Wednesday, October 22, 2014

KILA LA HERI MTOTO WA MKULIMA.

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo PindaWaziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, ametangaza niya yake ya kuwania urais katika uchaguzi ujao .

Pinda aliyasema hayo mjini London ambako mkutano wa viongozi unaoangazia uwekezaji zaidi katika bara la Afrika unaendelea .

Viongozi hao wanatumaini kuyashawishi mashirika makubwa zaidi ya uwekezaji, katika mkutano huo wa siku mbili, kwamba yanafaa kuwekeza zaidi katika mataifa ya Afrika, hasa Nigeria, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ghana na Togo


CHANZO: BBC


Mtazamo:

Wenyewe wahafidhina wanailinganisha CCM sawa sawa na bahari na wanachama wake kama samaki wakubwa kwa wadogo awe papa awe nyangumi. Ukimtoa samaki baharini ukamtosa mchangani thamani yake imeisha. 

Kila la heri wote waliotangaza nia. Blogu hii haina mgombea inayempigia debe. Blogu inaheshimu mawazo na haki za wahusika waliotangaza nia yao ya kugombea  uchaguzi mkuu 2015 kama haki ya msingi na inaheshimu misimamo yao, hoja zao pamoja na itikadi zao ndani na nje ya CCM.

No comments: