Saturday, July 12, 2014

WASICHANA MIKOA YA KUSINI JIHADHARINI NA MBINU HII YA MAUAJI

 
 
 
Wimbi jipya la mauaji ya wasichana limesababisha vifo vya wasichana saba wilayani Nachingwea mkoani Lindi baada ya kubakwa na kunyongwa kisha kuwekewa vijiti na chupa kwenye viungo vyao vya uzazi.

Gazeti la HabariLeo linaripoti kuwa, katika kipindi cha miezi minne iliyopita wasichana wamekuwa wakipigiwa simu nyakati za usiku na wanapopokea wito wa simu hizo na kukutana na wale waliowapigia simu, matokeo yake huwa ni kubakwa, kunyongwa na kuwekewa vijiti ama chupa katika sehemu za siri.
 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amebainisha aina hiyo ya mauaji jana wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine alipofika kuwatazama majeruhi ambapo alisema kuwa mauaji hayo yanaendelea na juzi, mwingine aliuawa katika mazingira yayo hayo.

Alisema, 
"serikali ya wilaya ilishatoa namba za simu kuwa unapopigiwa simu mtoto wa kike fanya juhudi kumjulisha mwenzako au piga simu kituo cha polisi ili kuweza kukabiliana na watu hao wanaotoa roho za watu."
Mwananzila alisema kuwa binti mmoja aliyepigiwa simu na kundi hilo, aliamua kupiga simu kituo cha polisi na ndipo mtego ulipowekwa. Baada ya yeye kutoka nje, polisi walikuwa wameshazingira maeneo hayo. Watuhumiwa walipomfuata, binti alianza kuvutana nao, hatimaye Polisi wakawatia mbaroni.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaonya mabinti hao na kusema: 
“ni makosa kwa wasichana kutoka nje baada ya kupigiwa …
"kinachotakiwa kwanza mjulishe mwenzako, lakini unafanya siri madhara yataweza kukutokea, hususani watoto wa kike".CHANZO: WAVUTI KUTOKA   GAZETI LA  HABARI LEO

No comments: