Thursday, June 27, 2013

KUVUNJIKA KWA MFUMO WA USALAMA DALILI KUU YA KUTAMALAKI UFISADI

 Na Lula Wa Ndali Mwana Nzela,
Maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa “ufisadi ni adui mkubwa zaidi wa usalama wa nchi wakati wa amani kuliko vita” ni ya kweli. Nyerere alielewa kile ambacho inaonekana watawala wetu wa leo wameshindwa kukielewa – ufisadi (corruption) unapoachwa kutamalaki ina matokeo makubwa na hasi kwa taifa na usalama wa taifa.

Tukio la ughaidi lililotokea Arusha hivi juzi ni dalili tu ya matokeo ya kuvunjika kwa mfumo wetu wa usalama ambao –naomba kusema – umeathirika na ufisadi. Ufisadi husababisha uvunjaji wa haki.
Jambo moja lililo wazi kuhusu ufisadi ni kuwa unagusa moja kwa moja juu ya upatikanaji wa haki katika jamii. Hii ni kweli katika ngazi zote za kimtazamo ambazo tunaweza kuzitumia. Mtu anapoenda kupata huduma kwenye taasisi ya umma anatarajia kuwa atatendewa kwa haki. Hivyo anapoenda na kuomba fomu fulani za kujaza au kuulizia jambo fulani anatarajia kuwa fomu hizo zitapatikana bila mizengwe au majibu atapewa ya kumtosheleza.

Mtu huyo anapofika eneo hilo la kazi anakuta huo mfumo haufanyi kazi hivyo na badala yake akiwa anasubiri na kuona mtu mwingine ambaye anajulikana sana au ana ujiko fulani anapopewa kipaumbele na kuhudumiwa. Si kwa sababu alikuwa na miadi au kwa sababu nyingine yeyote bali kwa sababu mtu huyo mwingine ana mikono yenye kulainisha. Na hili ni kweli kwani kuna watu wengine hawajali kabisa utaratibu au mfumo uliopo; wao wanaenda kwenye maofisi akijua kabisa kuwa akifika pale atapenyeza rupia popote penye udhia. Haki inavunjwa.

Lakini katika kiwango kingine cha matokeo ya ufisadi ni pale ambapo usalama wa wananchi na wa nchi unakuwa matatani. Unapoenda Polisi unatarajia kupata huduma ya weledi yenye kuonesha kuwa polisi wanajali usalama wako na wanakujali wewe mwenyewe.

Lakini unapokutana na ukiritimba usio wa lazima na zaidi ya yote kama huduma wanayokupa haiendani na weledi wa jeshi la polisi basi unajikuta ni mhanga wa ufisadi. Hili linakuwa kweli zaidi kama inatokea kuwa ili upate huduma unayostahili inabidi upenyeze ‘kitu kidogo’ ili kulaainisha mikono ya watu.
Hata hivyo ufisadi una athari kubwa zaidi kwenye mifumo mikubwa ya nchi.Kwa nchi maskini kama ya kwetu ambayo ina wengi wanaotaka kuvuna kupitia migongo ya wengine ufisadi unajitokeza katika mfumo mzima wa utendaji wa serikali.

Imeshaandikwa mara nyingi kuhusiana na jinsi watendaji wanavyotaka kitu kidogo ili waidhinishe hatua fulani fulani au ili mikataba fulani iingiwe. Mtu anaposoma ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ushahidi wa hili uko wazi kabisa. Na taarifa zimesharudiwa mara kwa mara kuwa Tanzania inapoteza kati ya asilimia 20 hadi 30 ya fedha za bajeti kwa njia za ufisadi. Haya ni mabilioni ya shilingi ambayo yanapotea kila mwaka.

Hata hivyo, uthibitisho wa kutamalaki kwa utawala wa kifisadi unaonekana katika kumomonyoka kwa mfumo wa usalama (security system) ya nchi. Kuweza kuelewa hili mfano mmoja unatosha kuelezea. Mfugaji anajua kabisa kati ya majukumu yake mengi hakuna kubwa kama kuwalinda wanyama kutoka wanyama wakali kama simba, chui, mbwa mwitu n.k.

Hivyo, mfugaji ni lazima aweke ulinzi mzuri kuanzia wakati wa kuchunga, wapi pa kuchunga na kuhakikisha kuwa mifugo yake haiingii kwenye mtego wa wanyama wakali. Wanyama wanapopelekwa machungani jukumu la ulinzi linamuangukia mchungaji. Kwa waliowahi kufuga wanajua kuwa kabla wanyama hawajaondoka zizini mchungaji anahakikisha wote wamesalimika usiku na anapowarudisha jioni anafanya mahesabu tena; hii ni katika kujua kama wanyama wote wapo na wote wako salama.

Lakini jukumu kubwa kabisa la ulinzi linatokea zizini; je zizi liko imara kiasi gani?Je watu wanapolala wanyama wako salama kiasi gani?Sasa endapo watu wanaamka asubuhi na kukuta wanyama wamezagaa kila kona, damu imemwagika na wanyama wengi wamekufa na wengine wamechukuliwa jambo moja linakuwa wazi; mfumo wa ulinzi umefeli.

Yaani, mfumo wao ulikuwa ni kujiandaa dhidi ya wanyama wachache au mnyama mmoja kushambulia zizi na siyo kundi la wanyama wengi kushambulia. Na labda ni mfumo ambao haujafikiria kuwa watu wanaweza kuja kushambulia wanyama na kuiba. Mfugaji mwenye akili hawezi kurudi katika mfumo ule ule wa ulinzi ambao umethibitisha kushindwa!

Nimeandika mara nyingi sana mwaka huu na huko nyuma kuhusiana na kuvunjika kwa mfumo wa ulinzi na usalama na hasa ukosefu wa weledi, maono na uadilifu. Nimedokeza mara kadhaa kuwa viongozi wa sasa wa vyombo vyetu vya ulinzi hasa Polisi na Usalama wa Taifa pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani wameshindwa kulihakikishia taifa usalama.

Wameshindwa si kwa sababu nawasingizia bali ushahidi wote uliopo unadhihirisha hili. Wanaweza kupigiwa saluti, kupandishana vyeo na kuvishana nishani lakini kuhakikisha usalama wa nchi yetu hili wameshindwa.
Kuna matukio mengi sasa nchini na mengine hata ukiripoti watu hawashtuki tena! Nani kasikia juu ya tukio la polisi kutumiwa na mhalifu aliyetaka kubaka binti mmoja? Huyu binti na mwenzake na watu wengine wakamuweka chini ya ulinzi mhalifu huyo lakini kabla hawajajua mhalifu akawapigia polisi na polisi wakaja kumchukua kishkaji na kuwapiga mkwara walalamikaji? Ni matukio mangapi ya uporaji yanatokea sehemu mbalimbali nchini kila usiku?

Hakuna hata hivyo mfano mzuri wa kushindwa kwa mfumo huu wa usalama kama kuongezeka kwa matukio ya ushambuliaji, utekaji nyara na unyanyasaji wa wananchi unapokuja uchaguzi mdogo. Kwa miaka hii miwili na nusu tumeshuhudia matukio ya ajabu, ya kuudhi na kusikitisha ya wananchi kushambuliwa na siyo tu wananchi bali pia viongozi wao.

Na ambacho tumekiona na hili ni uthibitisho wa kushindwa kwa mfumo – ni jinsi gani mashabiki, wanachama na wapenzi wa CHADEMA ndio wamekutwa na mahanga hayo halafu wanalaumiwa wao wenyewe! Si tumeshuhudia tangu Kiteto? Tumeona haya Igunga, tumeona Songea, tumeona Tukuyu na tumeyaona Arusha tena si mara moja?

Cha kushangaza ni kuwa Rais Kikwete ana imani sana na vyombo vyake na ndio maana haachi kutoa maagizo kila linapotokea tukio kuwa polisi ati wawatafute na kuwatia mbaroni wahusika. Tukio hili la pili la Arusha ni ushahidi wa kushindwa kwa uongozi wa Said Mwema kwenye jeshi la polisi na ni uthibitisho kuwa Mkuu wa Operesheni wa Jeshi hilo ameshindwa kutoa uongozi na uelekezi wa jinsi jeshi linatakiwa kufanya kazi katika ulimwengu wa demokrasia ya vyama vingi.

Tukio la Arusha limejaa kila aina ya ushahidi kuwa jeshi letu limekuwa ‘compromised’ kiasi kwamba kuliacha lilivyo ni janga la usalama kwa nchi yetu.

Tayari tumeshaona fikra zinazoliongoza jeshi hili; kama Kamuhanda pamoja na tukio lile la Iringa anapandishwa cheo na kuletwa makao makuu ni wazi kuwa hata wa Arusha wanahitaji kupandishwa vyeo na hata Said Mwema mwenyewe anastahili kupewa tuzo nyingine au nishani nyingine. Ushauri wangu ni kuwa Kikwete awape nishani zaidi na vyeo zaidi na mafao zaidi watendaji wake wa usalama maana inaonekana ana imani nao sana!

Vinginevyo, Watanzania tukubali ukweli ulio wazi, ufisadi umeligharimu taifa sana. Siyo katika masuala ya uchumi tu bali zaidi katika mfumo wa utawala wa Sheria na Taratibu. Tukishakubali hili ni wajibu wetu kuanza kufikiria ni nani ataweza kuufumua mfumo huu na kuunda upya.Maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa “ufisadi ni adui mkubwa zaidi wa usalama wa nchi wakati wa amani kuliko vita” ni ya kweli. Nyerere alielewa kile ambacho inaonekana watawala wetu wa leo wameshindwa kukielewa – ufisadi (corruption) unapoachwa kutamalaki ina matokeo makubwa na hasi kwa taifa na usalama wa taifa.

Vinginevyo, Watanzania tukubali ukweli ulio wazi, ufisadi umeligharimu taifa sana. Siyo katika masuala ya uchumi tu bali zaidi katika mfumo wa utawala wa Sheria na Taratibu. Tukishakubali hili ni wajibu wetu kuanza kufikiria ni nani ataweza kuufumua mfumo huu na kuunda upya.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/kuvunjika-kwa-mfumo-wa-usalama-dalili-kuu-ya-kutamalaki-ufisadi#sthash.GZshHlqk.dpuf

No comments: