Wednesday, January 29, 2014

KUMBU KUMBU- JOSEPH KILASARA MFUNGUO

 Joseph Kilasara Mfunguo 04/04/1984
-29/01/2000
Miaka 14 siku na wakati kama wa leo tokea ututoke. Umeacha mwangwi wenye machungu na simanzi katika familia ndugu jamaa na marafiki. Natambua kuwa pamoja na kulia na kulalamika huku hakuwezi kukurudisha tena huku duniani, ila ninaamini huko uliko umeshakuwa mkubwa kwetu. Upendo wako na moyo wako wa kusamehe hata pale ulipokosewa unanifanya nikiri wazi na nitamani kuufikia japo kuduchu lakini Mungu ndiye atoaye karama zote kwa yule amchaguaye. Joseph nitazidi kukukumbuka na kukuenzi mathali mimi nipo  hai duniani. UPUMZIKE KWA AMANI 

1 comment:

Subi Nukta said...

Baraka,
Poleni kwa msiba.
Apumzike pema Joseph.
Liko tumaini kwa maisha ya baadaye, Mungu akufariji kwa neno hilo.