Tuesday, April 30, 2013

DAR EAGER TO PROCESS CASHEWS FOR EXPORT 

Statistics made available by Cashewnut Board of Tanzania (CBT) indicates that the country used to produce over 20 per cent of global cashew in the 1970s peaking at 145,000 tonnes in 1974, but then in 1980s collapsed to some three per cent before regaining to 158,000 tonnes in 2012.

Most of the Tanzania raw cashew crop that accounts to about 90 per cent is exported to other countries including India as raw crop and only a small portion of less than 10 per cent, is processed internally. Concerned with the situation, the government is seeking a way that would help cut back the loss the country incurs by exporting raw cashew.

The Ministry of Agriculture, Food and Cooperatives has been in talks with a British investor to set up processing plants that would help to control that loss. The Minister for Agriculture, Food and Cooperatives Eng Christopher Chiza pointed out that Tanzania has a substantial potential to extend production and increase the amount it exports by adding the value of domestically processed cashewnut beyond the current 10 per cent while also making use of by-products.

He said that most of the largescale cashew firms are export processor, with only few that are both processors and traders. The total installed cashew nut processing capacities for the large firms in Tanzania in 2012 was about 94,000 tonnes per season.

"The average capacity utilization rate for the large-scale cashew nut processing firms has been low at about 21 per cent last year, and failure to utilize full capacity is due to insufficient funds for purchasing raw cashewnut and meet production costs, poor managements skill and product market uncertainty," Eng Chiza explained.

Adding that; "Earlier, the country had about 12 factories for processing nuts but in 1990s all were sold to private firms to rescue the market of raw nuts produced, we thus struggle hard to ensure that we process cashew nuts locally as we are about to conclude talks with the investor.

"The government saw it wise to look for investor in cashew nuts processing factories to help curb losing a lot of economic gains by exporting raw nuts in the world markets," he noted. Bank's of Tanzania's Annual Report for 2010/2011 indicates that cashewnut sector is one among the main contributors in the exports basket for Tanzania standing at third position from tobacco and coffee.

The report says further that cashewnut contribution in the export earnings would have been even higher if the crop would have been processed before exporting. The export of raw nuts bears negative structural impacts on the industry such as the export of employment opportunities and the loss of income for other cashew by-products.

CBT statistics on cashew production since independence shows that the trend of production was increasing since independence and peaked to 145,080 tonnes in 1972/73 then started to decrease gradually recording as low as 16,400 tonnes in 1986/87. It was also revealed that production started to again in mid 1980s and in 2000/2001 a total of 122,289 tonnes were recorded.

As for 2012/2013, he said, the quantity of cashewnut collected as of February 9 this year stood at 121,703 tonnes. The increase of production was due to increased acreage, government subsidy on pesticides and adoption of good agricultural practices including weeding, pruning and spraying of pesticides.

Tanzania is also known to produce premium quality cashewnut fetching higher prices in the world markets compared to cashew from other countries in Africa and such quality is attributed to favourable weather and soil conditions the country enjoy s coupled with good agricultural practices exercised in the farms.

Trade data from Food and Agriculture Organization (FAO-2012) shows that Tanzania now exports over 150,000 tonnes of nuts per year compared to 65,000 tonnes ten years ago. The data further shows that Tanzania domestic consumption of cashew nuts also soared from an estimated 20,000 tonnes in 2010 to around 25,000 tonnes in 2012.

FAO Data indicates that there is significant growth in the trade, showing the increase in Indian output and the dramatic appearance of Vietnam as a supplier of nuts kernels to rival Brazil. These three exporters supply over 90 per cent of the kernel traded globally. Domestically, consumption of cashew in the country has also shot up.

The increasing domestic consumption of cashew kernels is due to improved distribution system through street vendors, shops, minimarkets and supermarkets. CBT Director General Mr Mfaume Juma recommended for the government to consider waiving taxes for machineries and spare parts earmarked for establishing and running of processing factories in the country to reduce costs to the investors in cashew nuts processing.

Concerned and determined to ensure that cashew nuts are locally processed and subsequently added value, Mr Juma noted that the government should also consider to provide more incentives to investors who have shown interest in establishing factories in agro-processing with particular emphasis to cashewnut sub sector from which the country is losing a lot of economic gains by exporting raw nuts in the world market.

CBT Director also appealed to the government to consider remitting 100 per cent of the export levy collected by Tanzania Revenue Authority (TRA) from exporters of raw Cashewnut to the Cashewnut Industry Development Trust Fund (CIDTF) to support establishment of new processing factories in the country as a way of achieving the target of locally processing all cashewnut produced in Tanzania within the next three years.

Cashew nuts provide an important source of income for some 250,000 smallholder farmers in Tanzania. They are especially important in the southern coastal region, where the districts of Mtwara, Lindi, and Ruvuma account for 80- 90 per cent of Tanzania's marketed cashew crop.

According to the East and Southern Africa Agribusiness Network (ESAANet), network aiming at facilitating increased regional exchange of information, average smallholder cashew farmer occupies about one to two hectares of cashew trees, sometimes intercropped with food crops, mainly cassava, grain staples and legumes. Large-scale private plantations occupy about 2,000 hectares in Lindi and Mtwara regions.

Most of the cashew was planted in the 1950s and 1960s, with a marked decline in planting since mid 1970s.DAILY NEWS

GADO TOON


Wednesday, April 17, 2013

HOTUBA YA UPINZANI MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MH. PROF. KULIKOYELA KANALWANDA KAHIGI (MB) KUHUSU MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA 2012/2013 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YA RAIS – MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA KWA MWAKA WA FEDHA 2013/20141. UTANGULIZI


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la 2013, naomba kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, kuhusu mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya 2012/2013 na makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2013/2014.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, kipindi hiki itajikita katika mambo machache mahususi katika Ofisi ya Rais - katika Utawala bora, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mahusiano na Uratibu - ambayo tunayaona ni mapungufu. Lengo la kufanya hivyo ni kuitaka Serikali ama ichukue hatua ya kuyatokomeza mapungufu hayo kwa kutangaza hadharani nia yake ya kuyakomesha, kisha ichukue hatua mwafaka, au ijiuzulu kwa kushindwa kuongoza dola.


UTAWALA BORA


2.1. Idara ya Usalama wa Taifa – Ikulu


Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu sasa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA imeitaka Serikali kuwachukulia hatua maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa – Ikulu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu vya utekaji na utesaji kwa watu wanaoonekana kuikosoa Serikali, lakini mpaka sasa hakuna hatua dhahiri zinazochukuliwa ilhali matukio hayo ya utekaji na utesaji yanazidi kuongezeka katika nchi yetu.


Mheshimiwa Spika, aliyetajwa na Gazeti la Mwanahalisi kuhusika na kitendo cha kinyama cha kumteka na kumtesa Dkt. Ulimboka mwezi Juni, 2012 ni afisa wa Usalama wa Taifa, Ramadhani Ighondu Abeid. Tulitarajia Serikali, kupitia Jeshi la Polisi, ingemkamata na kumhoji mtu huyu ili kujiridhisha na tuhuma dhidi yake na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini mpaka leo hakuna chochote kilichofanyika kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu aliofanyiwa Dkt. Ulimboka, jambo ambalo linaashiria kwamba Serikali iliridhika na kilichotokea. Lakini jambo baya zaidi ni kwamba Gazeti la Mwanahalisi lililosaidia kugundua uhalifu huo lilifungiwa kwa muda usiojulikana.


Mheshimiwa Spika, mazingira ya kuteswa kwa Mhariri wa Shirika la Habari, ndugu Absalom Kibanda yanafanana sana na yale ya kutekwa na kuteswa kwa Dkt. Ulimboka. Aidha, aina ya utesaji (mfano kung’olewa kucha, meno na kutobolewa jicho) unafanana sana na aina ya mateso aliyopata Dkt. Ulimboka. Hivyo, ushahidi wa kimazingira unaonesha kwamba waliomteka na kumtesa Dkt. Ulimboka yumkini ni walewale waliomteka na kumtesa Absalom Kibanda au mawakala wao.


Mheshimiwa Spika, katika sakata la Dkt. Ulimboka, jeshi la polisi lilidai kuwa limemkamata mtu mmoja lililodai kuwa ni raia wa Kenya ambaye hatima ya kesi yake haijulikani mpaka sasa. Kwa tukio la Absalom Kibanda hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya watu walioshtakiwa kuhusu uhalifu huu dhidi ya binadamu. Dkt. Ulimboka ambaye angeweza kutoa msaada kwa Polisi kuwakamata waliohusika na uhalifu huo, hajahojiwa mpaka leo ingawa katika kiapo chake alichokiandika mbele ya mwanasheria wake alimtaja afisa wa Usalama wa Taifa - Ikulu kuwa alihusika kumteka na kumtesa. Inashangaza sana kwa nini Serikali haijataka kutumia maelezo ya Dkt. Ulimboka mwenyewe kuwakamata wahalifu. Jambo jingine la kusikitisha ni kwamba kuna dalili za wazi kwamba suala la kutekwa na kujeruhiwa vibaya kwa Absalom Kibanda limesahaulika kabisa.


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya Adhabu ya Tanzania (Penal Code), kuteka na kutesa ni makosa ya jinai. Ni aibu kwa Idara ya Usalama wa Taifa iliyokabidhiwa jukumu kubwa na la heshima kubwa la kuulinda usalama na usitawi wa nchi kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kikatili kama hivi. Kitendo cha kuhisiwa tu kwamba chombo hiki cha usalama kinajihusisha na vitendo vya kijinai moja kwa moja kinakikosesha sifa ya kufanya kazi ya usalama wa taifa. Na kwa kuwa chombo hiki kiko chini ya mamlaka ya Rais moja kwa moja tayari ni doa kubwa kwa Rais mwenyewe, Serikali yake na hata kwa chama chake.


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Ujasusi na Usalama ya Tanzania (Tanzania Intelligence and Security Services Act) ya 1996, Idara ya Usalama wa Taifa hairuhusiwi kufanya upelelezi wa ufuatiliaji - “ushushushu” kwa watu wanaoipinga Serikali kwa misingi ya kisheria na kikatiba (kwa maana ya vyama vya siasa, vyombo vya habari na wanaharakati). Ibara ya 5(2), kipengele ‘a’ na ‘b’ inasomeka hivi:


“It shall not be the function of the Service :
a) to enforce measures for security or;
b) to institute surveillance of any person or category of persons by reason only of his or their involvement in lawful protest or dissent in respect of any matter affecting the constitution , the laws or the Government of Tanzania”.

Mheshimiwa Spika, kwa tafsiri isiyo rasmi, sheria inasema hivi:
“Haitakuwa kazi ya Idara kufanya yafuatayo:
a) kutekeleza hatua za usalama, au
b) kufanya upelelezi wa ufuatiliaji wa mtu yeyote au kundi lolote la watu kwa sababu tu ya kuhusika na kupinga au kushiriki maandamano halali kuhusiana na jambo lolote la kikatiba, sheria au Serikali ya Tanzania”.

Mheshimiwa Spika, nimelazimika kunukuu sheria hii kwa kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA, inao ushahidi kwamba maafisa wa Usalama wa Taifa wamekuwa wakifanya upelelezi wa ufuatiliaji (surveillance) kwa watu wanaoipinga Serikali kwa misingi ya Katiba na sharia - jambo ambalo ni kinyume na sheria iliyopo.

Mheshimiwa Spika, ushahidi wenyewe ni kwamba baada ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA kutuhumiwa kwamba anahusika na ugaidi na video yake kurushwa kwenye mitandao ya kijamii, Muhidin Issa Michuzi, ambaye ni mpiga picha wa Rais, Ikulu, aliandika barua-pepe kwa Salvator Rweyemamu, Prosper Mbena, Hamis Mwinyimvua, Liberatus Mulamula, Msafiri Marwa, Laurent Ndumbaro na wengine ambao ni watumishi wenzake wa Ofisi Binafsi ya Rais akiwapongeza kwa kazi nzuri na ya ziada waliyoifanya ya kutengeneza video ya Lwakatare, na kuwaeleza kuwa hiyo ni kete kubwa kwao hivyo lazima waipigie kelele sana.

Mheshimiwa Spika, kuna ushahidi mwingine kwamba baadhi ya maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wanawahonga kwa kuwalipa fedha watumishi wa CHADEMA ili watoe ushahidi wa uongo dhidi ya kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa CHADEMA. Miongoni mwa maafisa hao ni Sinbard Mwagha. Huyu ni ni afisa usalama wa taifa anayefanya kazi makao makuu ya idara hiyo. Taarifa zilizopo ni kwamba ndiye anayetumika kuendesha michezo ya kuhonga wanasiasa wa CCM na upinzani, na kwamba ndiye anayehusika pia kuwapanga wabunge wa CCM waongee nini bungeni wakati wa vikao vya bunge kwa maslahi ya CCM.


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya Adhabu (Penal Code), kutengeneza ushahidi wa uongo (fabrication of evidence) ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha miaka saba gerezani. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani inalitaka Jeshi la Polisi kumkamata haraka sana Sinbad Mwagha ambaye tuna imani anafahamika na kumfungulia mashtaka ya kuhusika katika kutengeneza ushahidi wa uongo dhidi ya kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Ndugu Wilfred Lwakatare. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa maelezo ya kina juu ya hatua ilizochukua hadi sasa dhidi ya maafisa wa usalama wengine ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu.

2.2. TAASISI YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA NA MWELEKEO WA MATUKIO YA RUSHWA NCHINI


2.2.1 Rushwa inavyodidimiza uchumi na Maendeleo ya Taifa
Mheshimiwa Spika, rushwa na ufisadi bado ni tatizo kubwa katika nchi yetu na kikwazo kikubwa katika kuleta maendeleo ya nchi yetu. Bado hatujafanikiwa kupunguza tatizo hili kubwa linalodidimiza uchumi wa nchi yetu na linalochangia katika kujenga matabaka ya matajiri haramu na masikini waliosababishiwa umasikini na mfumo wa kifisadi.


Mheshimiwa Spika, kwa sababu Serikali ina kigugumizi kuhusu rushwa na ufisadi, baadhi ya taarifa zihusuzo mambo hayo hufichwa. Kwa mfano, Serikali imekaa kimya kuhusu baadhi ya mikataba na ripoti mbalimbali – jambo linalotafsiriwa kwamba ni mchakato wa kuwalinda watu waliohusika na vitendo vya rushwa au ubadhirifu.


Mheshimiwa Spika, ripoti kwa mfano za EPA, MEREMETA, Uchunguzi na ukaguzi wa kituo cha mabasi Ubungo, ripoti ya ufisadi katika UDA, ripoti ya sakata la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo - ni baadhi tu ya ripoti ambazo bado ni siri.


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti ya “The NATIONAL GOVERNANCE AND CORRUPTION SURVEY ya mwaka 2009, Ubinafsi na tamaa hasa ya viongozi wa Serikali inaongoza kwa asilimia 95.5 kama kisababishi cha rushwa hapa nchini.


Mheshimiwa Spika, kuna aina ya rushwa anayonufaika nayo afisa wa Serikali kwa kupewa mgawo wa kifisadi baada ya kutoa kandarasi kinyume na utaratibu au upendeleo kwa kampuni fulani. Hivyo, fedha hizo za mgawo zinaelekezwa kwa taasisi ambayo ana uhusiano nayo au kujengewa nyumba ilimradi fedha hizo za kifisadi zisipitie kwenye akaunti yake binafsi.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni kumetokea maafa ya kuanguka kwa majengo ya ghorofa na kuangamiza maisha ya watu hapa nchini. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba maafa haya yalitokea kwa sababu ya mfumo wa kifisadi na rushwa katika utendaji wa Serikali. Hii ni kwa sababu Serikali ilishashauriwa na na tume ya uchunguzi iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuwa maghorofa zaidi ya 100 Dar es Salaam yamejengwa chini ya kiwango, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, pamoja na Tume hiyo kutumia mamilioni ya fedha za walipakodi kufanya uchunguzi na kuandika taarifa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashawishika kuamini kwamba ukimya wa TAKUKURU kwenye maafa haya ya maghorofa kuporomoka ni kutokana na taasisi hiyo kuwa sehemu ya mfumo wa kifisadi unaoitafuna nchi hii. Ukiukwaji wa makusudi wa kikomo cha maghorofa (maghorofa 10) ulikuwa ni ishara tosha kuwa mradi huu uligubikwa na ufisadi – na TAKUKURU ilipaswa kufanya kazi yake ili kubaini kwa nini maghorofa yalizidishwa, na pia kwa nini hadi wakati huo taarifa za Tume ilikuwa haijatekelezwa.


Mheshimiwa Spika, sababu moja muhimu iliyotajwa katika Taarifa ya Tume hiyo ni kukosekana kwa usimamizi na uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa serikali (86%), uwezo mdogo wa kusimamia sheria na kuhakikisha zinatekelezwa na upungufu katika utoaji wa adhabu kali kwa wanaojihusisha na vitendo vya rushwa (85.6%).


Mheshimiwa Spika, ili tuweze kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa, kwanza kabisa ni lazima tujenge taasisi imara na huru na zenye kufanya kazi zake kwa weledi na umakini mkubwa. Lazima taasisi hizi si tu ziwe huru; bali pia zionekane kuwa huru. Muundo wa TAKUKURU ni vyema ukaangaliwa upya katika mchakato unaoendelea hivi sasa juu ya kuandika Katiba mpya.


Mheshimiwa Spika, Mkurugenzi wa TAKUKURU ambaye ni mteule wa Rais, ni vigumu sana kuwa huru na kuvichunguza vyombo vingine ambavyo vipo chini ya mamlaka ya Rais. Kwa maneno mengine, ni vigumu kumchunguza aliyekuteua na kuchukua hatua kali dhidi yake. Katika mfumo uliopo, Rais huyo huyo ndiye Mwenyekiti wa chama tawala; hivyo inakuwa ni vigumu sana kwa chombo hiki kuchukua hatua kali hata dhidi ya chama; kwani kufanya hivyo kutakuwa pia ‘kumuadhiri’ mkuu wake wa kazi aliyemteua ambaye kwa kofia yake nyingine ni Mwenyekiti wa chama. Lakini ni mara ngapi katika chaguzi za Chama cha Mapinduzi tumesikia Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM akilalamikia chaguzi hizo kuwa ziligubikwa na rushwa, lakini hatujawahi kusikia kuwa wahusika wa matukio hayo wamekamatwa na TAKUKURU japokuwa ushahidi unakuwepo.


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Umasikini ya mwaka 2011 iliyotolewa Mei 2012, umma haujaridhika na juhudi zinazofanywa na Serikali katika utendaji mzima wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa kutokana na sababu kuu kuwa watu wengi waliokuwa wanahusika na rushwa kubwa wameachiwa huru.


2.2.2. Maazimio ya Kongamano la Wadau wa Rushwa

Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 03.05.2010 kulikuwa na Mkutano wa kutathmini maazimio ya Kongamano la Rushwa la mwaka 2009 ambalo lilihusisha wadau mbalimbali wa kupambana na rushwa nchini wakiwemo kutoka Ofisi ya Bunge na mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Mheshimiwa Samwel Sitta ambaye alikuwa Spika wa wakati huo. Katika kongamano hilo, maazimio zaidi ya 30 ya jinsi ya kukabiliana na kupambana na rushwa katika taifa letu yalipitishwa.


Mheshimiwa Spika, miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na azimio namba (4) ambalo lilikuwa ni kuitaka TAKUKURU kuanzisha gazeti maalum litakalosambazwa mpaka vijijini lenye kuelimisha umma kuhusiana na masuala ya rushwa.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikali kulieleza Bunge juu ya hatua iliyofikiwa katika mchakato wa kuanzishwa kwa gazeti hilo. Aidha, azimio namba 11 lilihusu viongozi kutangaza mali zao pindi wanapokuwa wanaondoka madarakani; utekelezaji wake umefikia hatua gani?


Mheshimiwa Spika, katika azimio namba 15 la Kongamano la Rushwa, TAKUKURU ilitakiwa kuhakikisha kuwa inawekeza zaidi katika fani ya habari za kiuchunguzi (investigative journalism) kwa ajili ya kuwajengea uwezo zaidi wanahabari katika kufichua na kuandika taarifa za rushwa hapa nchini. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua utekelezaji wa azimio hili umefikia wapi na hasa ikizingatiwa kuwa gazeti la Mwanahalisi lililokuwa linaandika habari za kiuchunguzi kuhusiana na rushwa sasa limefungiwa kwa muda usiojulikana.

Mheshimiwa Spika, azimio la 27 la kongamano hilo liliitaka serikali iache mara moja utaratibu wa kuwahamisha watumishi wa umma ambao ama ni wabadhirifu/walarushwa kama sehemu ya adhabu kutokana na kitendo cha wizi na/au ubadhirifu wa mali ya umma kwenye ofisi za umma na badala yake washughulikiwe kwa mujibu wa sheria za rushwa na za jinai zilizopo katika mfumo wetu wa sheria hapa nchini. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kupata majibu ni hatua gani serikali imefikia katika kutekeleza azimio hili kama kweli tuna nia ya dhati ya kupambana na wabadhirifu wa fedha za umma na walarushwa kwenye Ofisi za umma.


3. MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA


3.1. Utaratibu wa Ajira kwa Mkataba kwa Watumishi waliostaafu


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sheria za Tanzania, watumishi wa umma hutakiwa kustaafu kwa hiari wakiwa na umri wa miaka 55, na watimizapo miaka 60 hutakiwa kustaafu kwa lazima. Hata hivyo, baadhi yao wamekuwa wakipewa mikataba ya kuendelea na kazi hata baada ya kutimiza umri wa kustaafu kwa lazima.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haipingi kumwajiri mstaafu kwa mkataba kama mstaafu huyo ndiye pekee mwenye ujuzi na uzoefu wa kazi anayotakiwa kufanya. Ila kuna baadhi ya watumishi waliotimiza umri wa kustaafu kwa lazima, wakapewa mikataba ya kuendelea na utumishi Serikalini, bila kuwa na sifa iliyotajwa. Kambi Rasmi ya Upinzani ilitegemea kwamba, Serikali ingeajiri watumishi wengine kushika nafasi hizo baada ya mikataba hiyo kumaliza muda wake hasa ukizingatia tatizo kubwa la ajira linalowakumba vijana katika nchi yetu. Serikali ya CCM imeendelea kuwaacha wastaafu hao kuendelea na utumishi bila hata kutoa mikataba mipya baada ya ile ya mwanzo kumalizika.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaomba iwataje baadhi ya wazee waliotimiza umri wa kustaafu kwa lazima, wakapewa mikataba ya utumishi Serikalini, mikataba hiyo ikamaliza muda wake, lakini bado wanaendelea na kazi:


1. Ndugu John Tendwa – Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania


Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Ajira wa Msajili wa vyama vya Siasa John Tendwa ulimaliza muda wake tangu Novemba, 2012 lakini bado anaendelea na kazi bila ya mkataba mwingine. Aidha, alipohojiwa na waandishi wa habari juu ya jambo hili alikiri kuwa ni kweli mkataba umeisha lakini sababu za yeye kung’ang’ania ofisi alisema iulizwe mamlaka ya uteuzi wake, yaani Rais. Hata hivyo, Ndugu Tendwa aliwakataza waandishi wa habari kutoa taarifa hii katika vyombo vya habari kwa alichodai kuwa ingeleta mgogoro na malumbano makubwa yasiyo na tija.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haiamini hata kidogo kwamba John Tendwa ndiye mtu pekee mwenye sifa za pekee za kuwa Msajili wa vyama vya Siasa miongoni mwa Watanzania. Hatupendi kusema kuwa ufanisi wake umepungua wala hatupendi pia kusema kwamba kuendelea kwake kubaki ofisini bila hata ya mkataba ni kutokana na kujipendekeza kwake kwa Rais na uhodari wake wa kukipendelea chama tawala na Serikali yake lakini tunapenda kusema kuwa wapo watu wengine wenye sifa ya kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa. Ni jambo jema kuwapa wengine uzoefu, na ni jambo jema pia kuzingatia sheria na kanuni zinazoelekeza masuala ya utumishi wa umma.


2. Mkurugenzi – Manispaa ya Moshi – Bernadeta Kinabo


Mheshimiwa Spika, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Moshi, Bernadeta Kinabo, naye alishastaafu kazi, akapewa mkataba kuendelea na kazi na mkataba huo uliisha muda wake tangu mwaka 2011, lakini bado yupo ofisini anaendelea na kazi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe majibu, ni kwa nini Halmashauri na Manispaa ziendeshwe na watumishi wa mkataba wakati kuna watumishi waandamizi katika Halmashauri na Manispaa hizo ambao wangeweza kufanya kazi hizo?


3.2. Nafasi na Haki za Walimu katika Sekta ya Utumishi wa Umma


Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu sasa walimu wamekuwa ni kada ya utumishi wa umma ambayo haitendewi haki na Serikali. Nasema hivi kwa sababu kwa miaka mingi walimu wamekuwa wakilalamika kuhusu mishahara duni, lakini pia baadhi yao (wengi kiasi) wamekuwa hawalipwi stahili zao kwa mfano malimbikizo ya mishahara, fedha za uhamisho, n.k. Mara zote walimu kupitia chama chao wanapolalamika kupata maslahi yao Serikali imekuwa ikiwajibu kwa jeuri kuwa madai yao hayalipiki na pia wanapotangaza mgomo halali kama njia ya kuifanya Serikali iwasikilize, Serikali imekuwa na tabia ya kukimbilia mahakamani kuweka zuio la mgomo huo na hivyo kuwaacha walimu njia-panda bila kujua la kufanya.


Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya bajeti ya Elimu mwaka 2012/2013, Kambi Rasmi ya Upinzani ilitoa angalizo kwamba Serikali isiwaburuze walimu wasije wakabaki na kinyongo na kufanya mgomo baridi ambao matokeo yake huwa ni mabaya kuliko mgomo halisi. Serikali hii ya CCM, kama kawaida yake, iliendelea kuziba masikio, na matokeo yake tunaona jinsi ambayo elimu ya nchi hii inavyozidi kuporomoka. Kwa mara ya Kwanza katika historia ya Tanzania, wanafunzi zaidi ya asiliami 60 waliofanya mtihani wa kidato cha nne kidato cha nne 2012 walipata daraja sifuri. Bila shaka mojawapo ya sababu kubwa za anguko hili ni Serikali kupuuza madai ya walimu kama Kambi Rasmi ya Upinzani ilivyodokeza mwaka jana.


Mheshimiwa Spika, hukumu ya mahakama juu ya mgomo wa walimu mwaka jana 2012, ni kwamba Serikali ilitakiwa kukaa na chama cha walimu (CWT) na awepo msuluhishi katika yao (third party) katika kutafuta ufumbuzi wa madai ya walimu dhidi ya Serikali. Kwa kuwa mpaka leo hapajakuwepo na kikao cha usuluhishi kati ya Serikali na Chama cha Walimu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaliomba Bunge sasa kama chombo cha uwakilishi lakini pia kama muhimili wa dola unaojitegemea kuwa msuluhihishi kati ya Serikali na Chama cha Walimu ili haki itendeke kwa pande zote mbili.


3.3. Utaratibu wa Kupima Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma


Mheshimiwa Spika, mwaka 2004 Serikali ilitoa waraka wa utumishi namba 2 wa mwaka 2004 kuhusu utekelezaji wa utaratibu na kupima utendaji kazi wa watumishi kwa uwazi. Lengo na madhumuni ya waraka huu ni kupima na kuongeza ufanisi kwa watumishi wa umma ili kuleta tija, na hivyo kustawisha maendeleo ya nchi yetu. Zaidi ya hayo, waraka huu unaondoa utaratibu wa zamani wa kupima utendaji kwa watumishi.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali iliambie Bunge hili na wananchi wa Tanzania kwamba ni mafanikio kiasi gani yamepatikana tangu kuanza kwa utekelezaji wa waraka huu.4. MAHUSIANO NA URATIBU


4.1. Mchakato wa Katiba Mpya na Mapungufu yake
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Hotuba ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni, aliyoitoa kwenye mkutano huu wa bunge tarehe 11 Aprili, 2013 ni kwamba kulikuwa na makubaliano kati ya kamati maalum ya CHADEMA na Rais juu ya marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2011. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, marekebisho yalitakiwa kufanywa kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza ilifanyika katika Bunge la Februari, 2012. Aidha, kwa mujibu wa makubaliano hayo, awamu nyingine mbili za marekebisho ya sheria hiyo ya mabadiliko ya Katiba yalitarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka jana, yaani 2012. Mwaka 2012 ulimalizika kabla ya makubaliano hayo kutimizwa.


Mheshimiwa Spika, katika hotuba yake ya kuukaribisha mwaka 2013, Rais Kikwete, alipokuwa akilihutubia taifa kama ulivyo utaratibu wake wa kila mwisho wa mwezi alisema hivi, nanukuu:


“Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwezi wa Februari, 2012, nilieleza kwamba katika mazungumzo baina ya Serikali na vyama vya siasa na wadau wengine juu ya marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tulikubaliana tushughulikie marekebisho ya Sheria hiyo hatua kwa hatua. Tulikubaliana kuanza na mambo yanayohusu Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi ili Tume iundwe na ianze kazi. Baada ya hapo tuangalie vipengele vinavyohusu Bunge Maalum na Kura ya Maoni.

Tulifanya hivyo kuhusu Tume ya Katiba na sasa tunajiandaa kuanza mazungumzo kuhusu ngwe iliyobaki yaani, Bunge Maalum na Kura ya Maoni. Kama mazungumzo yatakamilika mapema kunako Januari, 2013 mapendekezo hayo yatafikishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano katika kikao cha Februari kwa uamuzi. Vinginevyo itakuwa katika Bunge la Aprili, 2013.

Ndugu Wananchi;
Kuhusu Kura ya Maoni, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaelekeza kuwa Kura ya Maoni itatungiwa Sheria yake maalum. Ni matumaini yangu kuwa matayarisho yake yataanza mapema iwezekanavyo. Nawasihi wananchi wenzangu, viongozi wa vyama vya siasa na asasi za kijamii tuwe watulivu, tuendelee kushirikiana katika mchakato huu wa Katiba mpaka tulifikishe jahazi ufukweni salama kwa mustakabali mwema wa nchi yetu na watu wake”.


Mheshimiwa Spika, ahadi ya Rais kwamba Serikali ingeleta awamu zote mbili za marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya mwisho wa mwaka 2012 haikutimizwa. Aidha ahadi nyingine aliyotoa Rais wakati akitoa hotuba ya kuukaribisha mwaka 2013 kwamba marekebisho hayo yangefanyika katika mwezi Februari 2013 au Aprili 2013 bado haijatekelezwa na hatuoni dalili ya kufanya hivyo.


Mheshimiwa Spika, nataka kuweka kumbukumbu vizuri kwamba, madai ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba siyo ya kuokoteza. Ni makubaliano halali kati ya wadau mbalimbali kama vile vyama vya siasa, asasi/mashirika n.k. na Rais. Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka Rais asimamie ahadi zake, na taifa lina haki ya kujua nini kilitokea mpaka ahadi hizi kushindwa kutekelezwa.


Mheshimiwa Spika, jana tarehe 16.04.2013, Waziri Mkuu, wakati akihitimisha hotuba yake alitoa ahadi kuwa “huenda serikali ikawasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria hiyo kwenye Bunge hili la Aprili kama muda ukipatikana kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza”. Kwa maelezo hayo, ni wazi kuwa Waziri Mkuu hana hakika na kutekelezeka kwa ahadi ya Rais katika Mkutano wa Bunge wa Kumi.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani, kwa kutambua kwamba mambo haya yako chini ya Ofisi ya Rais, tunaitaka serikali itamke mbele ya bunge hili ni lini marekebisho hayo yatafanyika. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inayoongozwa na CHADEMA inarudia tena, kwamba: haitakuwa tayari kuendelea na mchakato wa katiba mpya endapo marekebisho ya sheria hiyo hayatafanyika pamoja na utekelezaji wa mambo ambayo tuliyasema wakati wa hotuba ya Waziri Mkuu.


4.2. Tume ya Mipango na Majukumu yake
Mheshimiwa Spika, jukumu kubwa la Tume ya Mipango, pamoja na mambo mengine, ni kuratibu utekelezwaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haina mgogoro na utendaji kazi wa tume hii, ila inashangazwa na uundaji wa chombo kingine chini ya Ofisi ya Rais ambacho kimsingi kazi zake zingepaswa kufanywa na Tume ya Mipango.

Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu, katika hotuba yake ya bajeti alisema kwamba: “Serikali imeona ni muhimu kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa kuanzisha mfumo imara zaidi wa kupanga vipaumbele, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo. Mfumo huo ambao utasimamiwa na Chombo maalum (President’s Delivery Bureau) chini ya ofisi ya Rais, Ikulu, unazingatia uzoefu wa nchi ya Malaysia”.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inatambua kwamba Serikali imeuchukua mpango huu kutoka Malaysia, kutokana na mkutano wa kimataifa wa 'Langkwi' uliofanyika mwezi Juni 2011 ambao Rais Jakaya Kikwete alishiriki kwenye “mkutano wa tafakuri” 'Putrajaya' ambapo Waziri Mkuu wa Malaysia Mhe. Dato' Razak aliuelezea mpango huu kuwa ulileta mabadiliko ya kiuchumi katika nchi yake. Katika mkutano huo wa tafakuri, Waziri Mkuu wa Malysia alisema kwamba mafanikio ya mpango huo ulitokana na misingi ifuatayo:


i. Uongozi shupavu na ulio tayari kwa mabadiliko ya kuipeleka nchi mbele.


ii. Kuweka mipango ya kimaendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa


iii. Nidhamu katika utendaji na utekelezaji


iv. Uwajibikaji wa serikali na kuwa tayari kukiri madhaifu yake.


Mheshimiwa Spika, mpango huu wa kuanzishwa kwa idara hii ambayo inajitegemea kwenye Ofisi ya Rais tayari umeshaanzishwa kama alivyokiri Waziri Mkuu katika hotuba yake na kwamba Rais tayari ameshazindua awamu ya kwanza ya maabara tangu tarehe 22.02.2013, na vipaumbele ambavyo vimepitishwa ni sita kama ifuatavyo: Nishati, Uchukuzi, Kilimo, Elimu, Maji na Ukusanyaji wa Mapato.


Aidha, kwa mwaka huu wa fedha mpango huo umeweka bayana kuwa kwa upande wa Nishati lengo ni kuongeza uzalishaji wa nishati kutoka Megawati 1,438 hadi kufikia Megawati 2,780. Katika usafirishaji kipaumbele ni kufungua korido ya kati kwa kufikia uwezo wa kusafirisha tani milioni 5 ifikapo 2015 na hatimaye tani milioni 8 ifikapo mwaka 2025. Kwa upande wa elimu kipaumbele ni kuboresha elimu ya msingi na sekondari na kuhakikisha kuwa kiwango cha ufaulu kinafikia asilimia 70. Kwenye kilimo mkakati kipaumbele ni kufungua mashamba ya kibiashara wakati upande wa maji ni kuhakikisha kuwa asilimia 67 ya Watanzania wanapata maji safi na salama. Kwa upande wa ukusanyaji wa mapato, lengo ni kuhakikisha kuwa tunaongeza mapato kwa kiwango cha asilimia 50.


Mheshimiwa Spika, Serikali tayari imeshatenga fedha kwenye bajeti ya mwaka huu wa 2013/2014 kiasi cha shilingi bilioni 8 na imeomba fedha kutoka kwa wafadhili wa nje kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kitengo hiki kipya chini ya Ofisi ya Rais Ikulu. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikali kutoa majibu kwa Watanzania juu ya mambo yafuatayo:


i. Je, vipaumbele vya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano uliopitishwa na Bunge hili mwaka 2011 ndio vimeachwa au vitatekelezwa sambamba na vipaumbele hivi vipya?


ii. Je, Kwa nini Serikali imeanzisha kitengo kipya cha Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) (Kitengo cha Usimamizi na Ufanisi wa Utendaji) chini ya Ofisi ya Rais wakati kuna Tume ya Mipango ambayo kimsingi ndiyo yenye wajibu wa kusimamia vipaumbele vya Taifa na Mpango mzima wa Maendeleo wa Taifa?


iii. Je, ikitokea tena, Rais akakaribishwa kwenye “mkutano mwingine wa tafakuri” kama uliofanywa na kiongozi wa Malaysia, na kukuta mipango mizuri zaidi, Serikali italazimika tena kupanga upya vipaumbele vya Taifa na Mpango wa utekelezaji kama inavyofanya sasa?


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA, ni mdau mkubwa wa maendeleo na inauheshimu mpango wa Taifa wa Maendeleo lakini namna Serikali inavyotekeleza Mpango huo hatuna hakika kama malengo ya Mpango huu yatafikiwa. Kambi Rasmi ya Upinzani haioni sababu yoyote ya msingi ya kuanzisha kitengo kipya cha usimamizi wa mpango wa maendeleo wakati Tume ya Mipango ipo. Kinachoonekana dhahiri ni kwamba Serikali hii ya CCM kila kukicha inatafuta mbinu mbalimbali za kutumia fedha za walipa kodi wa Tanzania bila kujali sana matatizo ya Watanzania. Nasema hivi kwa sababu kitengo hiki kipya kilichoanzishwa bila sababu ya msingi, hivi punde kitaanza nacho kuomba mabilioni ya fedha kwa ajili ya uendeshaji wake wakati tayari kuna Tume ya Mipango ambayo ndio mratibu na msimamizi wa Mpango wa Maendeleo.


4.3. MAHUSIANO YA MADHEHEBU YA DINI NA SERIKALI


Mheshimiwa Spika, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni alieleza vizuri tatizo la udini katika hotuba yake aliyoitoa hapa Bungeni tarehe 11 Aprili, 2013. Hapa itatosha tu kusema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo matukio ambayo yanaashiria udini. Baadhi ya matukio hayo ni:


· Kushambuliwa kwa viongozi wa dini, na wengine kuuawa


· Kuchomwa moto nyumba za ibada


· Mgogoro wa nani achinje


Yapo matukio mengine; na haya yote yamesababisha taharuki, vilio, na utovu wa amani na usalama miongoni mwa wananchi walioguswa na matukio haya.


Mheshimiwa Spika, wakati watu wakizidi kuathirika na matukio yanayoashiria udini, serikali haijachukua hatua kali kukomesha matukio hayo.


Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali kushindwa kukemea au kusuluhisha kwa haraka migogoro wa kiimani uliotokea hapa nchini, umesababisha kutolewa kwa matamko makali na madhehebu ya dini ambayo kimsingi yanaonesha jinsi mahusiano kati ya Serikali na taasisi za dini yanavyozidi kudorora.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kuwa kati ya migogoro yote ya kijamii hakuna mgogoro mkubwa na tete kama ule wa kiimani, kwani mgogoro huo hauna itikadi za kisiasa na kwa maana hiyo athari zitakazotokana na mgogoro wa kidini unaathiri jamii nzima. Ni jukumu la Serikali kuwaeleza Watanzania ni hatua gani za maksudi zinachukuliwa katika kutatua mgogoro huo unaoelekea kusambaratisha amani na mshikamano wa Taifa letu?


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaishauri Serikali yetu na vyombo vyake vya usalama, sheria na amani kuchukua hatua mara moja bila kuchelewa dhidi ya watu au vikundi vyovyote vinapoanza uchochezi wa kidini. Tabia ya kuachia uchochezi wa kidini kuendelea pasipo hatua madhubuti kuchukuliwa ni udhaifu mkubwa wa uongozi na uwajibikaji wa Serikali ambayo jukumu lake la kwanza ni kulinda usalama wa nchi na watu wake.

5. MASUALA MENGINE


5.1. Utawala Bora Ngazi za Halimashauri, Kata na Vijiji


Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu sasa dhana ya utawala bora imekuwa ikionekana kuwa inapaswa kutekelezwa kwenye ngazi ya serikali kuu. Katika ngazi ya serikali za mitaa utawala bora kwa jumla umeachwa bila kuwekewa msisistizo. Ni muhimu serikali ihakikishe kuwa utawala bora unakuwa ni sehemu ya utendaji wa kila siku kwenye ngazi zote – kitongoji, kijiji, kata, wilaya na mkoa. Ni muhimu Serikali ihakikishe kuwa waliopewa wajibu wa kusimamia hilo wanatimiza wajibu wao kikamilifu.


Mheshimiwa Spika, hali ya utawala bora imezorota sana kwenye ngazi ya serikali za mitaa, na hasa ikizingatiwa kuwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini wamekuwa na utamaduni wa kuingilia maamuzi mbalimbali yanayofanywa na vikao halali vya Halimashauri za Manispaa na Wilaya. Sasa hivi Wakuu wa Wilaya na Mikoa wamekuwa wakiingilia na hata kushurutisha maamuzi mbalimbali na hivyo kukwamisha utekelezaji wa maamuzi yanayofanywa na vikao hivyo na kuathiri utendaji kazi wa Halimashauri hizo.


Mheshimiwa Spika, tabia ya kutokuheshimu utawala bora kwenye ngazi ya Halimashauri umekua na kusambaa mpaka kwenye ngazi za Kata na Vijiji kwani sasa watendaji wa vijiji na Kata wamejigeuza na kuwa wao ni Polisi, Mahakama na Magereza. Viongozi hawa wamekuwa wakiwanyanyasa sana wananchi kwa kuwakamata, kuwahukumu na hata kuanzisha magereza kama ambavyo wengi wanavyoweza kushuhudia kuwa yapo baadhi ya maghala ya mazao ambayo sasa yamekuwa ndio mahabusu kwa wananchi wa vijijini.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa majibu ya kina kuhusiana na suala la utawala bora kwenye ngazi za Halimashauri, kata na vijiji. Ni hatua gani Serikali imewachukulia viongozi wa Halmashauri, Kata na Vijiji wanaowanyanyasa wananchi kutokana na itikadi zao za siasa na sababu nyingine? Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani inauliza: Wananchi wachukue hatua gani ili kuukomesha uonevu wa aina hiyo pindi unapotokea ?
5.2. Ukosefu wa Ajira na Ongezeko la Umasikini kwa Wananchi


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa jarida la “The African Executive” toleo Na. 415 la tarehe 3-10 Aprili, 2013, ni kwamba: tatizo kubwa kabisa la binadamu kwa siku hizi ni umasikini. Ili kuondokana na umasikini huo, hitaji la msingi kabisa ni kupata kipato kizuri ambacho chanzo chake kikubwa ni ajira. Kwa hiyo njia madhubuti ya kupambana na kutokomeza umasikini ni kutengeneza nafasi nyingi za ajira iwezekanavyo na kuwapatia watu ujuzi na utaalamu ili kujaza nafasi hizo.


Mheshimiwa Spika, jarida hilo linaelezea pia kwamba, kutengeneza nafasi za ajira bila kuwajengea wananchi ujuzi na utaalamu wa kufanya kazi hizo ni kazi bure kwa kuwa kazi hizo zitafanywa na wataalam kutoka nje na hivyo kutowanufaisha wananchi wetu. Kwa hiyo kama Serikali inawapa watu wake elimu bora na kuwajengea watu wake ujuzi na utaalamu na kama Serikali inaweka mazingira mazuri ambayo watu wanaweza kufanya biashara na kupata fedha, basi watu hao watajinufaisha wenyewe, watawanufaisha wengine na wanaweza kuisaidia Serikali kuondokana na umasikini. Hivyo uwezo wa watu kupata ajira na kipato unategemea sana jitihada za Serikali.


Mheshimiwa Spika, tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini linazidi kuwa kubwa na Serikali ya CCM imeshindwa kabisa kutatua tatizo hili. Tangu mwaka 2005 Rais kikwete aliwaahidi Watanzania Maisha Bora kupitia kaulimbiu yake ya “Maisha Bora kwa Kila Mtanzania”. Hiki ni kipindi cha pili cha utawala wake na maisha ya Mtanzania yanazidi kusinyaa, umasikini unazidi kuongezeka, na tatizo la ajira linazidi kuongezeka.


Mheshimiwa Spika, pamoja Serikali hii ya CCM kushindwa kutoa ajira za kutosha tofauti na ilivyoahidi bado imekuwa ikiwakejeli wananchi kuwa eti hata kufungua visoda ni kazi.


5.3 Kufukuzwa Kazi kwa Kuonewa


Mheshimiwa Spika, baadhi ya waajiri wa serikali wamekuwa wakinyanyasa na kuwanyanyapaa watumishi wa umma kutokana na itikadi za kisiasa. Unyanyapaa huu umechukua sura mpya kiasi ambacho mtumishi anapotoa mawazo mazuri ambayo ni ya kukosoa mfumo wa uendeshaji wa taasisi ya umma ili ufanye kazi vizuri zaidi anaitwa kuwa ni pandikizi la CHADEMA. Jambo hili linawavunja moyo watumishi wa umma kufanya kazi kwa ufanisi kwa kuogopa kuitwa ni wapinzani na matokeo yake utendaji katika sekta ya umma unazidi kudorora.


Mheshimiwa Spika, katika hali ya kusikitisha, Ndugu Emmanuel V. Gwalanje, ambaye ni Afisa Mifugo Msaidizi daraja la II katika Halmashauri ya Mufindi, alifukuzwa kazi kwa mashtaka dhidi yake kwamba anajihusisha na masuala ya siasa wakati wa kazi. Katika utetezi wake, Emmanuel V. Gwalanje alieleza bayana kuwa hajawahi kujihusisha na mambo ya siasa akiwa kazini na wafanyakazi wenzake ni mashahidi; pia rekodi yake ya mahudhurio kazini ni nzuri lakini amesingiziwa hivyo kwa kuwa alihudhuria mkutano wa siasa baada ya saa za kazi.


Mheshimiwa Spika, mchakato wa kumfukuza Ndugu Emmanuel V. Gwalanje ulikuwa mfupi sana. Notisi ya Mashitaka iliandikwa tarehe 18.03.2013, utetezi uliwasilishwa tarehe 21.03.2013, barua ya kufukuzwa kazi tarehe ilitoka tarehe 28.03.2013. Kambi Rasmi ya Upinzani inashawishika kuamini kwamba uamuzi wa kumfukuza kazi Emanuel Gwalanje haukuwa wa haki ikizingatiwa kwamba hakuwahi kupewa onyo hata moja kama kweli alikuwa akijihusisha na kazi ya siasa wakati wa kazi. Aidha, muda mfupi wa mchakato wa kufukuzwa kwake unatia shaka kama kuna uchunguzi wa kina uliofanyika kubaini bila shaka yoyote kuwa Emmanuel Gwalanje kweli alihusika na kazi ya siasa wakati wa saa za kazi.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inamtaka Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mufindi, E. Kaduma, pamoja na Afisa wake wa Mamlaka ya Nidhamu kuwasilisha mchakato na hukumu ya mashitaka dhidi ya Emmanuel Gwalanje kwa Waziri wa Utumishi wa Umma ili kubaini uhalali wa mchakato mzima.


Mheshimiwa Spika, nimetolea mfano shauri la Emmanuel Gwalanje wa halmashauri ya Mufindi, lakini yapo matukio mengi ya watumishi wanaofukuzwa kazi kiholela katika halmashauri na taasisi za Serikali kutokana na chuki binafsi na unyanyapaa wa kisiasa. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kukemea tabia hii.

5.4 Huduma kwa Watumishi wa Umma wanaoishi na VVU


Mheshimiwa Spika, mwaka 2006 Serikali ilitoa Waraka wa utumishi wa umma namba 2 wa mwaka 2006 kuhusu huduma za watumishi wa umma wanaoishi na virusi vya ukimwi. Chini ya waraka huu waajiri wa watumishi wa umma wanapaswa kuhamasisha watumishi kupima VVU, na kutoa huduma muhimu kwa wale watakaokuwa wameathirika. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe taarifa katika bunge hili kuwa ni kwa kiwango gani waraka huu umetekelezwa na ni gharama kiasi gani imetumika mpaka sasa katika kuwahudumia watumishi wa umma wanaoishi na VVU kwa maana ya lishe broa, madawa, nauli za kuhudhuria matibabu na stahili nyingine?

______________________________ __________________


PROF. KULIKOYELA KANALWANDA KAHIGI (MB)


MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI


OFISI YA RAIS -


MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA


MAHUSIANO NA URATIBU


17 APRILI, 2013


SHUKRAN: JAMII FORUMS

Thursday, April 4, 2013

TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIAJUKWAA LA WA WAKRISTO TANZANIA (TCF)

 “ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI, NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA” (Lk.2:14)

TAMKO LA PAMOJA LA MKUTANO MKUU WA DHARURA WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA
   
1.Utangulizi    

Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) linajumuisha Taasisi Kuu za Makanisa nchini kama ifuatavyo:- Jumuiya ya Kikristo Tanzania – CCT Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania – TEC Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania – PCT Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA (Watazamaji) Katika Mkutano wake Mkuu wa Dharura uliofanyika katika Kituo cha Mikutano na Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini, Jijini Dar es Salaam, tarehe 8 Machi, 2013;   Wajumbe walitafakari kwa undani juu ya kuzorota kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini Tanzania, pamoja na mauaji na mashambulizi ya viongozi wa dini; na hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya uhalifu huo unaotekelezwa na Waislamu wachache.    

Katika taswira hiyo, Kanisa lilitathmini juu ya wajibu, utume, na sauti yake ya kinabii kwa taifa letu kuhusiana na mambo hayo.    

2. Hali halisi ilivyo hivi sasa hapa nchini kwa mtazamo wa Kanisa Ushahidi wa kihistoria na kimazingira unaonyesha wazi kuwa kwa sasa Kanisa nchini Tanzania limo katika kipindi cha mateso ya kimfumo (systematic persecution), kama vipindi vingine 10 vya mateso katika Historia ya Kanisa hapa duniani. Pamoja na mateso haya ya kimfumo, tunatambua wazi kuwa wanaotekeleza haya ni kikundi kidogo tu cha Waislamu wa Tanzania, kama wale wengine wa Barani Afrika (k.m. Boko Haram kule Nigeria).   Waislamu walio wengi hawafurahii mambo yanayotokea. Wao pia wanaitazamia Serikali kuthibiti hawa wachache wanaochafua dini ya Kiislamu na kuwafanya Waislamu wote waonekane kuwa maadui wa Ukristo, jambo ambalo siyo kweli. Kutokana na hali hiyo, mkutano mkuu wa dharura wa Jukwaa la Wakristo umeyaangalia maeneo makuu yenye migogoro ikiwa ni pamoja na:  

 2.1. Mgororo wa nani anastahili kuchinja kitoweo Hivi karibuni hapa nchini tumeshuhuduia mgogoro juu ya uchinjaji wa mifugo ambayo nyama yake inapaswa kuuzwa kwa watu wa imani mbalimbali wakiwemo Wakristo na Waislamu. Tunafahamu kwamba sheria ya nchi yetu inaweka bayana juu ya usalama wa nyama hizo kiafya, lakini sheria haielekezi kuwa dini fulani ndiyo waumini wake wanapaswa kuchinja mifugo hiyo.    

Kwa misingi hiyo Kanisa linatamka kuwa:-    

a) Hoja ya dini moja kudai kuhodhi (exclusive right) uchinjaji wa mifugo kwa misingi ya imani yake ni kinyume cha haki ya uhuru wa kuabudu ambayo amepewa kila mtu ndani ya nchi hii kikatiba katika Ibara 19.  

 b) Kwa kuwa kuchinja wanyama na ndege ni Ibada kwa Waislamu, Kanisa litambue na kuheshimu jambo hilo.   Lakini pamoja na kutambua haki ya Waislamu kujichinjia wanyama na ndege kama Ibada kwao, Wakristo wasilazimishwe kula nyama zilizochinjwa kwa misingi ya Ibada za Kiislamu.   Kwa kuwa wananchi wa Tanzania ni wa dini mbalimbali na mila za makabila mbalimbali, tunaitaka Serikali itamke wazi kuwa kila raia ana uhuru wa kufuata imani yake katika suala la uchinjaji.    

c) Kuhusiana na jambo hili tunashindwa kabisa kuelewa msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali.   Wakati wa Serikali ya awamu ya pili chini ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Muislamu, ulipotokea ugomvi wa mabucha ya nyama ya nguruwe Dar es Salaam, Rais huyu Mstaafu kwa kulinda Katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda, alisema mwenyewe kwa nguvu zote kuwa kila mtu ana uhuru wa kula anachotaka na mtu wa dini moja asimhukumu mtu wa dini nyingine kwa kile anachokula. 

Baada ya Rais Mstaafu kukemea jambo hili, hali ikawa ya amani na utulivu.   Kwa nini Serikali yetu ya sasa inapata kigugumizi kuhusiana na suala zima la nani achinje? 

d) Kwa mantiki hiyo hapo juu katika kipengele cha a-c, Wakristo wanaitaka Serikali iweke utaratibu wa kugawana machinjio na mabucha kati ya Wakristo na Waislamu ili kila Mtanzania awe huru kujinunulia kitoweo mahali anapotaka.   Sambamba na kuitaka Serikali kufanya hivyo, tunawakumbusha Wakristo wote Tanzania kuelewa kuwa watakuwa hawajavunja sheria yoyote ya nchi wakiamua kujichinjia kitoweo chao wenyewe. Kuhusiana na tangazo hili kwa Wakristo wote, tunaitaka mihimili ya dola (Serikali na Mahakama) kuheshimu Katiba ya Nchi yetu, na kipekee kuhusiana na jambo hili Ibara ile ya 19. 

e)   Kwa upande mwingine, kwa kuwa tayari zipo bidhaa za vyakula katika nchi hii ambazo zina nembo ya ‘halal’ na nyingine hazina nembo hiyo, huu ni uthibitisho kuwa vyakula hivyo vimegawanywa kwa kufuata misingi ya imani za kidini. Kwa hiyo, madai ya kugawanya machinjio na mabucha kwa kufuata misingi ya dini sio jambo jipya kwa sasa katika nchi hii.   

 2.2 Uchomaji wa Makanisa ulioambatana na vitisho na mauaji ya viongozi wa KanisaKanisa linalaani vikali mauaji ya kidini yanayoendelea kufanywa pamoja na vitisho (systematic persecution) kwa viongozi wa Kanisa na Wakristo wote kwa ujumla. Mtiririko wa matukio mbali mbali ya nyuma yanatudhihirishia kuwa kumekuwepo na mpango wa muda mrefu wa haya yanayotokea sasa hivi.    

Tarehe 15 Januari 2011, kundi la Waumini wa Kiislamu walipokutana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, miongoni mwao walikuwamo mashehe, walijadili hali ya nchi ya Tanzania kuongozwa kwa mfumo wa kidini.    

Mkutano huo ulihitimishwa kwa kutoa tamko dhidi ya kile kilichoitwa mfumo Kristo katika nchi yetu! Japo Serikali na vyombo vyake vya usalama wa Taifa vimekuwa vikipata taarifa za vitisho dhidi ya viongozi wa Kanisa, mauaji, kuchomwa kwa nyumba za ibada, pamoja na maneno ya uchochezi kupitia mihadhara, vipeperushi, CD na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taasisi zinazofahamika, hata hivyo Serikali kwa kiasi kikubwa imeshindwa kuchukua hatua kwa wakati muafaka na wanasubiri hadi maovu yatendeke ndipo ati waanze kufanya uchunguzi.  

 Kwa Serikali yetu inaonekana wazi kuwa katika hili ile methali kwamba “Kinga ni bora kuliko tiba” haina maana yoyote.    

Hii ni kuonyesha udhaifu mkubwa wa vyombo vya usalama wa Taifa au pia kwamba vyombo hivi vinafurahia kutoweka kwa amani nchini mwetu, jambo ambalo linalifanya Kanisa nchini Tanzania liamini kwamba matukio haya yanayoendelea kutokea ni dalili kuwa Serikali ina agenda ya siri dhidi ya Ukristo.    

Kutokana na hayo Jukwaa la Wakristo Tanzania linatamka kama ifuatavyo:    

a) Tunatambua kwamba ni jukumu la Serikali kuwatendea raia wake kwa usawa na bila ya ubaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 12 na 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.   Viongozi wa Kanisa wanatamka kwamba Serikali imeshindwa kuheshimu Katiba juu ya hizi haki za raia wake na kupelekea waamini wa dini ya Kikristo kukosa imani na Serikali iliyoko madarakani, hasa kuhusu ulinzi na usalama wao na mali zao kama inavyoagizwa kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.   Kama Serikali inaona haiwezi kuwahakikishia wananchi usalama wa uhai wao na mali zao, na hivyo kuwafanya waishi maisha ya hofu inayotokana na vitisho, basi kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, hakuna sababu ya Serikali iliyoko madarakani kung’ang’ania kuongoza nchi.    

b) Kwa kuwa ulinzi wa raia ni haki ya kikatiba na kisheria, Serikali inatakiwa iwalinde raia wake.    Kama Serikali imeshindwa kuwalinda raia wake, Kanisa linataka Serikali ikiri hivyo ili Kanisa liwaambie wananchi waiwajibishe Serikali na Viongozi wanaoifanya Serikali ishindwe kutimiza wajibu wake.   Jukwaa la Wakristo linasema: Kama Serikali haitachukua hatua za makusudi dhidi ya mambo haya yaliyoainishwa hapo juu, Kanisa litachukua hatua ya kuwaambia waamini wake kwamba Serikali iliyoko madarakani inaibeba dini moja, na hivyo Kanisa litatafakari upya uhusiano wake na Serikali.  

 3. Wakristo walioko Zanzibar Wakristo walioko Zanzibar wanatishiwa maisha yao na mali zao zinaharibiwa mara kwa mara, kiasi cha wengine kuamua kuhamia Tanzania Bara. Kigezo cha unyanyasaji huo ni suala la udini na muungano. Inaonekana ni kama vile Watanzania waliozaliwa Bara hawana haki ya kuishi Visiwani. Na kumbe wale waliozaliwa Visiwani wafikapo Barani wana haki zote. Kanisa linaitaka Serikali iwahakikishie Wakristo walioko Zanzibar usalama wao na wa mali zao maana hiyo ni haki yao ya Kikatiba.    

4. Vitisho na mauaji ya Wanakanisa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ichukue hatua za makusudi za kuzuia vitisho na mauaji kwa Viongozi wa Kanisa na Wakristo kwa ujumla. Vinginevyo Kanisa litautangazia ulimwengu kuwa Tanzania ni nchi mojawapo inayovunja haki za binadamu kwa ubaguzi wa kidini na kulitesa Kanisa kimfumo.    

5. Matumizi ya Vyombo vya Habari: Kwa kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimeruhusu vitumiwe kuwatukana Viongozi wa Kanisa, tunatoa nafasi kwa vyombo hivyo kuomba radhi; vinginevyo tutaitaka dunia ivielewe kuwa navyo ni sehemu ya chanzo cha migogoro. Pia tunachukua nafasi hii kuvitahadharisha vyombo mbalimbali vya habari kupima kwa kina ni nini kinachosemwa na viongozi wa kidini ili kuviepusha vyombo hivyo kutumika kwa nia ya uchochezi; yasije yakatukuta kama yale yaliyotokea kule Rwanda 1994.  

 6. Hitimisho: 

Kanisa linaendelea kusisitiza kuwa silaha kuu ya Mkristo katika nyakati hizi ni maombi na kufunga. Kwa mantiki hiyo, Kanisa linawataka Wakristo wote nchini Tanzania kuungana kwa pamoja katika maombi na kufunga kwa muda wa siku saba kwa ajili ya hali hii iliyojitokeza hapa nchini. Maombi hayo na mfungo vifanyike kabla ya Pasaka, yaani kuanzia, tarehe 24/3/2013 hadi 30/3/2013.    

Kwa niaba ya Maaskofu 177 walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Dharura wa Jukwaa la Wakristo na kutoa maazimio hayo.  

 1. Askofu Peter Kitula – Mwenyekiti CCT

 2. Askofu Tarcisius J. M. Ngalalekumtwa Rais TEC  

3. Askofu David Batenzi Mwenyekiti PCT DAR ES SALAAM,        MITAZAMO YA WANAMAONI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA MZALENDO.NET   Makame silima 22/03/2013 at 3:52

Wazanzibar Taget ya Tamko hili la wakristo mazumuni hasa ni Zanzibar kwa kuliwa Padri Mushi, Hii ndio chachu zaidi ya kikao hichi utazani Tanganyika hakuliwi Mapadri au vitendo vya mauaji kama hayo ya Maskofu.
Hili la Padri Mushi linawasi wasi kuwa inawezekana ni vile watu wanavyo sema kuwa mtandao wa kundi la Maskofu kuingiza Madawa ya kulevya umehamia Zanzibar bada ya kule Bara kustukiwa na kukamatwa maskofu wengi.

Lakini kwa upande wa Zanzibar hili limekuzwa kwa sababu kuna agenda ya siri kutumilia mwanya huu ili kuwazibidi/kuzibitiwa wananchi wa Zanzibar kwa vitisho vya udini au Ugaidi kwa vile wananchi wa Zanzibar %99 ni waumii wa dini ya Kislamu na Mapadri wameshindwa kuwazibiti kutokana n wingi wao Wazanzibar .

Wazanzibar tutahazari na chokochoko na sumu wanazo zimwaga ndani na nje ya Zanzibar wakristo kuipaka matope Zanzibar na watu wake ili ionekane Zanzibar wananchi wake wanawapiga vita Wakristo wa Zanzibar hali yakuwa ni chuki zenye kupandikizwa na Mapadri wa Tanganyika.

Tahadharani viongozi wetu wa Smz na mbinuza Maskou kuipaka matope na kupandikiza fitna za udini , Wananchi wa Zanzibar inajulikana kuwa ni waumini wa dini ya Kislamu %99 n wana haki kwa wingi wao kuweka mbele dini yao ambayo ndioyenye utamaduni wa kizanzibar.

Kwa hio viongozi wa Smz mukikubali kulichwa mawazo na kupokea sumu za % 0 ya Mapadri walkuja Zanzibar na mukaacha 599 ya wenyeji wa Zanzibar basi Zanzibar na watu wake mudakuwa hamukuitendea haki na Allah hato wacha kwa hilo.

Huwezi kusema kama kigezo cha Maskofu wakitumiacho kuwa Tanzania haina dinina unaweza kuichi na kuhubiri dini yako popote pale ndani ya Tanznia? hii kwa Zanzibar isiruhusiwe kwani Tanzania ni nchi ya Muungano wa nchi mbili yani ilokuwa Tanganyika na Zanzibar .

Kwa upande wa Zanzibar inayo dini kwa vile utamaduni wa Zanzibar unatokana na dini yao na mila zao zinatokana na dini yao sasa ukisema Tanzania haina dini nikuwanyima haki ma-jourty ya Zanzibar ambao wakazi wake ni waumini wa dini ya kislamu.

Tunawanasihi viongozi wetu wa Smz wasiangalie siasa tu , wajaribu kuzinduka kwa kuangalia mbinu na mipanga ya makafiri kwa kutaka kuinakamiza Zanzibr na kizazi chake, hili ni jukumu kubwa kwao mbele ya Allah.

Hii leo niaibu kuskia familia ya kizanzibar inauza dini yao kwa $100 dolla (innalillahiwainnailaihirojiun) M/mungu wazinduwe viongozi wetu wa Smz na uiokowe Zanzibar yetu, hal ni yakutiha na ni aibu na fedheha.


Fidoski 21/03/2013 at 5:46


Habari hii sio kwa wanamzalendo bosi wangu, hii habari ni kwa serikali ya Kikwete, hayo ni madai yao kwa serikali, ila mimi naona wamekosa hekima viongozi hawa wa dini, maana kama kweli nyinyi ni watu wazuri na malengo yeni mazuri basi wangetumia busa na hekima ktk kudai hili suala lao. kuna taratibu nyingi tu

1. wangeomba wakutane na raisi moja kwa moja ili waweze kumuelezea a to z au

2. kama kumuona ni ngumu wangemuandikia barua raisi wakafikisha madai yao kwa njia ya barua halafu wakasubiri majibu kutoka kwa raisi baada ya hapo wakiona hawajaridhika na maji hayo ndio watoe tamko sio kutoa tamko kwanza tna kwa vitisho eti wanaitishia serikali isipofanya hivyo wanavyotaka basi watawatangazia wananchi waitoe madarakani serikali iliopo, wawatangazie wakristo wezao na sio wananchi wote maana kwa mananchi anejitambua hawezi kusikiliza utumbo huu na aka take action eti tu kwasababu ya kuchinja, ivi unaakili wewe? sala la kuchinja unalishadidia kiasi cha kuitishia serikali, huko ni kukosa hekma na busara tena hawa ni viongozi wa juu wa dini, sijui hao wanaowaongoza wanajifunza nini kupitia viongozi hawa? eti jamani hebu nisaidieni.

Kama ni kudai na sisi tutadai siku ya mapumziko iwe alhamisi ( kwa ajili ya maandalizi) na ijumaa ( kwa kufanya ibada na mapumziko) kwa waislamu, maana tumeshakuwa wajinga sisi waislam tunaokubali kupumzika jumamosi na jumapili ambapo wakristo wote wanakwenda kufanya ibada katika makanisani. au vipi jamani?

Ashakh (Kiongozi) 21/03/2013 at 7:55
MMMhhhh

Kweli kazi kwetu! Hao ndio Wakiristo.

Ndio walioiweka serikali hii madarakani kwa makubaliano wautumikie, ikiwa wamekhalifu miadi hapo watakuwa wamekwenda kinyume namakubaliano yao na hivyokutoamwanya wa kukuadhibu.

Inaonekana kama vile na wao wameogopa kitu fulani hivi, kwani hawana kawaida ya kuripuka kama hivi. Wao huenda na strategies tu, iweje leo waje na msimamo dhahiri shahiri?

Moja katui ya haya; wameona mambo hayawaendei vizuri au wamejiona sasa wameshapata power ya kusema na kufanya chochote wananchotaka.

Mwisho nasema “WAKOME” kuihusisha Zanzibar na fitna zao.Hala abdalla 21/03/2013 at 6:21
Kweli haya ni maneno ya kusemwa na watu wa Mungu?huu si uchochezi tu na uongo wa wazi?toka lini Zanzibar kunyaynyaswa wa bara?bali tumeshuhudi wao kupewa fursa zaidi,tunao makatibu wa kuu na maofisa kibao,pia hata ktk uchaguzi wapemba wangapi wanoishi Unguja zaidi ya miaka 10 wamekataliwa kupiga kura lkn wao hukusanywa kwa gari na kupewa priority,nna mfano mmoja tulikua na mfanyakazi wa nyumbani hapo mpendae ambae alifika znz chini ya mwaka ikawa uchaguzi tayari basi alitwambia mwenyewe wameekewa gari na sheha na wabara wenzake ili wapelekwe kujiandikisha, na huo udini udini gani ?

kwa sababu Waislam wamechoka maonevu wamepaza sauti kidogo tu ndio imekua mwao?Waislam mara kibao wamenyanyaswa kwa mavazi yao kuna waliotolewa madarasani na maofisini kwa kuvaa hijabu au kofia lkn hatujawahi kusikia sister kakatazwa kuvaa nguo yake juu ya kua kuna uniform ikiwa ni chuo au schoo au kazini nlikua nafanya degree tulikua na masister wakisoma nurse lkn wakivaa nguo zao na scurf zao,rangi ya blue na wenzao wakivishwa vimini pink na kikofia hata uwe muislam hapana ruhusa.

kama wao ni waadilifu mbona hatujasikia wakitaja mauaji ya sheikh?au roho ya mkristo tuu ndio tamu ya sheikh halali kutoka kikatili?

na kama wao ni watu wa amani mbona pale wakereketwa wakikatoloki na wengine wanapoanzisha fujo hawakemei au ni safi tu kwao ni halali kuwadhulumu waislam maana kwao wao si binaadam maana hawajamuamini Yesu.

basi yasiishie kuchinja tu wajue kua na holiday iwe na friday,na kwaya marufuku ofisini na redio za kikristo, la sivyo na Quraani na mawaidha yapigwe,pia hatuishii kuchinja tu itabidi shughuli za makafir ( =watu waliokataa tauhidi) marufuku kushiriki kwani kuna nyama haramu pia kununua mishikaiki na vitu vyote vya nyama,na hii inamaana hata kama ndugu yako wa damu usiende hii ndio chuki wanayotaka kuipandikiza hali hapa bara utaona mtu ana mtoto au ndugu wa damu au wazazi ambao ni muislam.

lkn mm naona wanafanya dhulma wakijua bcos wanajua wanamtumikia Mungu asie sahihi kama kweli ni watu wa Mungu wa haki wasingesema haya.

Na hizi chokchoko za znz ni ajenda yao mahsusi lkn na sisi tunasema ALLAH atawashinda

“wanataka kuizima nuru ya ALLAH kwa vinywa vyao na ALLAH ni mwenye kuitimila”

wataondoka tu patupuINSHAALLAH na dhulma zao zina mwisho wao hawana hati miliki ya nchi.


Ghalib 21/03/2013 at 10:13
ipo nasi kupigania siju ya alhamis na ijumaa kuwa ni siku ya mapumziko kislamu kwa waislamu, leo hi kazini tuende na msikitini tuende au ukose kazi !

Wao jumapili wanafanya ibada zao wakiwa free kabisa ! Nani anaupendeleo katika hili taifa ?

Sisi zanzibar asilimia 99 waislamu kwa nini alhamis na ijumaa haiwi ni mapumziko ? Wakati umefika kudai haki zetu

wakiristo wanaonesha wazi wazi nia zao zilivyo kuwa mbaya zidi ya wazanzibari waislamu hasa ndiko waliko lenga hoja yao.

Kuuliwa kwa padri mushi wana ushahidi gani kwamba haya ni mapigano zidi yao na waislamu ? Huu ni uchochezi, hapa wameenda mchomo,kwa vile hi habari wameandika kanisa sheria zitapuuzwa, tusubiri baada ya siku tatu watatoa tamko sio wao walioandika huo utumbo ju.