Wednesday, October 8, 2014

LEO NI MAKABIDHIANO YA RASIMU YA KATIBA YA BUNGE MAALUM LA KATIBA.Uwanja wa Dodoma umefunguliwa tangu asubuhi saa 12 asubuhi na kuna idadi kubwa ya Askari kuimarisha ulinzi ndani na nje ya uwanja.

Kuna shamrashamra mbalimbali zikiongozwa na vikundi vya uhamasishaji vya Chama cha Mapinduzi.

Pia kuna Idadi kubwa ya Wageni kutoka mikoa mbalimbali waliokuja kwa usafiri maalum wa mabasi kushuhudia tukio hili la kukabidhiwa Rasimu ya Bunge la Katiba.

 Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA unaoundwa na vyama vikuu vitatu yaani Chadema,CUF na NCCR hautahudhuria sherehe za makabidhiano ya Rasimu ya Bunge Maalum la Katiba.

 Haya yanatokea wakati kukiwa na mgawanyiko mkubwa Tanzania na Visiwani kuhusu rasimu iliyopendekezwa na Tume na ile iliyopendekezwa na Wabunge wa bunge maalum la katiba ambao idadi kubwa walikuwa ni wa Chama Tawala Pia rasimu ambayo ni ya Upande mmoja hasa ikizingatiwa serikali ya Zanzibar imegawanyika makundi mawili Kundi moja la CCM likiunga mkono Rasimu ya Bunge  na la pili la CUF likilaani na kupinga  hii ambayo inaonekana inawakandamiza Wazanzibari .

Uamuzi  wa mwisho ni wananchi wakati wa kupiga kura ya maoni. Kanisa Katoliki kupitia kwa Makamu Rais wa TEC Askofu Severine Niwemugizi wameshaweka wazi msimamo wao wa kura ya HAPANA huku Shura ya Maimamu kupitia Katibu wake Sheikh Rajab Katimba nao wakiweka msimamo wao wa kura ya HAPANA.

No comments: