Wednesday, October 8, 2014

KAZI NA DAWA.

Update:

Polisi Mkoani Kagera imewafukuza kazi Askari wake watatu kwa kuweka picha za mahaba kwenye mitandao ya kijamii. Askari hao walikuwa wanafanya kazi kikosi cha usalama barabarani Wilayani Missenye.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Henry Mwaibambe amesema picha hiyo sio ya kuchakachua na ilipigwa na askari mwenzao ambaye pia amefukuzwa kwa kuwa kitendo hicho kimelidhalilisha jeshi la Polisi
.


Mtazamo Wangu:

Kuwafukuza hawa jamaa sio dawa hasa ukizingatia ukubwa wa kosa lenyewe. Wangeitwa na kuonywa. Yapo makosa mengi yanayolidhalilisha Jeshi hili sio kosa la kumfukuza mtu kazi na kumharibia Maisha. Waonywe na kukumbushwa miiko ya kazi zao.

 Kuna kesi nyingi sana za wakubwa za kutembea na hawa maaskari wadogo wa kike wakiwa depo ama wakitoka depo tena kwa lazima lakini kwa sababu ni ishu za wakubwa na kwa sababu kila kitu ni amri ya jeshi, hakuna kuuliza. Isitoshe hili ni suala la hiyari kilicholeta utata labda ni hayo Magwanda.

No comments: