Tuesday, December 10, 2013

KWA HERI MADIBA

Kwa heri Madiba kiongozi uliesimamia utu
Kwa heri madiba kiongozi mwenye uthubutu
Kwa heri Madiba kiongozi uliyeamini Ubuntu
Kwa heri Madiba kiongozi uliyekuwa na msimamo usio butu.

Hata walipojaribu kutaka kukuvunja moyo hawakuweza
Hata walipotaka kupandikiza sumu ya uasi waliishia kwenye majeneza
Hata walipoiweka minyororo ya ubaguzi kelele zilisikika kwenye magereza
Wewe ndie Nelson Rolihlahla Mandela kiongozi kusamehe uliyeweza.


HAMBA KAHLE MADIBA -SIYABONGA 1918-2013.

No comments: