Kwanza kwa tafsiri ya kawaida ya "mfumo kristu" ni "utaratibu unaotumika kuongoza/kutawala mahali/watu kwa misingi ya dini ya kikristu"

Nchini Tanzania kumekuwepo na madai kuwa Tanzania "ni ya mfumo kristu",

Madai haya ni mazito na yanahitaji majibu yakinifu kutoka serikalini kwakuwa yanagusa imani za watu, yana athiri uchumi wetu, yana athiri siasa za nchi yetu, yana athiri elimu yetu pia yana athiri ajira nchini, lakini serikali imekuwa kimya kwa mda mrefu sasa,

Kwa dhana hiyo hapa wanaosema Tanzania ni ya mfumo kristu inamaana kuwa sekta zote zinazosimamiwa na serikali ya Tanzania zipo chini ya Ukristu na hata serikali kuanzia Urais hadi mjumbe wa nyumba kumi nk!

Mwaka 2011 nilijipa kazi maalumu yakuusaka ukweli kuhusu madai hayo,

UTAFITI wangu ULIFANYIKA katika majiji ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Zanzibar, hii ni kutokana na kuwa majiji haya ndio kitovu cha mambo yote na mwelekeo wa taifa letu, na ndiyo yenye wakazi wengi zaidi ambao ni zaidi ya 15% ya Watanzania wote!

Haikuwa kazi rahisi kupata nilichokihitaji hasa kila nilipojaribu kuomba ufafanuzi kwa walioimba na wanaoendelea kuimba wimbo huo wa "Mfumo Kristu" kukosa majibu mujarabu,

Nilipanga safu yangu ya kiutafiti katika makundi yafuatayo,

1) Siasa,
2) Elimu
3) Ajira
4) Uchumi

A. Katika anga la siasa hapa nilijikita kuangalia Watanzania wanaohudumu katika ngazi za kimaamuzi ya kisiasa tu kwa jiji la Dar, Mbeya, Mwanza, Arusha na Zanzibar

Jiji la Dar limekumbatia wanasiasa 521,556 ambao huendeshea shughuli zao za kisiasa Dar tu, niliowahoji imani zao za kiroho ni 360,001 kati ya hawa 270,823 ni waamini wa Uislamu na 89,100 ni waamini wa Ukristu huku 72 ni waamini wa imani zingine na 6 ni waamini wa Urasta fari.

Kundi la wanasiasa lililobaki nilitumia kigezo cha majina yao japo kina akisi kwa 98% tu ya ukweli wao!

Jiji la Mbeya lina wanasiasa 1360 ambao wanahudumu katika siasa ndani ya jiji hilo. niliowahoji kujua imani zao za kiroho ni 386 kati ya hawa 272 ni waamini wa Ukristu na 112 ni waamini wa Uislamu huku 2 ni waamini wa imani zingine na hakuna waamini wa Urasta fari.


Jiji la Mwanza lina wanasiasa 2682 wanaohudumu katika siasa ndani ya jiji hilo, niliowahoji kujua imani zao za kiroho ni 1230 kati ya hawa 324 ni waamini wa Uislamu na 696 ni waamini wa Ukristu huku watu 58 ni waamini wa imani zingine na hakuna waamini wa Urasta fari.

Zanzibar ina wanasiasa 682 wanaohudumu katika siasa ndani ya mamlaka hiyo, niliowahoji kujua imani zao za kiroho ni 123 kati yao 120 ni waamini wa Uislamu na 2 ni waamini wa Ukristu huku watu 1 ni waamini wa imani zingine na hakuna waamini wa Urasta fari.


B. ELIMU

Hapa kwenye sekta ya elimu kwakutumia takwimu za wizara ya Elimu, nilitumia majina ya wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2011-2012 kutambua imani zao japo sio njia aminifu kwa asilimia mia.

Mkoa wa Dar mwaka 2011 walihitimu wanafunzi wa kidato cha nne 120,032, kati yao 111,231 ni Waislamu, na 8,801 ni Wakristu, hapa dini nyingine hazikuangaliwa!

Mkoa wa Mbeya mwaka 2011 walihitimu wanafunzi wa kidato cha nne 76,136, kati yao 25,621 ni Waislamu, na 50,515 ni Wakristu, hapa dini nyingine hazikuangaliwa!

Mkoa wa Mwanza mwaka 2011 walihitimu wanafunzi wa kidato cha nne 100,116, kati yao 23,522 ni Waislamu, na 76,594 ni Wakristu, hapa dini nyingine hazikuangaliwa

Zanzibar mwaka 2011 walihitimu wanafunzi wa kidato cha nne 89,139, kati yao 89,138 ni Waislamu, na 1 ni Wakristu, hapa dini nyingine hazikuangaliwa


C. AJIRA

Kwamjibu wa takwimu zilizopo Wizara ya Utumishi na ambazo mimi nimetzitumia kama rejea kuu ni kuwa,

Mwezi wa 7 mwaka 2012 Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na wafanyakazi 876,981, kati yao 492,238 ni Waislamu, wakati 384,700 ni Wakristu na 43 ni wa dini nyinginezo!

Mwezi wa 7 mwaka 2012 Mkoa wa Mwanza ulikuwa na wafanyakazi 226,139, kati yao 114,023 ni Waislamu, wakati 112,116 ni Wakristu na 0 ni wa dini nyinginezo!

Mwezi wa 7 mwaka 2012 Mkoa wa Mbeya ulikuwa na wafanyakazi 199,226, kati yao 99,221 ni Wakrstu, wakati 100,005 ni Waislamu na 0 ni wa dini nyinginezo


Mwezi wa 7 mwaka 2012 Zanzibar ilikuwa na wafanyakazi 113,206, kati yao 113,001 ni Waislam, wakati 205 ni Waikristu na 0 ni wa dini nyinginezo


D. UCHUMI

Katika anga la uchumi nchini nilimulika zaidi idadi ya wafanyabiasha katika miji hiyo kwakutumia takwimu za TRA na BRELA

Mwezi wa kumi nambili Mwaka 2012 jiji la Dar es Salaam pekee lilikuwa na makampuni (Limited) 4737 kwamjibu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, kati ya hayo utafiti unaonyesha 3826 yalikuwa yanamilikiwa na waamini wa Uislamu kwa 100%, wakati 911 yalikuwa yanamilikiwa na Waamini wa Ukristu,

Eneo la Kariakoo ambako kunamkusanyiko mkubwa wa wafanyabiashara na biashara zao kulitoa picha stahiki za utafiti wangu,
Kariakoo na viunga vyake pekee nilitembelea maduka 489,125, kati ya hayo 312,568 yanamilikiwa na waamini wa Uislamu, na maduka 176,500 yalikuwa yanamilikiwa na waamini wa Ukristu wakati maduka 57 wamiliki wake ni wa dini nyingine


Mwezi Januari Mwaka 2013 jiji la Mbeya lilikuwa na makampuni (limited) 197 kwamjibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kati ya hayo utafiti unaonyesha makampuni 102 yalikuwa yanamilikiwa na waamini wa Uislamu, wakati makampuni 95 yalikuwa yanamilikiwa na Waamini wa Ukristu.

Jiji la Mwanza lilikuwa na makampuni (limited) 204 kwamjibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kati ya hayo utafiti unaonyesha makampuni 102 yalikuwa yanamilikiwa na waamini wa Uislamu, wakati makampuni 95 yalikuwa yanamilikiwa na Waamini wa Ukristu.

Zanzibar ililikuwa na makampuni (limited) 81 kwa mjibu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar, kati ya hayo utafiti unaonyesha makampuni 72 yalikuwa yanamilikiwa na waamini wa Uislamu, wakati makampuni 9 yalikuwa yanamilikiwa na Waamini wa Ukristu.

Msomaji unaweza kutumia mang'amuzi yako kujua hoja ya wenye hoja!

Ndugu zangu Watanzania, tuendeshe siasa za kistaarabu kuilinda nchi yetu iliyojengwa kwa jasho na damu, dhana za kufikirika na zenye agenda mtambuka na wakwale zitalipeleka taifa letu pabaya!