Wednesday, November 13, 2013

WANASIASA WANAPOFANYA PICNIC KATIKA MASUALA YA MSINGI YA NCHI KWA KIGEZO CHA TUME NA KAMATI MAALUM.Kuna kamati maalum ya wanasiasa wapo "picnic" mkoani Mtwara wakifanya mjadala na wananchi juu ya chanzo cha vurugu za gesi zilizotokea mkoani Mtwara mapema mwaka huu kabla na baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Kinachoshangaza na kuchekesha ni kitendo chao cha kuchunguza chanzo wakati wao wanajulikana kwamba ndio nguzo na chanzo cha vurugu zote kwa wananchi kuchoshwa na porojo zao wao wakivimba matumbo maendeleo hayaonekani hata kwa kuwakumbusha na kuwakumbusha katika masuala ya msingi. Ingekuwa heri wangesema iundwe Tume ya Maridhiano baina ya Serikali na Wananchi "Truth and Reconciliation Commission" kwani wapo wengi wahanga wa matokeo haya na wao wanasiasa wawaombe msamaha wananchi. 

Badala yake unasababisha madhara tena baada ya kuonywa tena na tena baada ya madhara unakuja kumuuliza yule uliyemtenda ati kwani ilikuwaje? Haumuulizi ukiwa na guts za kumuuliza unamuuliza ukiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, ving'ora na Mwananchi akipigwa na jua kali. 

Mkimaliza mnaingia kwenye gari yenye viyoyozi mnapanda ndege makarani wenu wanaandika ripoti mnaipeleka posho ya mamilioni mmekula ambayo ni kodi ya mwananchi. Yaani hamna cha kupoteza. Wapo watakaoona wanahukumiwa bure lakini watake wasitake ni lazima waukubali ukweli. Wanasiasa mmezidi kuupotosha ukweli na kibaya zaidi mnawatumia makasuku ambao wanaupotosha ukweli kwa jamii nzima ya kitanzania. 

Tanzania sio mali yenu na vizazi vyenu, Tanzania ni ya Watanzania.

No comments: