Saturday, November 29, 2014

RAIS AWASILI KUTOKA AMERIKANI
Rais amewasili kutoka Amerikani na kuzungumza na waandishi wa habari kwenye chumba maalum cha watu mashuhuri (VIP) uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere . Baadhi ya watu muhimu waliojitokeza kumpokea ni pamoja na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Didas Masaburi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliachim Maswi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama .

Rais amewashukuru waliokuja kumpokea na amewaomba waliohudhuria kikao hicho kufikisha kwa Watanzania wengine ambao hawajapata firsa ya kuja kumpokea. Anasema kuwa operesheni  yake ya ugonjwa wa kansa ya tezi dume imeenda vizuri na madaktari wamefanikiwa kuondoa ugonjwa.

Kuhusu ya vikao vya Bunge vinavyoendelea  Dodoma kuhusiana na kashfa ya miamala ya Escrow, amesema kuwa hawezi kuyasemea kwa vile hana taarifa za kutosha juu ya yanayoendelea huko.  Rais amesema kuwa pindi atakapopata taarifa rasmi kuhusiana na  yanayojiri huko ataweza kuyasema kama ataona kuwa kuna haja ya kuyasemea.AJALI YA HELIKOPTA DAR YAUA 4Ajali ya Helicopter ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya marubani 3 wa Jeshi la Polish Tanzania. Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala Kaluse , Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa Simba, Pc. Josso Selestine, Na urbanization wa Kiraia Capt. Khalfan. Ajali imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ilala Dar es Salaam. PICHA KWA HISANI YA MROKI.

No comments: