (RITA) wakati akikabidhi mali na madeni ya IPTL, ilionesha kwamba deni lote alilokuwa akidaiwa TANESCO na IPTL kama Capacity Charges ni Shilingi bilioni 370.70, sawa na Dola za Marekani milioni 224.30. Katika majadiliano kati ya TANESCO na IPTL, gharama zilizokubaliwa kama Capacity Charges zilizokuwa zinadaiwa ni Shilingi bilioni 275.20. Fedha hizi ni pungufu kwa Shilingi bilioni 95.50 ya madai ya IPTL. Hadi kufikia tarehe 25 Novemba, 2013, fedha iliyokuwa katika Akaunti ya Escrow ilikuwa jumla ya Dola za Marekani milioni 22.20, sawa na Shilingi bilioni 36.72 na Shilingi bilioni 161.39.

Mheshimiwa Spika, ukaguzi maalum umeonesha pia kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow wakati wa kuifunga ni Shilingi bilioni 182.77 na kuwa na upungufu wa Shilingi bilioni 123.90 wa madai ya IPTL.

Iwapo Serikali ilistahili kutoa fedha katika Akaunti  ya Escrow wakati Shauri la ICSID, London inaendelea.
Mheshimiwa Spika, Kesi iliyopo ICSID, London ilihusu madai ya Benki ya Standard Chatered ya Hong Kong yaliyotokana na kununua deni lililotokana na uwekezaji katika Mtambo wa IPTL wa Tegeta. Katika Mkopo huo, Mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na Mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta viliwekwa kama dhamana.

Mheshimiwa Spika, TANESCO haikuhusishwa kwenye majadiliano ya dhamana hiyo. IPTL ilishindwa kumaliza marejesho ya Mkopo huo na hivyo Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong kuanza kuidai TANESCO madeni yaliyotokana na Mkopo huo. Hata hivyo, fedha katika Akaunti ya Escrow ilitokana na Ankara za Capacity Charges zilizokuwa zikibishaniwa kati ya TANESCO na IPTL kuhusu viwango vilivyotumika kukokotoa malipo hayo na siyo mikopo ya IPTL.
Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, Standard Chartered Bank Hong Kong siyo mhusika (not a party) katika Mkataba wa tarehe 26 Mei, 1995 wa PPA kati ya TANESCO na IPTL. Kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, madai yo yote yaliyotokea nje ya nchi yakihusu uwekezaji ulioko nchini ni lazima yasajiliwe hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Kwa mantiki hiyo, Shauri lililoko ICSID, London halihusiani na fedha za Akaunti ya Escrow bali mikopo ya IPTL. Hata hivyo, wadai wa IPTL waliamriwa na Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 5 Septemba, 2013 kuwasilisha madai yao kwa PAP. Benki ya Standard Chatered ya Hong Kong haijafanya hivyo.


Ulipwaji wa Madai na Madeni

Mheshimiwa Spika, Kuhusu madai na madeni dhidi ya IPTL ikiwemo VAT, Serikali na BOT ziliitaka IPTL iweke KINGA (Indemnity) ili kuihakikishia Serikali kuwa endapo kutakuwa na madai au madeni ya aina yo yote, IPTL itawajibika kuyalipa. Tarehe 27 Oktoba, 2013, IPTL ilitoa KINGA hiyo, nanukuu:

“IPTL do hereby agree to INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all present and future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or all losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the Tegeta Escrow Account or part thereof to IPTL pursuant to the Agreement for Delivery of Funds”.

Gharama za Mawakili (Mkono & Co. Advocates na
Hunton & Williams ya Marekani) Katika Kuendesha Kesi za IPTL
Mheshimiwa Spika, Hadi Hukumu ya Mheshimiwa Jaji Utamwa inatolewa tarehe 5 Septemba mwaka 2013, TANESCO na Serikali zilikuwa zimewalipa Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) jumla ya Shilingi za Tanzania bilioni 62.90 na bado Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanaidai TANESCO Dola za Marekani milioni 4.50. Katika ushauri wao walikuwa wamependekeza kwa Serikali wapewe kazi nyingine ya kwenda kutetea Guarantee ya Serikali pamoja na kupinga Hukumu ya tarehe 12 Februari, 2014 iliyotolewa katika uamuzi wa ICSID-2. Ushauri wao upo katika Memorandum ya tarehe 9 Oktoba, 2013 waliyowasilisha TANESCO.

Mheshimiwa Spika, Wakati ambapo hatukujua ni kiasi gani Serikali na TANESCO ingeweza kupata kwa kuendelea kupinga Capacity Charges za IPTL, tunajua fika ni hasara gani tumepata kupitia malipo ya Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) yaani ya Shilingi bilioni 62.9 na bado wanadai Dola za Marekani milioni 4.5.

Mheshimiwa Spika, kumalizika kwa mgogoro huu wa IPTL si tu kwamba kumetuondoa kwenye hatari ya kuendelea kukamuliwa na Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) hawa bali pia katika mazungumzo yaliyofanywa kati ya TANESCO na IPTL tumeweza kuokoa takribani Shilingi bilioni 95 katika madai ya awali ya IPTL.
  Ushauri wa Mawakili (Mkono & Co. Advocates na
    Hunton & Williams) wa TANESCO wa Tarehe 4
    Oktoba, 2012

Mheshimiwa Spika, Mawakili wa TANESCO na Serikali yaani Kampuni za Mkono & Co Advocates na Hunton & Williams waliandika ushauri wa pamoja wa tarehe 4 Oktoba, 2012 ambapo walifafanua kwa kina juu ya Shauri lililokuwa likiendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID) ya London. Katika Ushauri wao walionyesha wazi kwamba TANESCO ilikuwa na nafasi finyu mno ya kushinda katika Kesi iliyokuwa ikiendelea kati ya TANESCO na SCBHK.

Mheshimiwa Spika, katika ushauri wao walieleza mambo muhimu ambayo ni vema Bunge lako Tukufu likayaelewa hasa kwa ajili ya watu wanaodhani kwamba ilikuwa ni makosa kwa TANESCO kukaa na IPTL baada ya Hukumu ya Mahakama Kuu ya tarehe 5 Septemba, 2013. Baadhi ya maeneo walioshauri TANESCO ikae na IPTL kujadiliana kwa kile kilichoelezwa na Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) kuwa uwezekano wa kushinda kesi ni mdogo ni pamoja na:-
 Ushauri wa Mawakili unaokinzana
Mheshimiwa Spika, tarehe 4 Oktoba, 2012, Mawakili wetu (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) walitoa ushauri kwamba, kwa kuzingatia utetezi walioutoa kwa TANESCO kwenye kesi hii kule ICSID, London kiasi cha chini kabisa kinachoweza kuidhinishwa na Mahakama ya ICSID, London kama malipo ya Capacity Charges kwa IPTL ni kati ya Dola za Marekani milioni 85 hadi 90 na Mawakili wetu (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams)  wakasema, nanukuu, “This could be considered TANESCO’s  Best Case Scenario”. Hata hivyo waliendelea kusema “This best Case Scenario is overly optimistic”

Mheshimiwa Spika, katika maelezo yao mengine ya tarehe 4 Oktoba, 2012, Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanasema, “In these circumstances, SCBHK may recover 100% of its claimed damages of USD 130 milion even if substantially TANESCO prevails on a portion of its equity defense”.

Kwa lugha nyingine Mheshimiwa Spika Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanasema kiasi cha chini kabisa ambacho TANESCO ingedaiwa na SCBHK kingekuwa Dola za Marekani milioni 130 bila kujumuisha gharama nyingine za moja kwa moja kwa IPTL.
Mheshimiwa Spika, Katika majumuisho yao ya tarehe 4 Oktoba, 2012, Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) waliishauri TANESCO ikae na SCBHK na kukubaliana nje ya Mahakama na kumlipa Dola za Marekani kati ya milioni 75 na milioni 90 na kiasi kitakachobaki kikidaiwa kilipwe kwa wadai wengine, wakiwemo IPTL, Law Associates na Kampuni ya Mafuta ya TOTAL.

Mheshimiwa Spika, Kufikia tarehe 5 Septemba, 2013 kwa mujibu wa Taarifa ya Mfilisi (RITA), ilionesha kuwa Kampuni ya IPTL ilikuwa ikiidai TANESCO zaidi ya Dola za Marekani milioni 224.30, sawa na Shilingi bilioni 370.70. Majadiliano yaliyofanyika kati ya TANESCO na IPTL tarehe 9 Oktoba, 2013 yaliwezesha kukubaliana kuwa malipo stahiki kwa IPTL ni jumla ya Dola za Marekani milioni 166, sawa na Shilingi bilioni 274.56. Kati ya hizo, Dola za Marekani milioni 121, sawa na Shilingi bilioni 220.13 zilikuwa kwenye Akaunti ya ESCROW na Dola za Marekani milioni 45, sawa na Shilingi bilioni 74.43 zitalipwa kwa kipindi cha muda mrefu usiozidi miaka mitano.
Kama fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni za Umma
                           
Katika ukurasa wa 58 wa Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow zilikuwa za Serikali.

Ufafanuzi:

Mheshimiwa Spika, Huu si ukweli zipo sababu kuu zinazothibitisha kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali.

1.     TANESCO ilikuwa inapata huduma ya umeme bila kulipa moja kwa moja IPTL, lakini ikawa inapeleka fedha hizo katika Akaunti ya Escrow.

2.    TANESCO ilisimamisha kupeleka malipo kwenye Akaunti ya Escrow na wala kulipa IPTL kuanzia tarehe 30 Oktoba, 2010.

Pamoja na kutokulipa, TANESCO iliendelea kupata huduma ya umeme kwa kadri ilivyohitaji kutoka IPTL.

Mheshimiwa Spika, katika Ukurasa wa 36 hadi 42 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo tumekabidhiwa inaonesha kiasi ambacho TANESCO inadaiwa na IPTL.
Mheshimiwa Spika, Kulingana na Taarifa hiyo  ukurasa wa 36 hadi 42 imeonesha kuwa kiasi ambacho kilipaswa kuwekwa kwenye Escrow Account kwa mujibu wa Ankara za IPTL ni Shilingi bilioni 306.68. hata hivyo, kwa mujibu wa Ukaguzi huo fedha zilizokuwa kwenye Akaunti  wakati wa kuifunga ni Shilingi bilioni 182.77 na kuwa na  upungufu wa Shilingi bilioni 123.90 ikiwa ni deni ambalo TANESCO bado wanadaiwa na IPTL.

Mheshimiwa Spika, Kwa msingi huo fedha zote zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni mali ya IPTL na IPTL kama Wakala wa Kodi anastahili kudaiwa na mwisho kulipa kodi yo yote ambayo hajalipa.

Kwa msingi huo, Taarifa ya PAC haisemi ukweli kuhusu fedha zilizowekwa katika Akaunti ya Escrow kuwa ni fedha za umma.
Mheshimiwa spika, ili kuthibitisha kwamba fedha hizi siyo za Umma, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukaguzi wake wa Hesabu za TANESCO wa tarehe 31 Desemba, 2012 alielekeza kutoa fedha za Escrow kwenye Vitabu vya Hesabu vya TANESCO na kupunguza deni kwa kiasi hicho hicho kwa maelezo yafuatayo:

“As a result, the deposit balance in Escrow account does not meets the definition of an asset of the Company and therefore an adjustment has been made to de-recognize the asset and related liability to the tune of the amounts available in the Escrow account”.

Iwapo kwa mujibu wa Mkataba wa PPA TANESCO na IPTL walilazimika kutumia Mtaalamu wa Upatanishi (Mediation Expert) katika utatuzi wa mgogoro kabla ya kutolewa fedha zilizopo kwenye Akaunti ya Escrow.

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Kamati ya PAC ukurasa wa 9, imeeleza kuwa kwa mujibu wa Mkataba wa PPA, TANESCO na IPTL walipaswa kutumia Mtaalam wa Upatanishi katika mgogoro wa Capacity Charge.

Mheshimiwa Spika, tunapenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 18.1 ya Mkataba wa PPA, wahusika wa Mkataba huo ambao ni TANESCO na IPTL wanatakiwa kwanza kumaliza mgogoro baina yao kwa njia ya upatanishi (amicable settlement). Iwapo watashindwa kufikia makubaliano ndipo watalazimika kutumia Mtaalam wa Upatanishi kutatua mgogoro huo. TANESCO na IPTL walimaliza mgogoro baina yao kwa njia upatanishi kwa kufanya uhakiki wa kiasi ambacho kila upande ulikuwa unastahili kulipwa katika Akaunti ya ESCROW kabla ya akaunti hiyo kufungwa. Kwa msingi huo, hapakuwa na sababu ya kutumia Mtaalam wa Usuluhishi kama ilivyoelezwa katika Taarifa ya PAC.
Kama muda wote wa Mkataba wa TANESCO na IPTL hapakuwahi kuwa na Kamati ya Uendeshaji

Mheshimiwa Spika, taarifa ya PAC inaeleza kuwa hapakuwahi kuwa na Kamati ya Uendeshaji kwa kipindi chote cha Mkataba wa PPA. Ukweli ni kwamba, Kamati ya Uendeshaji iliundwa kabla ya kuanza uzalishaji wa Mtambo hapo 2002 na imeendelea kuwepo hadi leo. Kamati hiyo ina wajumbe  sita. Wajumbe watatu kati ya hao wanatoka TANESCO. Wajumbe watatu waliobakia wanatoka IPTL. Wajumbe wa TANESCO walikuwa ni kama ifuatavyo:

1.     Mhandisi Masanyiwa Malale;
2.     Mhandisi Christian Msyani; na
3.     Mhandisi James Mtei.

Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo si kweli kwamba Kamati ya Uendeshaji haikuundwa kama ilivyoelezwa na Kamati ya PAC katika ukurasa wa 10.
Wizara kutambua Hati za Hisa za Makampuni

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 27 wa Taarifa ya Kamati ya PAC, Kamati hiyo imeitaka Wizara ya Nishati na Madini kutambua usajili wa Hati za Hisa za Makampuni. Tunaomba ieleweke kuwa siyo majukumu ya Wizara kutambua na wala kujishughulisha na Hati za Hisa za Makampuni Binafsi. Aidha, katika ukurasa wa 45, imeelezwa kwamba “Waziri wa Nishati na Madini ndiyo Mamlaka ya kuthibitisha uhamishaji wa umiliki wa Kampuni katika sekta yake”. Ningependa kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba jukumu hilo pia siyo la Wizara ya Nishati na Madini ni vizuri majukumu ya Wizara yakaangaliwa vizuri na kutoleta mkanganyiko na kuwadanganya wananchi wetu. Hii inaonesha kuwa kamati haikupitia vizuri majukumu ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, katika Taarifa ya PAC, ukurasa wa 30 Aya ya 2, imeelezwa nanukuu “nilishuhudia nyaraka kwamba Piper Link ilinunua Hisa za MECHMAR na katika mauziano hayo Kampuni hiyo iliwakilishwa na Bw. Harbinder Singh Sethi hivyo huyu bwana ndiye Piper Link na ndiye PAP”. Kwa maneno haya ya Kamati ya PAC, aliyekuwa na hati za Piper Link ni Bw. Sethi na aliyenunua Piper Link ni Bw. Sethi anayemiliki PAP. Kwa kuzingatia maelezo haya ya kamati ya PAC, inaonesha kwamba hakuna tatizo la uhamishaji wa Hisa Asilimia 70 kwenda kwa PAP.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo ya Aya iliyotangulia, bado Kamati ya PAC ukurasa 44 wa taarifa yake, inaonesha kuwa Hisa hizo zinashikiwa na Martha Renju huko BVI lakini Martha Renju amefungua kesi mara mbili Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kutumiwa na SCBHK akiwa na lengo la kutaka kujipatia fedha za Escrow bila uhalali. Hata hivyo, amekuwa akiziondoa kesi hizo mahakamani.
Mikutano ya Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 29 wa Taarifa ya PAC, inasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ilifanya mikutano miwili mfulilizo kati ya tarehe 16 na tarehe 19 Septemba, 2013 na kwamba uharaka huo unatia mashaka kwamba kulikuwa na njama.

Mheshimiwa Spika, muda wa siku 3 kwa Bodi kukutana si jambo la kutiliwa mashaka kwani Bodi haikutani kwa ajenda moja tu. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa tarehe 16 Septemba, 2013 hapakuwa na kikao cha Bodi isipokuwa   kikao cha Bodi kilifanyika tarehe 19 Septemba, 2013. Hivyo si sahihi kusema kuwa Bodi ya TANESCO ilikuwa ina njama katika kushughulikia na kulitolea maamuzi suala la Akaunti ya Escrow na kwamba ilikutana ndani ya siku tatu.
Hoja ya Mwanasheria wa TANESCO Kufukuzwa Kazi

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 30 wa Taarifa ya PAC kuna hoja kuwa Mwanasheria wa TANESCO kwa wakati huo Bw. Godwin Ngwilimi aliagizwa na TANESCO kwenda Malaysia kufanya Due Diligence ya Kampuni ya MECHMAR Corporation na kwamba taarifa hiyo ya Due Diligence ilifikishwa katika Bodi na Bodi iliipuuza na kinyume chake Mwanasheria huyo aliachishwa kazi.

Mheshimiwa Spika, Taarifa hizi si za kweli na ni uongo uliokithiri kwa aliyekuwa Mtumishi wa Umma kuudanganya umma wa Watanzania kwa kiasi cha kutisha na Kamati inatoa taarifa ya uongo ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, ukweli wa jambo hili ni kama ifuatavyo:

1.     Mwanasheria huyo Bw. Ngwilimi alileta ombi la kusafiri kwenda Malaysia kwa kumdanganya Mwajiri wake kwa kudai kuwa alipewa ushauri wa kwenda Malaysia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika barua ya kuomba ruhusa alisema kuwa alikuwa aende na Mwanasheria Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliruhusiwa.  Hata hivyo, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali haikutoa Ofisa huyo na hivyo kuamua kwenda peke yake.

2.     Bw. Ngwilimi hakufukuzwa kazi na Bodi kama ilivyodaiwa katika Taarifa ya kamati ya PAC katika ukurasa wa 30, bali aliomba kuacha kazi mwenyewe kwa kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa barua ya yenye Kumb na. SEC.215/Conf/2/2014 ya tarehe 27 Februari, 2014 iliyokuwa inasomeka “Notice to Terminate my Service with TANESCO” akitoa notisi ya siku 90 kwa mujibu wa Mkataba wake wa kazi.
  Katika ombi lake alidai kuwa anaacha kazi kwa hiari yake mwenyewe kwa kuwa anahitaji kufanya shughuli nyingine na akaushukuru uongozi wa TANESCO kwa ushirikiano kwa kipindi chote alichofanyakazi. Machi 10, 2014 Shirika lilimjibu Bw. Ngwilimi kwa barua yenye Kumb. Na. N.837 kuwa Uongozi na Bodi ya TANESCO wamekubali ombi lake la kuacha kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo hayo ni wazi kuwa Bodi haikuwahi kumfukuza na Bodi haikukataa utoaji wa fedha za IPTL katika Akaunti ya Escrow. Badala yake Bodi ilielekeza IPTL ipewe fedha zilizopo kwenye Akaunti ya Escrow tu na kwamba usuluhisho uliyofanyika unakubalika. Aidha, Bwana Ngwilimi aliamua kuacha kazi mwenyewe na kukimbia baada ya kuelewa kuwa angechukuliwa hatua kutokana kumsingizia Mtumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa walitumwa wote na kusafiri wote kwenda kufanya kile alichodai due diligence.

MITAZAMO  BAADA YA UWASILISHWAJI WA RIPOTI YA ESCROW

Na Cripan Majura Musiba Jr, Facebook group ya Umoja Village,


Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe nadiriki kusema kuwa hakuna cha maana kwenye ripoti yao cha kuwafanya mawaziri kuwachia ngazi.

Ni drama tu lakini hakuna kipengele chochote cha sheria ambacho hakijibiki au kilichooneshwa kuwa kimekiukwa.
Lowasa na timu yake wamefanya yao na usiku kucha walikuwa wanalewa tu hapa dodoma.

Zitto kapiga porojo nyingi sana kuliko ukweli, na mwanasheria yoyote mahiri anazisambaratisha hoja zake zote ndani ya nusu saa.

Zitto ametetea sana BoT lakini alichoshindwa kuelewa ni kuwa Bot kama wakala ndiye alitakiwa aridhike na vielelezo vyote kabla hajalipa na kama havijakamilika hawezi kutoa fedha. Zitto anasema eti Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye alimuamuru Gavana hizo fedha zitolewe, toka lini Gavana wa benki anatoa fedha kwa amri ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Utata wa IPTL na Standard Chartered ni huko-huko kwao si IPTL iliyokopa, iliyokopa ni Mechmar na Mechmar haiwezi jitokeza kwani imeshafilisika kisheria, Standard Chartered karata yao ya mwisho..
Mapendekezo ya Zitto ya watu kuachia nyadhifa zao ni ya kishabiki na hayana mshiko, watu hawaachii tu nyadhifa zao kwa habari kama hizi ambazo hazina mshiko wa kisheria.

Isitoshe, fedha zilizolipwa escrow si kamili, hizo zilizobaki zilizuiliwa kwanini? Jibu tutalipata leo na ndilo litakalosambaratisha hoja ya kodi ya Zitto.


Kuna mengi sana ya kuchambua lakini tusubiri leo tusiandikie mate na wino upo. Ni matumaini yangu kuwa wote waliotajwa watapewa fursa ya kujibu.

BAADHI YA WAKATOLIKI WALALAMIKIA MCHEZO MCHAFU WA KISIASANa Charles Misango, Vijana Wakatoliki Facebook Group,

Mimi siogopi kulijadili kwa sababu za msingi. Hapa viongozi wa juu wa kanisa wametuhumiwa na tayari bunge limeagiza warejeshe fedha zote na kufilisiwa. Hili sio jambo dogo. Binafsi sipingi ila kuna utata mwingi naupata katika hoja za kamati ya Zitto. Nazo ni hizi zifuatazo:
1.    Wanasema benki ya Mkombozi itangazwe kuwa imetakatisha fedha haramu. Zipi hizo? Maana maelezo yanaonesha kuwa fedha hizi ni halali kabisa na ndio maana zilifunguliwa akaunti na zilikuwa chini ya usimamizi wa benki kuu. Zilijulikana zimetoka wapi na nani alilipwa. Sasa uharamu wake unatoka wapi hadi zitakatishwe na benki ya mkombozi? Lini zilianza kuwa chafu? Nani alizichafua? Na uhalali ama uharamu wa fedha unatokana na nini?

2.   Wakati kamati ikitumia vielelzo vya nyaraka kadhaa na mawasiliano ya waziri mkuu, na mawaziri wa Nishati na Madini akiwemo mwanasheria mkuu kutetea fedha hizo kutokuwa mali ya umma, kama ushahidi wa kuwatia hatiani, mbona ilishindwa kuwaita maaskofu na wale wote waliopewa fedha hizo na rugemalira, ili kuwahoji? Iliwaogopa nini na kwa nini iwahukumu bila kuwasikiliza ikijulikana kuwa kamati iliendesha uchunguzi huo katika sura ya kimahakama? Kuna usawa gani wa kujifungia mwenyewe, kujihoji mwenyewe na kutoa hukumu bila kuwapa haki ya kujieleza watuhumiwa? Ikumbukwe kwamba watuhumiwa ambao ni wabunge na mawaziri, wanayo haki ya kusimama bungeni na kujitetea. Je, hawa waliohukumiwa watajitetea wapi? Je Kamati haioni kuwa haijatenda haki, maana hata mwizi anapewa haki ya kusikilizwa

3.  Kamati inayo haki na pengine ushawishi wao unakubalika kwa vigogo wa kisiasa na kiserikali ambao wamepewa fungu la fedha hizi, kuwa pengine walihusika kwa namna moja ama nyingine kufanikisha mipango ya kuchotwa kwa fedha hizo na ndio maana wamepewa mgao wao. Swali je, hawa viongozi wa dini na raia wengine walipewa hela ili wafanye nini kufanikisha kuchota fedha hizo? Kama Askofu Kilaini na mwenzake wangekuwa wajumbe wa bodi ya benki kuu ama Tanesco, ningeweza kuelewa. Sasa Zitto angesema kamati yake inaamini wamepewa fedha hizo ili wasaidie kukamilisha nini? Hawakusema.
Nikisema haya, sina maana kwamba namtetea mtu; la hasha! Lakini tunataka ukweli na haki itendeke!

Maoni ya ndg. Damian Masanja, Kutoka Facebook group ya VIJANA WAKATOLIKI


Tumsifu Yesu Kristu. Imeandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Jiulizeni kwa nini hakuna mtumishi wa wizara ya fedha au nishati na madini waliopewa mgao? Ukijumlisha hizo fedha alizosema Zito na  Ccm yake hazifiki hata billion 100.zingine zimechukuliwa na nani? 

Kampuni ya PAP inamilikiwa na Seth pamoja na Simba trust yenye asilimia 50, kwa nini haikutajwa? Kwa nini wamiliki wake hawakutajwa? Kwa nini hakuna jina la kiislam hata moja?

Hapa kumbukeni kanisa Katoliki sasa linanyamazishwa na watawala kwa kuwachonganisha na waumini wake ili wasiwaamini viongozi wao. Kisa? Kanisa ndio liliongoza kuikataa katiba pendekezwa ya ccm baada ya kuitupa ya wananchi. Kanisa lilitoa waraka kulaani kitendo cha wabunge wa ccm kwa kivuli cha bunge la katiba.

Kanisa Katoliki likuwa na waumini wengi ndio linaweza kuiangusha ccm katika uchaguzi mwakani kama waumini wake watawasikiliza viongozi wao. Amkeni, hela kwenye akaunti yako inaweza kuingizwa bila wewe kujua wala kupenda.

Tuendeleeni kujua kuwa kanisa linateswa na utawala wa ccm. Hamjiulizi kwa nini mapadre wetu wanauawa kule Zanzibar na wauwaji hawakamatwi? tuendeleeni kuwa na mshikamano ili nguvu za kuzimu zisilishinde kanisa.

Fedha zilizoibwa ni billion 321 mbona huyu kibaraka wa ccm Zito ametaja kidogo sana? Zito alifukuzwa uanachama wa CHADEMA hivyo kupoteza sifa za kuwa mbunge kwa nini ccm ilimng'ang'ania? Anawalipaje? Angalieni msiangamie kwa kukosa maarifa ya kutambua njama za ccm. Kristo.......


Update Nov 26/11/2014

RIPOTI IMEWASILISHWA
Ripoti imekwisha wasilishwa na kubaini mapungufu kadhaa baina ya watendaji na kupelekea upotevu wa bilioni 306.

Mapendekezo

 • Kuwajibishwa kwa Mwanasheria mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na naibu wake, Katibu mkuu wa nishati na madini.

 • Kuvunjwa kwa bodi ya shirika la umeme la Tanesco

 • Kufuta umiliki wa PAP iliyoinunua IPTL inayomilikiwa na Harbinder Singh Seth pamoja na kuchukuliwa hatua za sheria

 • Kuundwa kwa chombo kitakacho shughulikia rushwa kubwa ukiachia TAKUKURU na chombo hicho kuwa na mamlaka ya kuchunguza na kupeleka mashtaka mahakamani.

 • Kufilisiwa kwa mali pamoja na kurudishwa fedha kwa wahusika wote waliopokea mgao wa fedha pamoja na wale watumishi wa Serikali kufukuzwa kazi.

 • Kuangaliwa kwa utaratibu mpya utakaovitazama vyombo vilivyoshiriki utakatishwaji wa fedha na hatua za kisheria kuchukuliwa (STANBIC na Mkombozi Commercial Bank)

 • Kutaifishwa kwa mitambo ya IPTL na kupelekwa TANESCO.

 • Kusimamia mapendekezo ya kamati wa Mwakyembe wakati wa mawasilisho ya kashfa ya Richmond 

 • Maamuzi yatategemea taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Bunge itakayotolewa tarehe 27/11/2014 pamoja na mijadala ya Wabunge itakayoendelea tarehe 28/11/2014

TETESI ZA WEREMA, TIBAIJUKA KUNG'ATUKA

Hatimaye mwanasheria mkuu wa serikali bwana Fredrik Werema amekubali rasmi kung'atuka katika
cheo hicho baada ya ripoti ya PAC kuwekwa rasmi hadharani huku waziri mkuu Mizengo Pinda akisema anasubiri hatma yake katika majadiliano  yatakayofanyika bungeni. 

Aidha waziri prof. Anna Tibaijuka naye amekubali kung'atuka baada ya ripoti ya PAC kusomwa bungeni.
Hayo yameamuliwa katika kikao cha CCM chini ya Philip Mangula kilichomalizika mjini Dodoma leo alfajiri. Pinda amesema kuwa hatma yake iko mikononi mwa wabunge kama watapitisha kwa kauli moja kuwa ang'atuke yupo tayari kufanya hivyo kutokana na ripoti ya PAC kutokumuwajibisha kwa lolote lile.

Ripoti ya PAC imewawajibisha kwa uzembe AG Werema, Saada Mkuya- fedha, Muhongo Sospeter- Nishati na madini na gavana Beno Ndulu.Aidha wengine ni vigogo wote wa juu wa Tanesco.

Kwa upande mwingine bunge litaamua  hatma ya waziri mkuu pamoja na mawaziri wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu huku wakikwepa sekeseke la kuwajibishwa na PAC.


Kikwete anatarajiwa kurejea kesho usiku ambapo atalazimika kumteua AG mpya na kulisuka upya baraza la mawaziri na kama wabunge wataamua kumsulubu Pinda( kutokana na utashi wao kwani hajabanwa na PAC) basi Kikwete atalazimika kuiunda upya serikali.


UJUMBE WA VITISHO KWA KAFULILA

Taarifa kutoka THE CITIZEN

“I think you have decided to die for seeking stupid popularity…I feel sorry about you because you don’t know who you are fighting”

MESSAGE REPORTEDLY SENT TO KIGOMA SOUTH MP DAVID KAFULILA

Kwa hisani ya Twitter ya Jamii Forums.

 • Taarifa  zinabainisha Bunge litaahirishwa hadi jioni.

 • Serikali (Lukuvi na wenzie) wanadaiwa kutumia mabavu  TegetaEscrow Report isomwe tu bila kujadiliwa

 • Watu wa PAP na hati yao ya mahakama wapo getini Bungeni wakitaka kutoa hati kwa BUNGE. BUNGE limegoma kupokea

 • Spika & Katibu wa Bunge wamejifungia ofisini kwa spika kujadili kabla ya Kamati ya Uongozi. Wenyeviti wengi hawajafika.

 • Wenyeviti Waliofika mpaka sasa ni Ngwilizi, Msola, Mbowe na Serukamba.

 • Wabunge wamepewa nyaraka bila hata kuwasilisha kwa kusoma. Kamati ya Uongozi inajadili amri ya mahakama.

 • Baada ya bunge kukaidi amri ya mahakama kuna madai kuwa Polisi wameagizwa wamkamate Spika na timu yake. So tunaweza kushuhudia kichekesho asubuhi hii Dodoma, cha polisi kuwakamata Spika, AG, Katibu wa bunge, na wengine waliokiuka amri ya mahakama.

 •  Zitto, Filikunjombe na wajumbe wengine wa PAC wamelala nje ya ofisi ya Spika wakiilinda ripori isichakachuliwe. Ktk hili nawapongeza.

 •  Baadhi ya Wabunge wameanza kuondoka kwa kuhofia vitisho. Ila na wale "wanafiki" wasiopenda misimamo yao ijulikane wameanza kuondoka kwa kusingizia vitisho. So hawa wanarudi hotelini na kwenda kujifungia ili wawaangalie wenzao wakifanya maamuzi kupitia TV. 

 •  Serikali imeandaa Mikakati wa kukata umeme baadhi ua maeneo (hasa mijini) ili watu wasiweze kufuatilia mjadala wa leo kupitia TV. Mkakati wa kukata umeme umekamilika kwa baadhi ya maeneo na hadi sasa kuna maeneo hawana umeme.!
HUKUMU YA ZUIO LA  MAHAKAMA KUHUSU MJADALA WA ESCROW  BUNGENI NA TAFSIRI YA KISHERIA.


Tafsiri ya Wakili Alberto Msando,
Mahakama imesema "status quo be maintained"

What is the status?

Status iliyopo ni Bunge liendelee na ratiba yake kama ilivyopangwa. Hiyo ndio tafsiri ya status quo. Kwamba kila kitu kibaki kama kilivyo. Mpaka jana hali iliyokuwepo ni ripoti kuwasilishwa leo na kujadiliwa. Hivyo basi hali inatakiwa ibaki kama ilivyo.

Endapo wabunge wataendeleza ushabiki basi heshima ya bunge itafikia kiwango cha chini kabisa kulingana na kile cha mahakama.

Tafsiri ya amri hiyo inahitaji akili ya kawaida sana. Akili ya kuangalia kushoto na kulia kuvuka barabara. Ni mlevi pekee ndio anaweza kuvuka barabara bila kuangalia. Hata chizi huwa anaangalia ndio maana ni mara chache utasikia chizi kagongwa na gari.


Ripoti ruksa kusomwa na kujadiliwa bungeni kwa sababu Amri ya mahakama imesema hali ibaki kama ilivyo!!! Ukichanganya na Katiba inavyosema kuhusu Mamlaka ya Bunge basi hakuna mgongano wa Mihimili ya Dola.

Update Nov 25/11/20

KIKAO CHA DHARURA IKULU NDOGO DODOMA

-Chanzo Yericko Nyerere kupitia Jamii Forums,

CCM wamekutana kwa dharura muda huu katika ukumbi wa ikulu ya Dodoma.

Agenda kuu ni kupitia ripoti nzima na MAPENDEKEZO ya PAC, Wanataka kupitia mapendekezo ya PAC mapema na kulekezana namna ya kuokoa, pia ripoti waliyogawa kwa wajumbe haina vielelezo kwa ajili ya rejea. Mbali na bank statements ya Rugemalila, imefichwa ya Pap.

Wamewaita wajumbe wote wa CCM waliopo PAC ili watolee ufafanuzi wa mapendekezo hayo.

Wajumbe hao ni:

Zainab vullu, Ali Mohamed kessy, Jabir marombwa, Faida Bakari, Kangi Lugola, Deo filikunjombe.

Katika hatua nyingine Katibu wa bunge Mr Kashilila amegoma kupokea barua ya Mahakama.

Barua hiyo imeletwa kwa ndege ya kukodi,Wakili aliyefungua kesi anatoka kijiji kimoja na Pm, alikuwa NCCR Mageuzi zamani sasa yupo CCM.
KESI YA KUZUIA MJADALA WA ESCROW KUJADILIWA BUNGENI YAFUNGULIWA MAHAKAMA KUU


-Chanzo IPP MEDIA,

Maafisa wanaojitambulisha kuwakilisha  Kampuni ya  Pan Africa Power-PAP wapo mahakama kuu ya Dar es salaam kufungua shauri la kuzuia suala la Escrow kujadiliwa na Bunge.

PAP wamefungua shauri hilo kwenye mahakama kuu kanda ya Dar es salaam  wakimshitaki waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG na katibu wa bunge kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa jambo lililokwisha kutolewa hukumu na mahakama na kukaguliwa na hivyo kutaka kuzuia mjadala wowote wa suala hilo hadi ufafanuzi wa mahakama utakapotolewa.

Kufuatia suala la maafisa wanaojitambulisha kuwakilisha Pan Africa Power-PAP kuwepo mahakamani kufungua shauri la kuzuia suala la Escrow kujadiliwa na Bunge Spika Mheshimiwa Anne Makinda  amesema hakuna mtu anayeweza kuzuia bunge kufanya kazi za kibunge.

Alitoa kauli hiyo baada ya wabunge kuhoji juu ya taarifa hiyo ya PAP Kufungua shauri na kusema kuwa Bunge lina Kinga ya kutoingiliwa hivyo Ripoti ya CAG itagawiwa kwa wabunge wakati wa mchana kwa maandalizi ya mjadala wa Escrow.

KUTOKA BUNGENI Kufuatia ombi la mheshimiwa Mnyika kwa Spika Ana Makinda leo asubuhi bungeni, Ana Makinda amejibu kuwa mpaka sasa hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa inayohusu kusimamisha ripoti ya CAG na TAKUKURU isisomwe bungeni, akishangiliwa kwa kelele na vifijo Makinda amesema kuwa hata zile kesi 10 zilizokuwazinasemwa kuhusu IPTL hazipo hivyo ripoti itasomwa kama ilivyopangwa  Jumatano 26/11/2014.

VITA VYAHAMIA TWITTER, FACEBOOK ,INSTAGRAM,WHATSAPP.

VITISHO KWA WANASIASA

Hadhari kubwa hawa wafuatao kwa kuwa wapo kwenye hatari zaidi. Hatari hii itapungua (haitaisha) baada ya ripoti kusomwa Bungeni lakini baada ya hapo kuna watakaoendelea kutaka kulipiza kisasi.
1. Nimrod Mkono (hata baada ya kunusurika bado anasakwa, wao wanaamini ni kinara dhidi ya kinachoendelea sasa)
2. David Kafulila (Wanaamini huyu anatumiwa na Zitto, Mengi na Mkono katika kufikia malengo)
3. Zitto Kabwe (Wanaamini bila nguvu ya ziada ya huyu mtu sakata hili lingepotelea hewani, wameshafanya mashambulizi ya kimkakati kwake na watajwa hapo juu bila ufanisi mkubwa)
4. Reginald Mengi (Huyu pamoja na kuwa wengi wanadhani ni vita yake dhidi ya Muhongo kama ambavyo propaganda zimekuwa zikieleza; bado hadi namba moja anaamini jamaa anahusika kuiangusha serikali yake kwa kutumia vyombo vyake vya habari na wanasiasa)
5. Mhariri wa The Citizen (Hawa wamekuwa mwiba mkali katika sakata hili, wao wanasema hawa watu ni tatizo na ni vyema wapunguzwe makali. Lolote linaweza kufanywa, umakini kwa mhariri ni muhimu sana kwa wakati huu)
6. Mhariri mkuu (admin) wa JamiiForums (Inadaiwa hapa JF zimekuwa zinaanzishwa thread zinapigwa pini wakati zilikuwa zikilenga kupoza nguvu ya sakata hili. Wao wanaamini JF inasomwa sana na kitu kikianzia JF kinakuwa viral; kuzuiliwa kwa mijadala yao kunaonekana kuwakera na tahadhari ni muhimu kwa mhusika).
Ifahamike kuwa, mashambulizi yao hayatakuwa ya moja kwa moja kama wengi wanavyodhania. Mashambulizi ya kibaiolojia huenda yakatumika.Update: Nov 24/11/2014

Inaandaliwa hoja ya kumpigia spika Makinda kura ya kutokuwa na Imani nae,  baadhi ya wabunge Wa ccm wanaanda mpango huo na  wametoka nje kumjadili kwa ubabe aliounesha na alivyojipanga kuzima mjadala.

Yule mtuhumiwa  aliyekamatwa na ripoti ya escrow, bwana Mohamed Mbaruk atapaelekwa mahakamani ili kukidhi matakwa ya sheria ya kutojadili jambo linalo subiri uamuzi wa Mahakama.

Wabunge wapinga ufisadi wameamua kuungana na wabunge Wa upinzani, pia mkakati wa kwenda jimboni kwa spika Makinda unaendelea  kuratibiwa. Update: Nov 23/11/2014

Baada ya kujihakikishia kuwa ripoti wameinyofoa kurasa zenye majina na ushahidi wa wizi wote,

Wamekuja na maazimio mawili makubwa,

1. PAC iwekewe kanuni (kibabe) kuwa itoe pendekezo kwa Spika la nini cha kufanya.

Baada ya hapo Spika atalitangazia bunge kuwa amepokea mapendekezo na ushauri wa PAC hivyo anaiarifu serikali hatua za kushughulikia tatizo hili,
Hili limeamuliwa spika atumie ubabe bila kuangalia kanuni wala busara.

2. Kwakauli moja vikao vya ccm vimeridhia Mh Ndugai afukuzwe Bungeni kwa siku 14 mpaka mgogoro huu uishe, 

Katika kutimiza azimio hilo, nikuwa amepangiwa kwenda ufaransa kwa mapuziko ya siku 14,

Safari yake itakuwa leo jioni.Update:.


UTETEZI WA BOT (BENKI KUU TANZANIA)
Hali ya taharuki imeibuka baada ya ccm kuiba kwakunyofoa kurasa zenye ushahidi wote wa wizi na majina ya wezi wote,

Kurasa za 56,57,59... Zote zimenyofolewa, kibaya zaidi wezi hawa wameiba kuanzia iliyopo Bunge kwa Kashilila, Kwa ofisi ya PAC, na ile ya CAG huko Dar,

Hali sasa inayoendelea nikuwa ripoti iliyobaki isiyo na ushahidi wala makali wezi hawa wamewagawia wabunge wa CcM na wananchi mtaani ili nakuwaambia wajionee wenyewe ripoti haina mtu wakuwajibika. 

Update: 
Moshi umeonekana umetanda maeneo ya Benki Kuu Tanzania jijini Dar leo  na kuleta hofu miongoni mwa wakazi na wapita njia.(Kikao cha Siri) Kikao kinaongozwa na Wasira na Lukuvi, 
HABARI KUTOKA MTANDAO WA JAMII FORUMS.

Na Yericko Nyerere,

Wabunge wa ccm wale wanaopiga kelele kuhusu Wizi huu wamewekwa mtu kati,

Kinafanyikia Ikulu ya Dodoma kwa siri kubwa, hata magari yao yote yameigizwa ndani kabisa, kwa hapa nje lipo Gari la Lembeli aina ya Range Rover Namba T382 lililokosa nafasi ndani. kikao hiki kimeitishwa kwa meseji tu hii ni baada ya jioni kutangazwa kuwa kimeahirishwa,

Sababu za usiri huu ni pale tulipowaanika jana katika kikao chao cha shinikizo kwa Werema ajiuzuru, Zigo limemdondokea Godfrey Zambi kuwa ndie aliyevujisha siri ile kwakuwa aligoma kuzima simu na alikuwa akichati fb wakati kikao kikiendelea, hivyo kikao cha sasa hivi katupwanje.

Kikao hiki kwa sasa kimembana Ndugai kwamadai anaihujumu serikali, 

Ndugai amezila kuendelea na Bunge amesema yeye sasa hata ongoza vikao, bora awe pembeni kuepusha msongamano!

Ccm imegawanyika makundi matatu, lile linaloshinikiza waliohusika na wizi huu wote wapigwe chini lakini,ukifuatilia kundi hili linavizia vyeo vya uwazili, na tayari kampenzi za kuwania vyeo hivyo zimeanza.Kundi la pili hili ni wanafiki wa kati wasio na msimamo, lenyewe linataka wafukuzwe wachache (maswi,tibaijuka,mhongo na werema) hili linasema linanusuru serikali isianguke.

Kundi la mwisho ni la wezi wenyewe, hili linafanya kila njia ripoti hii isisomwe bungeni, hili linaongozwa na Pinda na Werema.

UPDATES.22/11/2014

Ndege ya serikali ipo hapa Dodoma imekuja alfajiri hii 5-H CCM.. Aina ya folker F28 haijajulikana imemleta au imekuja kumchukua Nani, ila taarifa za awali zinasema Bilali alikuwa aje leo.

Hali ya mambo ni ngumu kama vile nchi ipo vitani...!

Kinana tayari ameletwa na Ndege mida hii,

Mrejesho wa Kikao Cha jana usiku

Imeamriwa popote alipo Spika Makinda aje, Ndugai out hadi sakata lipite, afanye awezavyo Pinda apone,.. Wachangiaji wakali wasipate nafasi iitwe briefing ya wabunge wote watapike nyongo nje ya waandishi ili siku ya mjadala kuwe na hewa safi.Kama ni kuondoka waondoke mawaziri ila sio waziri mkuu.

Inatakiwa njia ya kumuangukia au kumdhibiti Mh. Mengi wa IPP,

Leo agenda kuhusu Mengi itajadiliwa kwa kina katika kikao cha baadae. Ifahamike kuwa Vyombo vya habari vya Bwana Mengi vimekuwa vinalielezea jambo hili kwa uwazi na uhuru mkubwa kiasi cha umma kulielewa.


Updates: 

 ESCROW  NA MCHAKATO WA  KURA ZA MAONI CCM 2015

Utafiti wa awali  unaeleza, pamoja na Prof. Tibaijuka, vigogo kadhaa  nao wamelamba asilimia kubwa  ni wagombea Urais wa CCM 2015.
(1) Ngeleja amepata dola 400,000
(2) January Makamba dola 800,000
(3) Werema dola 2,000,000
(4) Jack Gotham dola 1,800,000 huyu ni mpambe mkuu wa Bernad Membe na fedha hizi zimetolewa kwa ajili ya uchaguzi.
(5) Ndg Nawaab Mullah dola 2,500,000 amepokea kwa Niaba ya Pinda kuchangia Mfuko wa Kampeni za 2015 .


 Mullah ndie ambae wanashirikiana na  kampuni tanzu ya Home Shopping Centre kwenye Mradi wa Umeme wa Kinyerezi na Pinda anawasaidia ili serikali itoe Goverment Guarantee Wapewe mikopo. huu mradi escrow ni cha Mtoto Ufisadi uliopo ktk Dili hii.  Tanesco walitangaza Tenda ktk Gazeti la The Citizen mwezi April/May kwa mwaka 2014  na walimpatia tenda za dola milioni 150 Kampuni ya  tanzu  ya  Home shopping Centre kwa ajili ya Kuipatia Tanesco Nguzo za Umeme.   Tend ya Nguzo  Kinyerezi  ina  harufu ya ufisadi wa dola milioni 150.

Pinda kwa sasa Anapiga Dili za vibali vya Sukari na Zakaria Hanspope, wanapitisha bila kulipa kodi  inadaiwa amekuwa akimtumia afisa wa serikali anayeitwa Masamaki.

 Mtikisiko! Serikali, CCM wahamia Dodoma. Pinda, Kagasheki watoleana uvivu

Hali sasa ni dhahiri si shwari tena mjini Dodoma.Pilikapilika za magari ya vigogo pamoja na ndege ndivyo vinavyotawala kwa sasa katika mabarabara na uwanja wa ndege!

Katika hali ambayo si ya kawaida, vigogo wa ngazi za juu wa CCM pamoja na serikali wameingia Dodoma kwa fujo hivi leo huku makamu wa rais dr. Mohamed Gharib Bilal akitarajiwa kutua hapa mchana wa leo tayari kuongoza kikao kutokana maelekezo aliyopewa na rais Jakaya Kikwete.

Jana waziri Prof. Mark Mwandosya aliitwa Dar kwa dharura na tayari amerudi Dodoma leo asubuhi na mapema akiongozana na vigogo wakuu wa CCM wakiwemo Kinana na Mangula.

Katika tukio jingine mbunge Hamisi Khagasheki amejikuta katika mtifuano mkubwa na wanaomuunga mkono Pinda baada ya kumtuhumu waziwazi waziri mkuu Pinda katika mitandao ya kijamii kuwa ni mwizi ambaye hakupaswa kusubiri hadi leo.

Miongoni mwa waliomjia juu Khagasheki ni John Komba huku akimdhihaki kuwa anaona gere baada ya kutoswa uwaziri!

CCM hapa Dodoma imepasuka vibaya sana kwani kuna wakati Pinda anazomewa waziwazi na wanaCCM wenzake wakiwamo wabunge hali inayoashiria kuwa sasa uwaziri mkuu wa Pinda umefikia tamati!

Bado hali ni ngumu na inaelekea Dr. Bilal anakuja na ujumbe kutoka kwa rais Kikwete.Pia tayari imethibitika kuwa zote hizo ni jitihada za kumnusuru Pinda ingawa Werema, Tibaijuka Muhongo, Masele na Maswi watalazimishwa kwa mara nyingine kujiuzulu leo. Hawa wote wameambiwa iwe isiwe ni lazima wang'oke kabla ripoti haijapelekwa bungeni!


Bernard Membe anapofanya juhudi za kuiangusha serikali yake


Na Nyangeta Marwa,

 Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Barnard Membe anatuhumiwa kufanya kampeni nzito kwa wabunge waishambulie na kuiangusha serikali bungeni kupitia saakata la Escrow. Mpango huu unaendeshwa kwa usiri na umakini wa hali ya juu huku kachero huyo wa zamani akiwatumia wabunge wa upinzani na si wa chama chake CCM. 

Taarifa zilizovuja kutoka ndani ya kambi ya Membe zinaeleza kuwa Membe anaitumia nafasi hii ya sakata la ESCROW kama fimbo ya kujiimarisha kuelekea 2015 kwa kumshughulikia mtu anayetajwa kumvurugia upepo wake wa kisiasa waziri mkuu Mizengo Pinda. Katika kufanikisha jambo hili, Membe anatumia ushawishi na hata kuwahonga fedha baadhi ya wabunge wa upinzani akimtumia mpambe wake wa karibu ambae ndiye humtumia katika kusimamia mipango yake ya urais Jack Steven Gotham. 


Inasemekana Membe ameamua kuendesha mkakati huu kwa siri kubwa akiwa amejificha nyuma ya kivuli cha waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambaye ndiye anatajwa kuwa anawatumia wabunge kumshambulia Pinda na serikali ili ajiuzulu kama njia ya kumsafishia njia ya Urais 2015. Hivyo Membe ametumia akili zake za ukachero kucheza na fikra za watu, na kufanya kampeni ya siri kumuondoa Pinda.

Aidha, Membe amekataa kuwatumia wabunge wa CCM akihofia kuwa watavujisha siri. Hadi sasa maelfu ya dola na shilingi yameendelea kutumika kufanikisha kazi hii. Taarifa za ndani zinaonesha kuwa Membe amekuwa akivujisha siri na kuwapa wabunge hao juu ya mipango inayofanywa na serikali kukabiliana na sakata hili. Chanzo cha kuvuja kwa habari hii ni baadhi ya wabunge hawa kuzungumza na wenzao wa CCM.

Mpambe wa Membe, Jack Gotham amekuwa ndiye muwakilishi wa Membe katika vikao vyake vya kushawishi watu wamuunge mkono Membe. Aidha amekuwa akimuwakilisha Membe katika vikao vya kusaka pesa za kampeni. Kabla ya kutua Dodoma, Jack alikuwa katika ziara ya nchi za kiarabu ambako Membe anasemekana kupata fedha za kampeni ya Urais. 

Hongera Membe. Tuungane kuiangusha serikali.Endelea na moyo huo wa kuwasaidia wabunge wetu wa upinzani.

Mpambe huyu wa Membe ndiye aliyesaidiwa kupata tenda ya mabilioni ya shilingi ya vitambulisho vya taifa ambavyo hadi leo bado vimekua ndoto. Jack Gotham ambae ametua na kujichimbia Dodoma kwa siri kubwa, amekuwa akifanya vikao na wabunge mbalimbali ili kufanikisha zoezi hilo. 

Baadhi ya wabunge ambao tunawahifadhi wanaotoka vyama vya upinzani wameitwa na kupewa maelekezo maalum ya kuhakikisha kuwa wakati wote Pinda ashambuliwe, achafuliwe na kushinikizwa awajibike kisiasa kwa kujiuzulu. Baada ya maelekezo wabunge hao walipewa fedha za kimarekani USD kama posho ya kazi kufanikisha anguko la Mizengo Pinda. 


Mgawanyiko wa Wabunge, Mchakato wa Urais 2015 na Mgongano wa kimaslahi baina ya wafanyabiashara na wanasiasa.

Wabunge wa Bunge la Tanzania wamegawanyika waziwazi juu ya issue ya Escrow na wengine wakiomba muda uongezwe ili kuwaumbua wale wanaotumika na kambi moja ya urais ili kupotosha umma juu ya fedha za Escrow.

Hapa kuna kambi mbili tena wengine huwa ni maadui lakini ktk hili sakata wameungana kwa mda ili wakimaliza lengo kila mmoja aludi kule kwa zamani. Kuna Kambi ya Mhongo,naibu wake,mawaziri wa zamani wa nishati,Maswi,Werema, Tibaijuka, pinda na wenzao kibao. 

Kuna kambi ya Mzee mengi, mkono, Zito, kafulila na wenzao wakiwemo wahindi kibao wenye Mgongano wa kimasilahi huko wizara ya Nishati. Hapa wengi si kwamba wana Uchungu na IPTL Bali wana usongo na Waziri Mhongo baada ya kuwanyima Vitalu vya Gesi huku Mkono akinyang'anywa Tenda za kisheria ameungana na Mzee mengi kupambana na Mhongo kwa nia ya kupigania Masilahi Yao Binafsi lakini sasa wanasaka Huruma za watu ili wawasaidie kujinufaisha. 

Hilo kundi la Werema wao wanatuhumiwa kujitotea mkwanja wa IPTL peke Yao pasipo kuwamegea akina Mkono ndiyo Maana wahindi wapinzani wa Yule Singasinga mmiliki wa IPTL wamechanga Pesa wakampatia Mengi akawapatia Zito na kafulila ili wapaze Sauti akiamini Kuwa Mhongo atajiuzulu na yeye kujitwalia Vitalu vya Gesi kiulani, Hapa kikubwa ni Mgongano wa Masilahi Kati ya Mengi na Mkono. vs Maswi na Mhongo, Wenye Uchungu na pesa ni Wananchi pekee lakini hao akina Mkono wapo after money tu.MWIGULU AAMUA KUPIGANIA HAKI YA MASIKINI NA WANYONGE KWENYE SAKATA LA IPTL/ESCROW.
AAMUA KUTANGAZA MISAMO WAKE WAZI WAZI MBELE YA MAWAZIRI WOTE.

Dondoo Kutoka Kikao cha Ndani ya Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana Dodoma kilichofanyika Ofisi za TAMISEMI. Kikao rasmi cha kujadili sakata la IPTL/ESCROW namna wahusika watakavyowajibishwa au kuokolewa.

Misimamo ya Mawaziri tofauti tofauti. Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu waziri wa Fedha anatajwa kuwa Waziri wa kwanza kuonesha msimamo wake wazi wazi kuwa Sakata la IPTL/ ESCROW ni hujuma dhidi ya Uchumi wa Nchi.acharuka,AAGIZA MALI ZOTE NA PESA ZOTE ZILIZOLIWA, ZILIZOTAWANYWA ZIKAMATWE.Naibu huyu ambaye mara kadhaa amekuwa akitajwa na vyombo vya habari kwa juhudi zake za kuokoa matumizi mabaya ya fedha na hata Watanzania wengine kuamua kumbatiza jina la Sokoine wa pili ikiwa ni kufuata nyayo za aliyewahi kuwa Kiongozi Makini Nchini hayati Moringe Sokoine.
Mwigulu ndani ya kikao hicho cha siri anatajwa kuendeleza ujasiri wake kuhusu mambo yenye masilahi ya Taifa. Wakati watu na tetesi mbalimbali zilikuwa zinaongelea kujiuzulu, Mwigulu
amejitokeza kwenye kikao hicho na kusema CAG ameshamaliza utata, sasa mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe.

Nanukuu kama nilivyosikia"Tumezoea kusema eti tumewajibisha watu kwa wao kujiuzuru, "Kujiuzuru ni kupewa Likizo ya kwenda kula fedha ulizoziiba"anasema Mwigulu, Hili ni jambo la mazoea,sasa, CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote, na wahusika wote wakamatwe"

Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunt zao zikamatwe, zifilisiwe zirudishwe kwa wananchi. Katika hatua nyingine Naibu huyo anayeshughulikia mambo ya sera, Mwigulu ameagiza mtumishi wa TRA aliyepewa 1.6bilion afukuzwe kazi, akamatwe, na akaunti ifilisiwe fedha irudi serikalini. Pia mitambo ya IPTL ikamatwe irudishwe serikalini.

Utamaduni wa watu kujiuzulu na kuhesebu kuwa ni adhabu ni jambo la zamani, sasa ili kukomesha wizi, uzembe na ufisadi sasa tuwakamate wahusika wote, tuwafilisi na tuwaweke ndani na tuwafunge.

Habari za uhakika kutoka kikao cha baraza la Mawaziri zinasema, jana Mwigulu Nchemba aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri mkuu nakusema kujiuzuru sio adhabu stahiki kwa wizi Mkubwa kama huu wa Mali ya Umma,Hisia hizo zikiwa zimegubikwa na maisha yake halisi ya umasikini aliyokulia na huku akihusisha Wizi wa fedha na hujuma dhidi ya Watanzania Masikini.

Mbunge huyo wa iramba anasisitiza kwa kusema " Tazama wanafunzi, watoto wa masikini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna masikini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai, wazabuni wanauziwa nyumba zao na mabenki huku wakiidai serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzulu? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia masikini? Hapana, "Enough is enough" ndg Waziri mkuu tuwakamate, tuwafilisi, tuwafunge. Pesa na mali virudi serikalini."

Kwa yule mtumishi wa TRA aliyekula fedha za IPTL zaidi ya 1.6 B,Mwigulu akatoa agizo kuwa "Nimemwagiza kamishna wa kodi amfukuze kazi yule wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu, na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe, na wahusika wakamatwe. 

Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga masikini na kuwapa likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini." Taarifa za uchunguzi zunasema tayari TRA imechukua hatua." Naibu Waziri KILIMO Mh.Godfrey Zambi wanusurika Kukunjana na Werema(Mwanasheria Mkuu wa Serikali). Wakati kikao kikiwa kimepanda joto la juu,Mawaziri wakifikia makubaliano kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na madini Maswi na Mawaziri waliohusika ni lazima waachie ngazi,Ndipo Werema alipotaka kumkunja Mh.Zambi baada ya kutoleana maneno machafu dhidi ya mali ya umma.

Madai yanakwenda mbali kuwa,Zambi alikuwa anapigia kelele kuwa inawezekanaje Mwanasheria mkuu kubariki wizi wa Fedha za Umma?.Ni wapi watu wa msoma wakasifika kwa wizi wa mali za Umma?.Chokochoko hizo ndio zilipelekea Ugomvi kati ya Zambi na Werema. Mbali na Mawaziri hao,Mh.Tibaijuka amekuwa Mwizi wakwanza wa IPTL kukubali kuwajibika katika sakata hili mbele ya kikao cha baraza la Mawaziri.

MWIGULU APIGIWA CHAPUO UWAZIRI MKUU
Habari kutoka ndani ya kikao cha siri kinachofanyika na wabunge wasiozidi 15 kimeonekana kuwa na mvutano mkubwa miongoni mwa wajumbe lakini tatizo lililo onekana ni kwamba baadhi ya wajumbe hao wapo kimaslahi zaidi kwani wapo wanao dai kwamba hawawezi kuwatetea wahusika wakati wao hawajapata kitu chochote huku wakizingatia kwamba sasa tunaelekea kwenye uchaguzi na kila mtu sasa anahitaji pesa kwa ajiri ya maandalizi ya uchaguzi jimboni mwake.

Maamuzi yaliyofikiwa iitishwe ( concas ) kikao cha wabunge wa ccm haraka iwezekanavyo ili kupeana misimamo na kuchimbana mikwara kwa wale ving'ang'amizi.

Kama itaonekana shinikizo ni kubwa la kumtaka pm ajiuzuru basi wafuatiliaji wa nyeti wanadai waziri mkuu asitokane na makundi yanayo wania uraisi ili kupunguza mvutano wa kiuongozi. Hivyo basi baadhi ya wabunge waliokuwepo eneo la hoteli ya Dodoma canival leo majira ya saa 5 walisikika wakisema Pm akijiuzulu nafasi hiyo apewe Mwigulu Nchemba kwani kwa siku chache alizokaa wizarani ameonyesha uwezo mkubwa. Hata kutohudhuria kikao kilichofanyika ni shinikizo toka kwa maswaiba wake kwamba asijihusishe na vikao hivyo huenda jina lake likawa moja ya majina yatakayo pelekwa bungeni na kuhitaji kupigiwa kura na wabunge hao .

Sababu hasa inayozungumzwa na baadhi ya wabunge wa ccm wanaopendelea kuja kuburudika hapa dodoma carnival ni kwamba Mwigulu anao uwezo wa kuwarudisha vijana ambao kwa kiasi kikubwa wamepoteza imani na serikali yao pamoja na chama tawala, Sasa sijui kama mawazo hayo ni sahihi..

Saa hizi hapa dodoma ni mwendo wa kubanana na wabunge , ukiona wamesimama wawili au watatu basi unajitahidi kujipitisha pembeni ili upate chochote kinachoendelea juu sakata la Escrow .JAMII FORUMS NA FACEBOOK GROUP YA UMOJA VILLAGE.

No comments: