Tuesday, October 7, 2014

UTENDAJI KAZI WA LOWASSA NI KICHOCHEO CHA UONGOZI IMARA TANZANIA .


WATANZANIA NI VIGUMU SANA KUMSAHAU EDWARD NGOYAI LOWASSANa Joseph Goebbles,

Baada ya kuleta ule uchambuzi wa mambo mbalimbali yahusuyo Uchaguzi Mwakani, kazi yangu ya pili ilikuwa ni kutembea mitaani kwa wananchi na kudadisi nini hasa wanachotaka na kutarajia katika uchaguzi mkuu wa 2015. Kitu kikubwa nilichojifunza ni kwamba watanzania ni wavumilivu sana na ni wachapakazi sana. La pili ni hili swala la wagombea wa CCM, wananchi bila kusita wamesema wazi kuwa ni vigumu kwa watanzania kumsahau Lowassa, kama mdadisi nilitaka kujua ni kwa nini wanasema hivyo? Majibu yao yalikuwa kama ifuatavyo........


1. Ujenzi Shule za kata
(Wananchi wanasema): Ni Lowassa huyu huyu aliyesimamia ujenzi wa shule za sekondari za kata Tanzania nzima. Hoja kwamba hazina walimu ni sahihi, lakini lipo swali la kujiuliza lakini kipi bora kutokuwa na vyote viwili, shule na walimu au kuanza kimoja?
Hapa wapo wenye hoja sahihi kabisa kuwa serikali ingeanza na kufundisha walimu kabla ya kujenga shule, lakini walimu hawa hawa iwapo wangehitimu kwa idadi kubwa na kukosa ajira, hoja hii ingegeuzwa na kudaiwa kuwa serikali inapaswa kujenga shule kwanza kabla ya kufundisha walimu. Kwamba Shule zinapokuwepo kasi ya mahitaji ya walimu inakuwa na mashiko (real) badala ya dhahania (imaginary) ila tusisahau kuwa hakuna safari isiyokuwa na mwanzo.


2. Mradi wa maji Shinyanga
Watanzania ni wepesi sana wa kusahau mambo, Sitashangaa kukuta wakazi wa kahama na shinyanga nao wakiwa kwenye mkumbo huu wa akina Diallo. Lowassa alisifiwa kama mkombozi siku za nyuma zilizopita, leo ndiyo tunampiga mawe na vijana wadogo wadogo wanadiriki hata kumtukana hadharani. Wananchi wa Kahama na Shinyanga, Lowassa akiwa waziri wa maji alidiriki Kutofautiana na kuwa wakali mithili ya mbogo kwa WAMISRI kwa ajili ya kuvuta maji ya ziwa victoria kutoka mwanza kwenda Kahama na Shinyanga. Hili jambo sio la mzaha ilihitaji kiongozi mwenye uwezo wa kudhubutu, ilihitaji kiongozi mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu, kitu alichofanya Lowassa na leo maji yapo Shinyanga. (Alidiriki kuuwambia WAMISRI nanukuu "kama munaona mazao yenu ni bora kuliko wananchi wangu, basi hamna tofauti na wauaji wakubwa katika dunia hii na mnastahili mtengwe na dunia nzima, nilisema na narudia kusema maji lazima watanzania tuyatumie kwa namna yoyote ile" (Majira may 22, 2005).


3. MAAMUZI MAGUMU DHIDI YA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA
Leo hii ninapoandika huu uzi tarehe 7, october, kama si Lowassa, viwanja vya mnazi mmoja vingekuwa magorofa ya akina Baghdad (wahindi), kwa wale wananchi waliyokuwepo 1994 wanakumbuka hili swala vizuri sana. Ni swala lililowazi na tunajua jinsi Lowassa alivyosimamia kidete bungeni mwaka 1994 na kuamua uzio wa mabati uvunjwe uliokuwa umezungushwa viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam, hakusubiri hata kumjulisha rais ila ulikuwa uamuzi sahihi kwa wakati sahihi.....Leo mashirika ya umma, mashirika binasfi na hata wanafunzi wanafanya matamasha mbali mbali katika uwanja huo, chama tawala kinafanya matamasha katika uwanja huo ila cha ajabu viongozi hao hao wanapokuwa mnazi mmoja wanaweza diriki hata kumtukana Lowassa mtu aliyeweka rekodi ya kuurejesha uwanja huo ila ni wa kuwasamehe kwani either hawajui historia ya nchi hii au wanapuuza historia ya nchi hii.


4. JENGO LA PPF
Ni Lowassa huyu huyu alifuta umiliki wa viwanja vya tajiri mmoja anayetamba jijini Dar es Salaam ambapo leo ndipo yamejengwa majengo ya PPF, International House na majengo mengine kadhaa. Leo hii haya majengo yamekuwa msaada mkubwa kwa shirika la umma kutoa ajira, na kutunza fedha za wajane, wakulima, wanafunzi nk badala ya kumilikiwa na mhindi moja. Leo hii PPF wamepata eneo la kutolea huduma kwa jamii, najiuliza bila Lowassa kurejesha eneo hilo leo PPF wangelikuwa wapi. kama mdau anayefaidika na PPF bila shaka naomba nitoe shukrani zangu kwa Lowassa.....Daima tutakukumbuka


5. City Water Saga
Ni Lowassa huyu huyu tunayembeza, aliwafukuza nchini kampuni ya City Water mwaka 2005, waliposhindwa kutimiza masharti yaliyokuwamo kwenye mkataba. City water walikwenda mahakamani, lakini hasilani hawakushinda kesi na wakatakiwa kulipa serikali ya Tanzania sh. billioni 15. Nakumbuka mkutano wao (City water, wadau wa maji Dar es Salaam, wakurugenzi wa Dar) "Lowassa alirudia tena na kuwaambia kama munaona mumeonewa kimbieni mahakamani ila huduma yenu ni mbovu hatuwezi kuvumilia, tena sasa hivi nawapa dereva wangu awapeleke maakamani kabla ya saa tisa na nunu mkafungue kesi, Hatuwezi kukubali upuuzi upuuzi, hii ni nchi yenye wananchi wanaoitaji huduma iliyo bora"; mwisho wa kunukuu


6. USIMAMIZI IMARA
Kwa aina za viongozi tulionao kuanzia mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na hata wakurugenzi wanahitaji usimamizi mkubwa sana, na katika karne hii hakuna aliyeonyesha karma hiyo zaidi ya Lowassa, wananchi wanakumbuka jinsi alivyokuwa mkali kwa hao watendaji na hata kudiriki kusimamisha baadhi yao ilimradi maslahi ya wananchi yatekelezwe kwa maendeleo ya nchi. Wananchi waliamini na wataendelea kuamini kwamba mtu kama Lowassa kama kweli tulihitaji kuyafikia maisha yaliyo bora, alifaa na atazidi kufaa katika historia ya nchi hii. Nani asiyefahamu kuwa kuanzia mawaziri mpaka mtendaji wa kijiji, alipokuwa waziri mkuu Lowassa akitokeza mahali watu wanatafutana na hata kula kona.
7. UJENZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI
Katika siasa za chama cha mapinduzi na ya nchi kuwa rais wa nchi tu hakutoshi ila kuna swali la kujiuliza je unaweza kuwa mwenyekiti wa chama tawala (kumbuka kofia hii ni moja), nafkiri hapa kwa wale wanachama wa ccm watanielewa (which I am not), ccm kama chama ni taasisi kubwa sana na yenye changamoto nyingi sana, ni taasisi yenye kelele nyingi, majungu, fitina, njama chafu nk hivyo ni watu wachache walio na uwezo wa kuwa mwenyekiti wa chama na at the same time kuwa rais, kama hauko imara sio siri moja kati ya hizo itakupwaya. Wana ccm je ni nani leo ana uwezo na nguvu ya kuhamasisha, kuimarisha chama na jumuiya zake? kama sio Lowassa........katika hoja hii namkumbuka sana JACKSON MAKWETA kuhusu aina ya viongozi watakaotuvusha na wenye uwezo wa kuwa mwenyekiti na at the same time kuwa rais. Makweta alisema hili tokea 2008 kuwa ni Lowassa tu aliye na uwezo wa kuwa na kofia mbili na hizo taaisisi zote zikawa stable. Aliongeza na kusema tunamuitaji mtu angalau asiwe kama Adolf Hitler, lakini Lowassa anatufaa sana wakati huu, hili liliongewa pia na kiongozi wa kiroho Askofu Laizer.
Bwana Edwin Ochele Ochwera "mkazi wa Tarime anaeleza kuwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wanaishi kama Mungu mtu katika eneo lake la kazi, mjane aliyeshindwa kutoa mchango wa shillingi elfu 5000 ya ujenzi wa maabara anawekwa ndani kwa siku 14 na mkuu wa wilaya bila melezo au mwalimu anayekatwa shillingi 10000 ya ujenzi wa maabara bila ya ridhaa yake Hapa Lowassa asingekubali na hata kuvumilia huu upuuzi; Kwa hakika tunamkumbuka sana Lowassa".....
Bwana Otitmach Gati mkazi wa Shirati alisema, Ndani ya ccm lipo kundi la watendaji wenye kufanya kazi kwa mazoea, hili swala linatufanya daima kutomsahau Lowassa. Najua wachache wanamchukia Lowassa kwa utaratibu wake wa kutofumbia macho maovu, wanaona utaratibu wake wa kuweka mambo wazi/hadharani ni kikwazo kwa wahuni ndani ya chama....
8. Richmond
Hili swala limeongewa sana sana, wengine wameongea kwa kufanya analysis, wengine wanaongea kwa mihemuko ya kihisia na hata wengine kwa mihemuko ya kimwili. Sitaki kuzungumzia hili swala tena kwani limeongewa tokea 2008, na kwa bahati nzuri tumepata fununu kuwa muda sii mrefu mhusika ambaye kamati ya Mwakyembe haikumhoji yeye binasfi ila baadaye ikamhukumu ataliongelea hili swala muda ukifika. kwangu mimi kubwa naona haikuwa sahihi kuacha kumhoji Lowassa kama waziri mkuu, haitaji ujasiri kulisema hili la kutompa fursa ya kumhoji Lowassa, kwa hulka ya ubinadamu ni rahisi kwa wajumbe wa hiyo tumekujitetea, lakini hapo ndipo umimi (egoism) unathibitika.
Biblia takatifu na Quran usema, mtendee mwenzio sawa na utakavyo utendewe wewe. na pia usema kipimo hicho ukitumiacho kumpima mwenzio, ndicho kitakachotumika kukupimia haki yako mbele ya safari; kisheria kuna dhana ya natural justice. ila all in all watanzania kwa sasa wameanza kujua ukweli na tunatumaini pindi Lowassa atakapoongea tena tutajua mengi (baada ya kuliweka wazi katika mkutano wa NEC na kusema uongozi wake wa juu ulikuwa unajua kila kitu kuhusu mchakato wa Richmond....)....

9. Lowassa atokwa machozi Chimwaga
Hili ni mahususi kwa wana CCM, hasa kwa wale wanaojaribu kuleta ugomvi na kuaminisha jamii kuwa kuna ugomvi kati ya Lowassa na JK. Naomba kuwaambia kuwa these people are still friends na wametooka mbali... nakumbuka mwaka 1995 baada ya JK kushindwa katika kura za maoni na Mkapa Bwana Lowassa alikuwa kituko pale Chimwaga alipododosha machozi wazi kabisa mbele ya wananchi, JK najua anasoma huu uzi au wapambe wake watasoma huu uzi, naomba mumkumbushe inawezekana kwa mambo mengi aliyonayo kasahau kwa namna moja au nyingine. Ni Vijana hawa wawili walikuwa mbele katika kila harakati tokea 1994/1995; historia ya JK katika mbio za urais katika miaka yote haikamiliki bila kutaja jina la Lowassa, Pascal Mabiti, Rostam Azizi, na Azizi Aljabry.


10. Chakula cha Njaa
Ni Lowassa huyu huyu aliyesimamia chakula katika kipindi cha njaa (kumbuka /2006/07kilikuwa kipindi cha ukame sana sana, uchumi wa dunia kushuka hivyo kuathiri hasa nchi masikini, uzalishaji kupungua nchini, na kilimo kushuka kwa asilimia 7.9% ila kwa umahiri wa Lowassa alihakikisha pamoja na hali hiyo wananchi wake hawafi na hata kulala njaa, alisimamia usambazaji wa chakula cha njaa kila tarafa, kila kata, na zaidi ya yote kila kijiji. Vile vile ni Lowassa huyu huyu aliyeleta jitihada kubwa sana katika kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam kwa utaratibu wa njia tatu, kuna watu wanasema hizo njia zilikuwa zinauwa watu sana, ila jamani hivi mpaka swala la kutoa elimu ya usalama barabarani mpaka waziri mkuu ndiyo atufanyie, kazi ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ni nini hasa?. Kwamba leo misingi yote ya barabara kupanuliwa za jiji la Dar es Salaam ni kwa vission aliyoakuwa nayo na yeye kuiasisi.....

Ni swali la kujiuliza sote, je Lowassa angekuwa madarakani mpaka sasa, unafikiri tungekuwa wapi kimaendeleo?

No comments: