Saturday, May 10, 2014

VITA YA GESI BAINA YA VIGOGO NA PROPAGANDA ZA KISIASA.Kutoka Mtizamo Huru.

BAADHI YA WABUNGE KUTUMIKA KUMUONDOA MUHONGO NA MASWI WIZARANI Na. Japhari Mghamba,

Wapo baadhi ya wabunge kutoka katika vyama vya upinzani na chama tawala wanaotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa hapa nchini kuratibu na kufanikisha zoezi la kumuondoa waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo na katibu mkuu wake Bw.Eliakim Maswi katika wizara hiyo,

Wafanyabiashara hao wamekuwa wakifanya majaribio kadhaa yenye lengo la kufanikisha dhamira ya kuwaondoa viongozi hao,sote tunakumbuka mgogoro wa kigogo mmoja tajiri na waziri Muhongo uliopelekea Prof.Muhongo kumvua nguo hadharani pale alipotaja umiliki wake katika rasilimali za taifa,

Prof.Muhongo na Maswi wamekuwa ni viongozi wa kupigiwa mfano katika usimamizi na uongozi wa rasilimali za taifa hapa nchini,kwa kipindi kifupi pale wizarani wameweza kuziba mianya ya Rushwa na Ufisadi wizarani katika idara,vitengo na mashirika yaliyo chini ya wizara yao.
Katika mpango kabambe wa kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinamilikiwa na serikali kwa lengo la kunufaisha Watanzania wote hususani wale wenye kipato cha chini wizara imelikabidhi shirika la maendeleo ya petroli na gesi nchini TPDC kuwa mshirika katika ushindani wa kibiashara ndani na nje ya nchi.

Juhudi za viongozi hao zimekuwa mwiba kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao walikuwa wakitumia mianya hiyo kuliibia taifa,kunyang’anya rasilimali za umma na kuzifanyia udalali,Wafanyabiashara hao wamekuwa wakilia kila mara katika warsha,makongamano na katika vyombo vya habari walioandaa wao au iliyoandaliwa kuwa wazawa wanaonewa,Neno “UZAWA” limekuwa ndio silaha yao pale wanatafuta huruma ya Watanzania,

Wafanyabiashara hao wakiongozwa na kigogo anayemiliki Dar Es Salaam tatu wameamua kubadili mfumo wa mashambulizi kwa Prof.Muhongo sasa wameamua kuandaa baadhi ya vijana na kuwapatia Smart phone kwa lengo la kuendeleza propaganda kwenye mitandao ya kijamii kama Jamii forum,Mtizamo huru,Facebook,Twitter,Tanuru la fikra,Fikra huru na Whats app.


Kama hiyo haitoshi mtandao huo wa wafanyabiashara wakubwa umeendelea kutoa fedha kwa wabunge hao na ushahidi uliopo ni msiba wa hivi karibuni wa mzazi wa mbunge mmoja nyanda za juu kusini aliyeambatana na mwenyekiti wa kamati moja ya bunge inayohusika na masuala ya kifedha,mwenyekiti wa kundi la UZAWA linalomiliki Dar Es Salaam tatu alitoa kiasi fulani cha fedha katika mazishi ya mzazi wa mbunge huyo.


Wabunge hao wamekwishaanza kuutekeleza mkakati baada ya kupewa masurufi na mataikuni hao wa kundi la UZAWA,mmoja miongoni mwa wabunge hao ni Mh.Kafulila aliyeandaliwa taarifa inayoitwa ufisadi wa IPTL inayohusisha vigogo kadhaa akiwemo waziri na katibu mkuu wake.
Mkakati unaosukwa ni kuwahusisha na baadhi ya watu wengine waliotajwa kama vigogo kwa lengo la kuficha dhamira,lakini mkakati wa dhani ni kuwang’oa waziri na katibu mkuu wake.


Kafulila amekwenda mbali zaidi akidai kuwa anaushahidi lakini ukweli ni kwamba wapo wabunge anaoshirikiana nao katika mkakati huo,si wabunge tu wapo pia baadhi ya wattumishi wizarani wasio na uzalendo waliopo kwa maslahi binafsi kwa lengo la kughushi nyaraka na kutengeneza uongo na uzushi ili kutimiza mkakati huo.


Ukweli ni kwamba kila kila kitu kimefanyika kisheria juu ya sakata hili la IPTL,Mahakama iliamua kuwa TANESCO iilipe IPTL,fedha hizo zinazotoka BOT ndio fedha halali za umeme wa IPTL uliokwenda TASNESCO,Jambo hili nila muda mrefu kabla Prof.Muhongo hajawa waziri na jambo ambalo lipo kisheria halikuanza leo lakini lazima tujiulize kwanini sasa?


Nilazima Watanzania wajue kuwa wapo baadhi ya wabunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamegeuza nafasi zao kuwa mtaji wa kusaka tonge ndio maana wengi wao hata bungeni wamekuwa wakibip bip kuhudhuria vikao,
Hayo yote yanatokea kutokana na viongozi hao kufungia wizi na ulaji wa wafanyabiashara hao na baadhi ya watumishi waliokuwa wakipiga madili wizarani,Watu hao wamekasirika sana hivyo ni lazima Watanzania tuungane kulipigania taifa letu kama waziri mkuu alivyosema leo bungeni kuwa tumuchie mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali afanye kazi yake jibu atakalotoka nalo ndio ukweli juu ya jambo hilo


Lakini bado nasisitiza kuwa lazima tuwe makini sana na wabunge wetu,viongozi wetu,vijana wasiokuwa na ajira na matapeli wa mjini wanaosubiri kuhongwa ili waweze kuishi mjini.ni lazima tufunge mjadala sasa Kafulila na wenzako mjikite kujadili bajeti msubiri taarifa ya CAG na TAKUKURU na kama tuhuma zenu ni uongo basi nanyi mjiuzulu na hatua nyingine za kinidhamu zichukuliwe juu ya wale wote wanaoishi kwa kuzusha na kupakaza uzushi na uongo kama Kafulila na wenzake.

No comments: