Monday, November 11, 2013

DEREVA WA BODA BODA AUAWA MTWARA.

Tukio la mauaji limetokea maeneo ya Mtwara /Mikindani mtaa wa Mkundi bara bara ya kwenda mji mwema kwa dereva wa Boda boda ajulikanaye kwa jina la SHARAFI anayekadiriwa na umri wa miaka 26 na 27  aliyekuwa akiendesha pikipiki namba T 645 CNY.

 Chanzo cha kifo chake ni kuchomwa na kitu chenye ncha kali. Haijaelezwa ni sababu zipi zilizopelekea mauaji yake lakini wabashiri wanasema pengine ni jaribio la wizi. Piki piki imeonekana umbali kidogo na eneo  tukio la mauaji. Mamlaka husika zinaendelea na uchunguzi.

HABARI NA PICHA: MUANYA MKOLOMA

No comments: