Thursday, July 24, 2014

MAONI YA MWANAZUONI: MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA CHANGAMOTO YA MUUNGANO.“MIMI NIMEJIFUNZA KATIKA POLITICAL SCIENCE (SAYANSI YA SIASA) KUWA NCHI INAPOKUWA MOJA KUBWA, BASI UCHUMI WAKE UNASTAWI NA WATU WANAPATA MAENDELEO YA KIUCHUMI KULIKO KUWA NCHI NDOGO,”

Mbona Singapore ni nchi ndogo sana isiyokuwa na mtaji mkubwa wa watu na ardhi lakini yenye maendeleo makubwa kuliko nchi zake jirani Malaysia na  Indonesia zenye mitaji mikubwa ya watu na mali asilia?. Mbona Rwanda au Malawi ni matajiri sana kuzidi mikoa mingi ya Tanzania ambayo mingi ni yenye utajiri watu na mali asilia mkubwa zaidi kuliko zilizo nao Rwanda au Malawi?!


Nchi ndogo ndogo zikiunganishwa pamoja na kuwa moja kubwa kunawafanya watu wake kuwa waliolewa mtaji mkubwa wa nguvu watu na mali asilia na hivyo kuwa ni wanotegemea zaidi uridhi wa mali kwenye maisha yao ya kujitafutia maendeleo ikilinganishwa wananchi ndani ya nchi kubwa ambao mtaji mdogo wa nguvu watu na mali za uridhi unawalazimisha kutegemea zaidi akili, bidii na maarifa kwenye maisha yao ya kujitafutia maendeleo.


Pia, kuwa sehemu ya nchi kubwa jirani kungezifanya nchi ndogo ndogo kama Singapore, Taiwan na Japan kungezifanya ziwe na maendeleo madogo kuliko zilizo nayo kwa sasa kutokana na migogoro itakayosababishwa na tamaduni zisizopikika kwenye chungu kimoja zipikike humo; ushindani wa kibiashara na maendeleo yake kiuchumi kupotea; na ndogo kupoteza uvutio wake kwa wawekezaji wanaoogopa riski nyingi zinazoambatana na nchi kubwa.


Ni kweli kabisa kwamba umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu kwa hili la umoja wa nchi iwe ni ushirikiano (shirikisho) na sio ungano (nchi kuungana kuwa moja).


Faida na athari zitokanazo na nchi kuungana na kuwa moja ni hizo hizo za familia za wanandugu ( wazazi, wadada, wakaka na watoto) kuamua kuwa karibu kwa njia ya kujijengea jumba moja kubwa litakalotumiwa na familia zote badala ya kila moja kujijengea nyumba yake ndogo na hivyo kutenganisha ya familia yasiyopikika kwenye chungu kimoja na kuunganisha yale yanayopikika chungu kimoja.
Nadhani umuhimu wa kuwa na muungano shirikisho badala ya muungano nchi moja au mbili utakuwa umeeleweka.


Dk A. Massawe

No comments: