Friday, February 7, 2014

HABARI ZA VIJIWENI

Blogu itaanza kukujia na habari za vijiweni. Habari za vijiweni itahusu maisha ya kila siku, skendo mbalimbali (sio za udaku) zinazohusu utendaji wa serikali na viongozi wake. Habari za vijiweni sio za kuthibitishwa vyanzo vyake ila ni habari ambazo zinakuwe zimejiri katika mkoa wa Mtwara na watu kuiongelea. Na leo tunakujia na habari kuhusu.......

KIGOGO WA OFISI YA MKUU WA MKOA MTWARA ATUHUMIWA KUKWAPUA SIMU YA KIGOGO MWENZAKE KWENYE KIKAO .

Habari zinaeleza kwamba kuna kiongozi wa ofisi ya mkuu wa mkoa (jina linahifadhiwa) anatuhumiwa kukwapua simu ya watendaji waliokuja mkoa wa Mtwara kwa ajili ya majadiliano na vikao vilivyofanyika kwa mkuu wa mkoa. Aidha mkwapuaji simu hiyo alikuwa mshiriki katika kikao hicho. Baada ya mheshimiwa kufanya kila jitihada ya kurejeshewa simu yake hiyo kushindikana, kwa sababu mkwapuaji alikwisha zima, aliamua kurudi Dar es Salaam na kuanza kufuatilia kupitia G.P.S na ndipo mwizi hiyo alipobainika. Inaelezwa mkwapuaji huyo alifuatwa nyumbani mwake na wahusika katika ulinzi mkali wakati akiwa kazini na akapata taarifa na yeye akachukua askari  wa kwake kwa ajili ya usalama walipokutana yakatolewa  maelezo na mhusika kuingia ndani na kuitoa simu hiyo. Kisha ikawa ni aibu juu ya aibu. 
Hii ndiyo habari ya vijiweni inayowika kwa  sasa Mtwara.

No comments: