Wednesday, March 19, 2014

JAJI WARIOBA ALIPOWASILISHA RASIMU YA PILI YA KATIBA KATIKA BUNGE MAALUM.
.

Mtizamo wangu

Suala la serikali 3 ni mtego mkubwa katika katiba yetu na mustakabali mzima wa  Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Suala la serikali 3 linatokana na unafiki wa baadhi ya watu wasioitakia mema nchi hii. Ni ama tuchague kwa mtizamo wangu tuuvunje muungano, tuingie kwenye mfumo wa majimbo ama serikali ya Muungano inayotambua dola moja yaani "states" ikiwa na serikali mbili.  

Wengi hawazungumzii federal state lakini nalo lina nafasi yake hasa katika uwakilishi, rasilimali, mgawanyo wa madaraka, huduma za kijamii, uwajibikaji na uhuru wa kutoa maamuzi kwa haki na uwazi. Suala hili nalo lahitaji mtizamo mpana sote tuelewe tusichezeshane sinema za kalikenya ama cheusi chekundu. Tuwe federalists sio serikali 3 ama unitary state asiyetaka akaanzishe serikali nyumbani kwake na mkewe.

 Ni kama namuona Nyerere. Waswahili husema asiyesikia la mkuu huvunjika guu na mtoto akililia wembe wacha umkate. Ole wenu wanasiasa mliopewa dhamana .

No comments: