Monday, November 3, 2014

NAKERWA SANA NA UJINGA WA WATANZANIANa Yericko Nyerere,

Tujapopita katika bonde la uvuli wa mauti hatutaogopa mabaya kwakuwa gongo lako na fimbo yako vitatuongoza.
Njia ni pana iendayo upotevuni na wanaoiona ni wengi bali njia iendayo uzimani ni nyembamba na waipitao ni wachache.
Wakati wewe unasema methali za kidunia "wengi wape", Mungu anasema "wateule ni wachache".

Nawachukia watz kwa ujinga wao katika jamhuri yao ya muungano wa wajinga!
Kamwe sitachoka kuwafunulia yaliyofichwa ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio halijapata kusikia.

Enyi watu wa jamhuri ya muungano wa wajinga, nanikawaloga?
Ninaposema taifa la wajinga nina maana pana zaidi.
Serikali ya ccm inawabaka mpaka kuwadhalilisha lakini watz tunasinzia tu nakujiimbia wimbo wa tuvumilie tu, hatuchukui hatua kuiwajibisha.

Wizi wa 600 bilioni umefanyika kwa utawala huu wa jk kuanzia 2012 lakini watanzania hawa wajinga ni mabingwa wa ulalamishi, na kuna kukundi kidogo tu cha wajinga mara mia kinachoongozwa na Paul Makonda wanaoweweseka mitandaoni kila dakika kuitetea ccm.
Wiki juzi Mwakyembe kasaini mkataba wenye wizi wa zaidi 400 bilion lakini watz wa jamhuri ya wajinga wapo tu wamelegeza miili tu huku nchi inateketea.

Gesi ya Mtwara inasombwa matani na matani kwenda urusi kinyemela chini ya usimamizi na kusindikizwa na JWTZ huku nchi yetu hata sera ya gesi haijaiandaa, ccm imeanzisha kampuni ya kuchimba gesi na kujitwalia vitalu mhimu kisha kuingia ubia na makampuni ya kigeni. Lakini wajinga mpo tu vibarazani mkinywa gahawa.

Twiga na urefu wote ule anakunjwa mzimamzima na kuingizwa kwenye ndege hadi Dubei, huku nyie jamhuri ya wajinga mmetulia tu.
Ajali za barabarani kwa miezi mitatu tu zimepoteza maisha ya watz 1080.

EPA, MEREMETA, KAGODA, DEEEP GREEN, zote zimechota bot kwa wizi zaidi ya 400bilioni, lakini rais wa wajinga jk anachekacheka tu eti anawaomba warudishe kwahiari, hivi kuna sheria ya nchi hii mwizi anaombwa arudishe kwa hiari tena akiwa anakula ngisi uswahili tu?

Ajabu hakuna anaejua kama pesa hiyo ilirudi kupitia akaunti ipi na ilipelekwa wapi.

Rais anaapa mbele ya umma kuwa Richmond haijui, lakini miezi mitatu baadae Richmond inanumuliwa na Dowans na rais huyohuyo anakuwa shahidi wa mnunuzi mmarekani.

Suala la katiba mpya ccm imewadhihaki maradufu nyie wajinga, mmetoa maoni yenu chini ya tume ya Warioba lakini ccm imeyapeleka toilet na kuwaletea dude liitwa "rikatiba" la Lumumba chini ya Chenge na Migiro, lakini ajabu watz wajinga wanachekacheka tu sawa na mtawala wao.
Wanawachezesha akili tu, mara kikombe cha babu, mara desi, mara dengue, mara viungo vya binadamu, ilimradi tu nyie wajinga muwe bize kwa vitu vya kijinga.


JE WATZ SIO WAJINGA?

No comments: