Tuesday, November 26, 2013

YALIYOJIRI : MKUTANO WA CHADEMA NA WAANDISHI WA HABARI Na Mohamed Mtoi Kutoka JAMII FORUMS

Mheshimuwa John Mnyika, Tundu Lissu na Benson Kigailla ndio wazungumzaji wakuu.
Mnyika - amewaleeza waandishi kuwa sekritarieti ya chama ilikaa kikao chake jana kujadili mambo kadhaa ndani ya chama.

Ameeleza kuwa wahusika wamesha andikiwa barua zenye tuhuma zao 11 wanazotakiwa kuzijibu ndanj ya siku 14.

Ameeleza kuwa press conference waliyofanya wamejitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao.

Benson Kigailla anaeleza mikakati inayoendelea kwenye kanda ambayo kimsingi ripoti zililetwa kwenye kamati kuu.

Anasema mpango na programu ya chadema ni msingi pamoja na M4C kanda unaendelea kwa mafanikio makubwa kwani misingi inaendelea kuundwa na mpaka sasa zaidi ya wakunzi elfu tisa kutoka katika kanda mbalimbali wameshafundishwa.

Anaeleza kuwa kuna timu nne zimeundwa kwenda kwenye kanda mbalimbali kukagua misingi iliyokwisha simikwa.

Ziwa Mashariki misingi 3069 kati 7098

Ziwa Magharibi 3840 kati 9757

Kaskazini 3278 kati ya 8417

Juu kusini 2113 kati ya 10,857

Magharibi Kata 235 kati ya kata 315

kanda ya Kati Kata 363 kati ya 495

Kanda Kusini 219 kati ya 387

Kanda ya Pwani misingi 846

Tundu Lissu.

walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba na maadili ya uongozi, kuvuliwa kwao nafasi zao hakuhusiani na mambo ya PAC wala kuuza nafasi zetu za wagombea kwa maccm, wala kutokushiriki kwenye ziara za chama.

anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu"

anasema chadema haijaanza kufanya maamuzi magumu leo, ilishafanya hivyo kwa Dr Walid Kaburu na kwa Chacha Wangwe na mara zote vyombo vya habari vimekuwa vinaandika kuwa CHADEMA yapasuka, mara CHADEMA inakufa lakini kipindi chote haijawahi kufa wala kupasuka, na hata kwenye hili haitakufa kama ikitokea kamati ikiwafukuza.

Lissu alieleza kuwa - Kitilla amepotosha kuwa kamati kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya ujumbe wa kamati kuu maana amechaguliwa na baraza kuu. Amesema Zitto alipaswa kumkumbusha rafiki yake maana yeye (Zitto) alikuwepo kwenye kamati kuu iliyo mvua ukatibu mkuu Dr Walid kaburu, na makamu mwenyekiti bara Chacha Wangwe. kama iliweza kwa Kaburu na Chacha Wangwe (Katibu mkuu na Makamu mwenyekiti) imeweza na kwake pia ambaye hana vyeo hivyo, hivyo aache kupotosha umma kwa makusudi.

muandishi mmoja aliuliza kuhusu vurugu za kuchana bendera huko Kigoma, majibu yalikuwa - kurugenzi ya ulinzi na usalama ya chama imewasiliana na viongozi wa chama Kigoma na watalitolea wao taarifa lakini taarifa za awali ni kwamba ulikuwa mpango wa kuigiza ulioandaliwa na watu waliotumwa na wameshajulikana na hatua zaidi ziko chini ya uongozi wa tawi husika.

No comments: