Wednesday, October 8, 2014

TAASISI ZAPIGWA KUFULI KUSHIRIKI ZABUNI ZA SERIKALI NA PPRA
Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) majina 10 ya taasisi na halmashauri ambazo zimeonekana kuwa na viashiria vya rushwa katika matumizi ya fedha za Serikali mwaka 2013/14.

Bodi hiyo pia imezifungia kampuni 23 kushiriki zabuni za Serikali, huku ikiagiza menejimenti ya PPRA kufanya uhakiki kwa taasisi 19 ambazo katika ukaguzi, zimeonyesha kufanya ununuzi unaotia shaka wa Sh1.7 bilioni.

Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Marten Lumbanga alisema jana kuwa taasisi zilizoonekana kuwa na viashiria vya rushwa katika ununuzi ni:-
 1. Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
 2. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
 3. Halmashauri ya Jiji la Mwanza
 4. Halmashauri ya Kondoa
 5. Halmashauri ya Monduli
 6. Halmashauri ya Kilwa
 7. Halmashauri ya Maswa
 8. Halmashauri za wilaya ya Kigoma
 9. Halmashauri ya Kibondo
 10. Halmashauri ya Tarime
 11. Halmashauri ya Musoma
 12. Halmashauri ya Ukerewe
 13. Halmashauri ya Maswa
 14. Halmashauri ya Kishapu
 15. Halmashauri ya Kilindi
 16. Halmashauri ya Lushoto
 17. Halmashauri ya Mkinga
 18. Halmashauri ya Bunda
 19. Halmashauri ya Butiama
 20. Halmashauri ya Rorya
 21. Halmashauri ya Kondoa
 22. Halmashauri ya Songea
 23. Halmashauri ya Singida
 24. Halmashauri ya Mwanza
 25. Halmashauri ya Iramba
 26. Mamlaka ya Maji na Mazingira Lindi
 27. Manispaa ya Kinondoni
 28. Manispaa ya Musoma
 29. Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Lindi
 30. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa PPRA, Dk Laurent Shirima alisema kuwa tatizo kubwa katika ununuzi wa umma ni watendaji kutokuwa makini au kutofanya kazi zao kwa uaminifu. Alisema PPRA imekusudia kuwaita wakuu wa taasisi zilizofanya vibaya ili kujua tatizo.


No comments: