Monday, June 10, 2013

SHUGHULI KUSIMAMA TENA LEO MTWARA

Ujumbe uliosambazwa wiki iliyopita kuwahimiza wana Mtwara kusitisha shughuli zao leo hii ili kuishinikiza serikali iwaachie viongozi wa vuguvugu la gesi Mtwara umeonekana umechukuliwa tahadhari na vikosi vya usalama ambapo matangazo yalitolewa siku ya jumamosi kuwahimiza wananchi kuendelea na shughuli zao  na kutoa taarifa yoyote inayoashiria uchochezi na uvunjifu wa amani hivi sasa vyombo hivyo  vimetanda katika kila kona ya mji wa Mtwara na safari hii wameweka vizuizi katika baadhi ya maeneo. Hata hivyo muitikio wa kusitisha shughuli sio mkubwa kama ilivyokuwa mwanzoni kwani kuna maeneo ambayo shughuli zinaendelea kama kawaida.

Hali ya hofu imetanda kufuatia mbunge kipenzi cha wananchi wa Mtwara Mjini Mheshimiwa Murji kukamatwa baada ya kujisalimisha mwenyewe akituhumiwa kwa uchochezi. Hali hii italeta athari kubwa kisiasa kwa upande wa chama Tawala maeneo ya Mtwara mjini. Mpaka sasa hakuna vurugu zozote zilizojitokeza na hali ni ya amani.

No comments: