Tuesday, November 4, 2014

OLE WAKO TANZANIA.
OLE WAKO TANZANIA...


Na Julius Mtatiro,

Taifa lenye vijana walio tayari kuua,
Kuua kwa ajili ya Ukuwadi na Utumwa,
Kuua kwa ajili ya kutumwa na wakubwa,
Matajiri waliogeuza nchi hii Ubwabwa.


Ole wako Tanzania unayechezea amani,
Amani iliyodumu barabarani hadi nyumbani,
Amani imekuwa ghari sasa jaribu vitani,
Kwa kutumia vijana waso maadili ukubwani.


Ole wako chama kubwa kulewa madarakani,
Hakika pakichafuka utakuwa mashakani,
Afrika italia wakubwa mbio ulayani,
Unaanza twamaliza tumechoka asilani.


Ole wenu vyombo dola kwa kushindwa majukumu,
Kwa hakika wananchi watabeba gurudumu,
Gari letu litasonga bila nyinyi kwa ugumu,
Tutalinda Tanzania kwa ushindi wa machungu.

No comments: