Thursday, October 9, 2014

WAWILI WAUAWA WAKITUHUMIWA UJAMBAZI MKOANI LINDI.Kunradhi: Picha sio nzuri na tunaomba radhi kwa wale ambao watakuwa wamekwazika na picha hizi.

Na Ramadhani Chilemba,

Wananchi wenye hasira kali wamewaua na kuwachoma moto watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Tukio hilo limetokea leo tarehe 08/10/2014 saa 4:00 Asubuhi katika kitongoji cha NAMANDUNGUTUNGU, maarufu kama MANZESE, kijiji cha SOMANGA, Wilaya ya kilwa Mkoa wa Lindi.


Watu hao wameuawa ikiwa ni siku moja tu tangu Alipotekwa, kupigwa na kuuawa Mwendesha pikipiki mmoja, maarufu kama bodaboda aliyeulikana kwa Jina la SELEMANI POMBE Mkazi wa Kijiji cha Somanga siku ya Tarehe 06/10/2014 saa mbilin usiku.
Mwendsha bodaboda huyo alipigwa na kuuawa kisha kunyang`anywa pikpiki yake aina ya SUNLG yenye Namba za usajili T678 CYB.


Tukio hilo limetokea katika eneo la Mitondo kijiji cha Somanga simu.
Mwendesha pikipiki huyo alitekwa na kuuawa alipokuwa anampeleka abiria wake katika kitongoji cha Mitondo na inasemekana abiria huyo alikwenda kukagua mkaa wake. Abiria huyo alifanikiwa kuwatoroka Majambazi hao baada ya kufanikiwa kufungua kamba alizokuwa amefungwa mikononi na miguuni baada ya kumjeruhi vibaya na kumbaka.

Watuhumiwa hao wa ujambazi wanasadikiwa kuwa ndio wanaofanya uhalifu katika maeneo ya NYAMWAGE-MUHORO-MARENDEGO-SOMANGA, maarufu kama Eneo la Vumbi. Wanateka magari,na kujeruhi watu, kulawiti na kuwanyang`anya fedha na mali zingine kama simu, computer n.k .

Jina la mmoja aliyeuawa ni RAMADHANI MAKUNGWA mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa kijiji cha Somanga, na mwingine hatujuweza kupata jina lake lakini kwa taarifa kutoka kwa baadhi ya raia zinasema mtu huyo ni Mwenyeji wa Lindi lakini yupo katika eneo hilo kwa Muda mrefu kidogo.

Kuuawa kwa watu hao kumetokana Na msako mkali ulioendeshwa na wananchi baada ya kukithiri kwa matukio ya ujambazi katika maeneo ya kilwa kama Nangurukuru, Miteja,Kipatimu,Njinjo,na somanga.

 Kwani Mnamo tarehe 03/10/2014 majira ya saa 4:30 usiku, gari zaidi ya kumi zilitekwa na Abiria, madereva na mautingo kuporwa mali na fedha pamoja na baadhi yao kubakwa na kulawitiwa na wengine kujeruhiwa Vibaya.
Tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha limetokea katika kijiji cha SNZA-MITEJA.

Baada ya kuwakamata watu hao kabla ya kuwaua, mmoja alisema wasimuue ataonesha ni wapi wenzao watatu walipo pamoja na pikipiki lakini kutokana na hasira za wanachi waliwaua na wengine wamezagaa katika pori la MIBUYU SABA raia aliyetoa taarifa za kuonekana kwa watu hao na kufanikiwa kuwakamata hao wawili aliwaona watu hao.


Hivyo Mpaka wakati huu msako unaendelea, Wananchi wengi wamezagaa na kuzingira pori lote la MIBUYU SABA kuwasaka hao watatu waliosalia pamoja na pikipiki zilizoporwa.

No comments: