Sunday, August 4, 2013

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015 (COUNT DOWN TO 2015 ELECTIONS-II)- 2

Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015

1.      Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2.      Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.      Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4.      Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5.      Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.      Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.      Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.      Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.      Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.  Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.  Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.  Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13.  Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.  Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.  Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.  Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.  Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.  Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.  Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20.  Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21.  Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22.  Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23.  Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24.  Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25.  Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.  Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27.  Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28.  Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29.  Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30.  Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31.  Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32.  Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33.  Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34.  Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35.  Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36.  Kulinda haki za walemavu - Makete
37.  Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38.  Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39.  Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.  Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41.  Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42.  Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43.  Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44.  Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45.  Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46.  Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47.  Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48.  Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49.  Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50.  Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51.  Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52.  Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53.  Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54.  Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55.  Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56.  Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57.  Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58.  Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59.  Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60.  Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61.  Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62.  Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63.  kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64.  Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65.  Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66.  Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67.  Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68.  Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha

69.  Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

No comments: