Monday, April 7, 2014

MGOMO WA BODA BODA MTWARA


Baraka Mfunguo,

Kufuatia sintofahamu ya wiki iliyopita baina ya Boda boda na Polisi katik viunga vya Mtwara na kupelekea maandamano ya boda boda ambayo yalizimwa na polisi, leo boda boda wamegoma kufanya shughuli zote za kusafirisha abiria mpaka madai yao ya msingi yatakaposikilizwa ambapo kubwa ni unyanyasaji wa polisi.

 Awali boda boda hao walikuwa wafanye mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ili kutafuta suluhu, mazungumzo ambayo hayajafanyika na kuamua leo kutosafirisha abiria ama kutoa huduma yoyote. Aidha ukionekana maeneo ya Magomeni, Nkanaledi, Mwembe Ningoje umepakia abiria kinyume na utaratibu wa maazimio ya bodaboda unapigwa mawe. Hivyo mgomo ni Mji mzima wa Mtwara.

No comments: