Sunday, November 2, 2014

MJADALA WA WARIOBA WAHUJUMIWA DAR.

Mwenyekiti wa iliyokuwa tume ya Katiba Mzee Warioba alipokuwa akitoa elimu kwa wananchi juu ya katiba kabla ya rabsha kujitokeza.

Baada ya rabsha kujitokeza ambayo inadaiwa imechochewa na CCM.
Mzee Warioba akitolewa nje ya ukumbi wa Ubungo Plaza mara baada ya fujo. Anaonekana kwa pembeni mratibu wa vurugu hizo ndg. Paul Makonda.Update : wadau wa Jamii Forums walizungumzia tukio la vurugu leo Ubungo Plaza.

(IMENUKULIWA KUTOKA JAMII FORUMS.)

Na Haki sawa,
"Hao vijana wameandaliwa na Paul Makonda , juzi alikuwa Serena hoteli na hao waliokuwa na mabango, ni mkakati ili midahalo izuiliwe kuwa inaamsha hisia mbaya ."

Na Ocampo Four,
"Tokea nizaliwe sijawai kukasirishwa na hili jambo la Makonda kumpiga na chupa Mzee Warioba. Ni utovu wa nidhamu, ni dharau, ni ujinga, ni utoto, ni ukora, ni u.p.mbavu, ni akili ndogo, ni kukosa hekima na misamiati ya namna hiyo kwa hili jambo la Makonda kumpiga na chupa mzee Warioba. Nilikuwepo kwenye eneo la tukio kwa macho yangu nikashuhudia Makonda akimpiga na chupa mzee Warioba, nimeumia sana sana. CCM lazima waruhusu mawazo mbadala ili kujenga Taifa na kamwe kundi moja lenye mawazo yanayofanana hauwezi kujenga Taifa, lazima kuwepo na mawazo huru kwa pande zote katika jamii. 

Ila nasita kusema kama kweli Makonda katumwa na CCM inawezekana kabisa katumwa na Nape au Sita. Warioba ni Kiongozi mstaafu tena katumikia Tanzania kwa moyo wote hivyo vijana kukosa adamu mpaka kufikia hatua ya kumpiga na chupa ni ujinga wa hali ya juu na vijana wa pande zote lazima tukemee hili jambo. Jeshi la polisi tafadhali mlifanyie hili kazi, na Makonda naomba nikupe ujumbe kuwa vijana hatutakaa kimya lazima tutakufanya kwa njia yoyote ile uweze kumuomba Mzee Warioba radhi na taifa kwa ujumla, Leo umefanya kwa Warioba, Kesho utasita kufanya kwa Mwinyi au Malecela au Mkapa...

Nimeuzunishwa sana na hili jambo....Shame on you Makonda"


Na Ocampo Four,
Maneno ya Butiku naomba kunukuu "Huu uhuni uliyofanywa na Makonda haukubaliki hata kidogo, kitendo cha kumpiga Warioba na chupa tunaomba serikali iliangalie jambo hili na pia kuhakikisha katika midahalo mingine huyu muhuni asiwepo, Asanteni" mwisho wa kunukuu. 


Maneno ya Butiku baada ya kikao kuisha akiongea na vijana nje ya ubungo plaza

Naomba kunukuu "Kamwe vijana wa CCM msikubali kuchagua viongozi wanaomtuma Makonda kutenda haya, ni uhuni na ujinga wa hali ya juu" alipoulizwa ni nani wako nyuma ya Makonda, bila kusita akasema Membe na Sita"Na Komando Kipensi,
"Wadau nipo hapa hali ya hewa imechafuka baada ya vijana kuonyesha mabango katiba inayopendekezwa inafaaa

Baada ya tukio hilo vijana wengine ambao wanaona haifai wakawavamia hao wenye mabango kua katiba inafaa....
Wakati mvutano huo unaendelea yule mbunge wa bunge la katiba mwenye ulemavu wa macho nae kavamiwa akaanza kupigwa .......

Wakati haya yote yakiendelea Makonda poul alikua yupo pembeni, baada ya kuona vijana wakimpiga mlemavu akaamua kuingilia kumuokoa mlemavu wakati hayo yote yakiendelea warioba alikua ametoka ukumbini hivyo si sahihi kusema makonda kampiga na chupa warioba.. maana warioba na butiku walitolewa mapema vuguvugu lilipoanza... ocampo ufor wacha uongo ....

Kitendo cha makonda kutaka kumwokoa mlemavu vijana wakamvamia kuanza kumpiga pia makonda.....

Kwa hali ilivyo wanzalishi wa vurugu ni vijana waliwavamia walioweka mabango kusema katiba inafaa.... je wasingewavamia kuna athari gani kwa nini waliwazuia wakati ni haki yao ya msingi kuwakilisha mawazo yao kikatiba...

Je ni busara kumpiga mlemavu kwa kua alishiriki bunge la katiba.... vijana wanampiga mtu asie ona. Je makonda kuamlia ugonvi mlemavu asipigwe kosa lake lipi?

Taifa linaharibika vyama vinatugawa ukisema katiba nzuri wewe ccm ukisema mbaya we ukawa sio sahihi..... 

Bado nipo ubungo unaweza niuliza lolote,,,,

Nimesikitika kumwona okampo ufoo akipotosha umma....kwa siasa za chuki" Na Abdull Kazi,

"Licha ya Paul Makonda kuwa kinara wa kumshambulia Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, wengine walioshiriki katika kuwaandaa vijana walioonekana na mabango ni pamoja na mtru aliyesajili laini yake ya simu namba 0656 5013 17 kwa jina la Valence Kisima.

Huyu bwana ndiye alikuwa anasambaza ujumbe wa kuwataka vijana amabo ni wafuasi na wanachama wa CCM katika vyuo mbali mbali kufika ubungo Plaza leo wakiwa hawana sare za Chama na kuwaeleza kuwa wanaenda kufanya kazi maalum, pia aliwaahidi kila atakayefika atapewa nauli ya kwenda na kurudi baada ya kazi hiyo"
VURUGU ZAJITOKEZA WAKATI WA MDAHALO WA KATIBA MPYA LEO UBUNGO PLAZA.

Na Baraka Mfunguo,

Mjadala uliokuwa unatolewa na waliokuwa wajumbe wa tume ya kurekebisha maoni ya wananchi kuelekea Katiba mpya na kurushwa moja kwa moja na kituo cha ITV umehujumiwa. Mjadala huu ulikuwa ukifanyika Ubungo Plaza ambapo Mzee Warioba alikuwa akiendelea kutoa mada katika kongamano ambalo liliandaliwa na kuratibiwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere. Kongamano hilo lililenga kutoa elimu juu ya mwenendo mzima wa mchakato wa kuelekea kwenye uandikwaji wa katiba mpya kuanzia kwenye tume na uchakachuaji wa bunge maalum la katiba. 

Ghafla wakajitokeza watu wasiojulikana wakiwa na mabango yaliyoandikwa "KATIBA TUMEIPOKEA, TUTAIUNGA MKONO" Ghafla rabsha zikaanza baina ya wafuasi ambao inaonekana wanatokana na itikadi za vyama viwili maarufu vya siasa. Hii ni hujuma kubwa kwa watanzania na wapenda demokrasia na nia fedheha na aibu kubwa kwa wazee wetu.

No comments: