Thursday, April 10, 2014

MTAZAMO KATIKA TAALUMA YA UCHUMI TANZANIA NA UKUAJI WA UCHUMI NIGERIANa Ben Wa Saa nane,

 Wanataaluma wa Uchumi Dr.Honest Ngowi,Wanasiasa Vijana wenye Taaluma za Uchumi Mwigulu Nchemba,Zitto Kabwe na wengineo tunahitaji sana kujifunza kwa Mwanamama Ngozi Okonjo-Iweala.Waziri wa Fedha na Uchumi wa Nigeria,Msomi wa Harvard aliyeona umuhimu wa Rebasing at this Material time.Ilikua ni jambo la kushangaza sana kwa miaka 24 Nigeria haijawahi kupiga calculations zenye weledi kuhusu uchumi wake na ujazo wa Masoko yake.Katika kipindi hiki ambacho Nigeria na Afrika Kusini zinachuana kiuchumi na katika ushawishi wa siasa za kimataifa hasa kwa Afrika ameamua kufanya kazi ya ziada .Kwa sasa anaweza kupanga mfumo mzuri wa uchumi tofauti na ilivyo nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania ambayo kabisa ina unplanned economy(Uchumi Holela).Huwa ninashangazwa sana na wasomi,Wanasiasa na vyama vya upinzani na chama tawala vinapotoa takwimu za kiuchumi kwa unplanned economy kama Tanzania.How accurate they are?Kulishana Takwimu na kupalilia uongo tu.

Nigeria sasa imetangazwa kuwa Taifa lenye uchumi Mkubwa Africa(The largest Economy) na kuipita Afrika Kusini.
Pato Ghafi la Ndani la Nigeria limefikia Dola Billion 509 huku lile la Afrika ya Kusini Likifikia Dola Bilioni 322

Kwa kawaida nchi nyingi hupima ukuaji wa uchumi wake kwa kufanya calculations kuangalia mabadiliko katika GDP yake kwa muda wa kila baada ya miaka 5 .Nigeria haijawahi kupiga hesabu hizo tangu mwaka 1990 yaani takribani miaka 24 iliyopita.

Kwa mujibu wa Idara ya Takwimu ya Nigeria,Wanauchumi wa nchi hiyo wameongeza sekta ya Mawasiliano na Filamu kwenye Takwimu.Ni dhahiri kuwa soko la Filamu la Nigeria lina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.Soko la Filamu la Tanzania linachangia kiasi gani?Nigeria walifikaje hapo?
Nigeria ilikua ikionekana kama taifa linalotegemea zaidi Uuzaji wa mafuta na ilikadiriwa kuwa pato la mafuta huchangia asilimia 32 kwenye GDP lakini ripoti ya wanauchumi juzi imeonyesha sasa pato la mafuta huchangia Asilimia 15 tu ya pato ghafi la Ndani(Gross Domestic Product).

Je,Ni nani anayeweza kusema kwa uhakika kuwa Dhahabu,Almasi na Gesi huchangia asilimia ngapi na hata Gesi ya Mtwara ina ujazo gani na inatarajia kuchangia asilimia ngapi ya pato la Taifa?
-Ripoti ya Juzi imeonyesha utegemezi wa kilimo katika kuchangia pato la Taifa nchini Nigeria umepungua.Kwa wanataaluma wa uchumi wanaelewa kuwa kupungua kwa utegemezi wa sekta ya Kilimo katika ukuaji wa uchumi maana yake Uchumi unapiga hatua kinyume na wengi wanavyofikiria.Nchi nyingi za daraja la kati hutegemea sekta ya viwanda kwa ukuaji.Inaitwa Secondary Economy na zile zilizoendelea duniania hutegemea sana huduma(Service) inaitwa Tertiary Economy.

Nchi inapopiga hatua kuondokana na utegemezi wa kilimo na kuingia katika uzalishaji wa viwandani(Manufacturing ) zaidi maana yake inapiga hatua zaidi kuelekea uchumi ambao unategemea Huduma(Services industry) kama Mabenki,Insurance,Hosipitality n.k.Nchi kama Marekani na Uingereza utegemezi wao kwa Kilimo ni chini ya Asilimia 3 ingawa zaidi ya nusu ya population ya dunia hutegemea kilimo.Si kwamba nchi ni maskini kwa kuwa inategemea kilimo bali wananchi wanategemea kilimo kwa kuwa ni maskini na wako kwenye kundi la wenye kipato cha chini (Low income earners).

Tanzania tunafanya mzaha.Tupo tupo tu kwenye kilimo na kubadili misamiati.Kilimo cha kufa na kupona,Siasa ni kilimo,Kilimo ni uti wa Mgongo,Kilimo kwanza n.k.Hatuna nia ya dhati kugeuza kilimo chetu kuwa commercial. Inatia uchungu na hasira kuongozwa na watu ambao hawako ambitius.Hatuna visionary leaders.Hatuna viongozi wenye ambitions na kwa bahati mbaya,ukweli Mchungu ni kuwa wanatoa reflection ya watu wanaowaongoza maana viongozi wanatoka miongoni mwetu.Ni lazima tukatae kuendekeza Status Quo.Unless we change or overthrow the Status Quo,still tutabakia kuwa Mashabiki wa kushangilia mchuano kati ya Nigeria na Afrika Kusini tu.Tukitoka hapo tunahamia Kwenye ushabiki wa Bafana Bafana Vs Super Eagles au Man Utd Vs Arsenal.Watawala ndio wanapenda hivi.Nasi tunakubali.

-Sisemi kuwa Nigeria na South Africa ndio wamefika,bali nafurahi na kutamani nchi yangu siku moja iwe miongoni mwa Taifa Kubwa kiuchumi na ambalo wananchi wake wanajivunia utaifa wao.Nchi ambayo kila mtoto anapata elimu bora,wanawake wanajiona kuwa salama katika mazingira ya uzazi.Nchi ambayo kila Mwanaume akiamka asubuhi hafikirii tutakula nini mimi na familia yangu leo bali afikirie ni shule gani bora ya kumpeleka binti yangu au niwekeze wapi kwa maendeleo ya familia yangu.

-Ni kweli pamoja na Nigeria kuwa na uchumi mkubwa haimaanishi wananchi wake sio maskini.Sisi tunataka kwenda Beyond hapo.Leo hii pamoja na kuwa na GDP kubwa lakini pato la Mwananchi linakadiriwa kuwa Dola 2,688 huku Afrika Kusini wananchi wake wanakadiriwa kuwa na pato(Per capital Income) linalofikia Dola 7,500 kwa mwaka.Population ya Nigeria zaidi ya watu Milioni 170 inasababisha per capital income iwe chini .South Africa ni fraction ya 1/3 ya population ya Nigeria.Hata hivyo kwa Nigeria hiyo ni advantage kwa long run.Ina potential market kubwa.They need to work hard ili watu wake wawe na purchasing power kubwa.waimarishe Afya,Elimu na Miundombinu pamoja na taasisi za fedha.

-Sasa hivi kutakua na mchuano mkali kati ya Nigeria na A.Kusini kuhusu nafasi ya Afrika Kusini kwenye kundi la nchi tajiri 20 (G20).Afrika kusini ni Mwanachama,je Nigeria haustahili nafasi?
-Uhalali wa muungano wa Masoko makubwa yanayoibukia duniani wa BRICS(Brazil,Russia,India ,China na South Africa) bila Nigeria utakuwepo?

Bila shaka hata masoko ya Nigeria yatavuta Mitaji ya Uwekezaji (Capital investment)kutoka ndani na nje ya nchi ukizingatia Afrika Kusini bado suala la migomo ya wafanyakazi linaathiri kwa kiwango kikubwa uwekezaji wa nje.Pia Afrika kusini inakabiliwa na nakisi kubwa ya bajeti(Budget Deficit) na Matumizi makubwa ya bajeti yaliyokosa uwiano.

Halikadhalika,Ushawishi wa Nigeria katika Diplomasia na siasa za kimataifa utaongezeka.
Napata uchungu na hasira sana nikiangalia aina ya siasa zetu ,Vyama vyetu na viongozi wetu.Ambitions 
,Ambitions ,Ambitions!


MAKALA IMEPATIKANA KWA HISANI YA MITANDAO YA KIJAMII-FACEBOOK

No comments: