Thursday, May 2, 2013

WARAKA WA LADY JAYDEE NA USHAURI NA MTAZAMO WANGU
Dada Lady Jay Dee kayatoa yaliyomo katika moyo wake. Sote kama binadamu yaweza tokea watu wakawa wamekwazana katika upande mmoja ama mwingine. Huu sio wakati wa kuegemea upande fulani na kuacha upande fulani wakati ukweli uko mahali fulani umejificha. Nadhani muda tu ndio utakaobashiri nani alikuwa mkweli na nani alikuwa sio mkweli. Mimi sio mwandishi wa show biznes. Ila natambua katika Show biznes kuna changamoto nyingi sio ndogo. Ila kubwa ni kwenye upande wa maslahi. Sote tu mashahidi ugomvi wa Hayati Michael Jackson na aliyekuwa bosi wake wa kampuni ya SONY Tommy Motola ulivyopamba moto na matokeo yake tumeyaona.

Huu si wakati wa vita vya maneno ama malumbano. Ni wakati wa kujua ni wapi tulipoteleza/nilipoteleza ili niweze kusonga mbele. Dhuluma, fitina , ubinafsi ni moja kati ya haiba za binadamu. Watu ni wabinafsi, hata mimi ni mbinafsi lakini hiyo hainipi haki ya kumhukumu mtu mwingine na haimpi mtu mwingine haki ya kumuonea mwingine kutokana na hali yake. Yapo mengi yamejificha chini ya kapeti. Na sio vizuri watu wakapata faida. Lady Jay Dee na CLOUDS FM tafuteni muafaka nyinyi ni vioo vya jamii na watanzania wanawaangalia. Hatutaki kujenga jamii yenye makundi yaliyo na uhasama tunataka kujenga jamii yenye umoja na upendo. Pesa sio kila kitu bali ubinadamu na utu pamoja na kuheshimiana.

Mwisho nawatakia , na natoa rai ya mapatano baina ya pande hizo mbili ili maisha yaendelee kama yalivyo. Lakini pia naomba Dada Lady Jay Dee azizingatie hizi comments/ kutoka katika blogu yake kwa mapana na hali chanya , nimeamua kuziweka hapa kwa maana kuu moja wapo wale ambao watabeza mafanikio yako, wapo wale watakaopendezwa na mafanikio yako (huwezi kuwajua) na wapo wanafiki (huwezi kuwajua), wapo watu na viatu (huwezi kuwajua), wapo watakaochukua changamoto zako kama njia ya kujinufaisha. KUWA MACHO.


-Baraka Mfunguo

HIZI NI COMMENTS CHACHE ZA KUZINGATIA  AMBAZO NIMEZITOA KWENYE BLOGU YA LADY JAYDEE.Anonymous said...

Lady Jay Dee (Judith), kisasi si kitu cha kuvaa moyoni. Nimeona wengi hapa wamekusifia kwa ujasiri lakini sijauona ujasiri huo. Ni kweli kuwa kuna wakati ulifurahia 'favor' za hao jamaa na bila kituo chao cha radio usingefika hapo ulipo, hilo ulipaswa kulisemea na kulitolea shukrani pia. Si nia yangu kusema kuwa clouds ni watu wema au wabaya, ila yawezekana kabisa mlikuwa marafiki na ikafika hatua urafiki ukavunjika. Kama wanakataza wasanii kuungana na wewe, nadhani hapo ni juu ya wasanii hao waliokatazwa kuamua ama kukubaliana nao au kuungana na wewe. Lugha ya usije kwenye msiba wangu huwa ni ya mzazi aliyekataliwa na mtoto, na sio ya mtoto aliyekataliwa na mzazi. Ni wazi kuwa mpaka unaandika hapa, ni kwamba kuna sehemu wakubana hadi imekuuma ndipo ukaja na wosia wako. Ulihitaji nasaha, za mtu mwungwana, mcha - Mungu. Huwezi toa lugha ya kisasi kisha ukasema tuone Mungu ni nani na binadamu ni nani. Mungu anajua unawaza nini hata kabla hujasema. Ulichopaswa kufanya ni kutafuta namna ya kuwasilisha ujumbe wako kwa wahusika bila kuchafua taswira yao kijamii. Dunia mzunguko, mnaweza kupatana siku moja kisha ukaja na wosia mpya hapa.
HILI JOTO HASIRA...............

May 1, 2013 at 4:08 PM


Anonymous said...

Mimi kiukweli niko upande wako Dada Jay Dee na ni mdau wako mkubwa tu, naukubali mziki wako na kazi zako pia. Najua wewe ni mkristo kitendo ulichofanya si cha kiimani kama ulivyosema Mungu ndo mpaji na muandaaji wa kila kitu chetu si vyema ukampangia Mungu adhabu ya kuwapa hao wabaya wako. KAULI NI NZITO SANA, Mungu anamipango yake siku zote, mimi napenda nikwambie tu kuwa bora ufute kauli hiyo kwani kwa tamaduni zetu hilo ni kosa hata kiimani pia. swali: jE! WABAYA ZAKO WAKIOMBA MSAMAHA KWA MUNGU WAO, WEWE UTAKUWA KATIKA FUNGU GANI? Hiyo ni kama kufuru. biblia inasema samehe 7 * 70 yatupasa tumwachie Mungu yeye ndo muamuzi wa yote! Ni mawazo yangu tu!


May 1, 2013 at 4:21 PM


Anonymous said...

unapapatika kama kuku aliyekatwa shingo, unachokifanya ni mchezo mchafu, kwa kuwachafua watu ili kuipigia promo show yako, ww na mume wako Gadna wote hamtumii comon sense inabidi mjipange, unafikiri tumesahau wasanii walioondoka kwenye bendi yako walichokua wanasema? ulikua ukiwanyanyasa na ujira wao ulikua mdogo na baada ya kazi huwapi, mpaka wengine wakakimbilia SKY LIGHT BAND, kila siku unawatukana watoto wa kiume utafkr umewazaa ww, nani asiyekujua LADY JAY DEE kwa kuvimba? dunia ndo inakupiga sasa, ww umepata stress baada ya kukimbiwa na wasanii, wenzako wanatafuta maslahi hapa town hawajaja kuuza sura, au kukushobokea wewe kwasababi Star, Salary ndo mpango mzima, ni mara ngapi umeanzisha ugomvi mbele ya wateja pale nyumbani lounge? Wateja wamekimbia pia kwasababu huduma zinazotolewa ni hafifu hazilingani na pesa wanayotoa, face changamoto zako na si kuchafua watu, unawasema watu JE USHAHIDI UKO WAPI? hzo big up za twitter na facebook ndo zinakupa kichwa? wao wenyewe hawajielewi wadananda tu, Ulipewa promo la nguvu miaka kibao, tena mume wako ndo alikua anapiga links mwenyewe kwenye jahazi na top 20, hakuna msanii wa kike aliyepata promo zaidi yako, kwani kina Stara Thomas walikua hawawezi? lakin ulibebwa ww, wao sasa ndo walalamike, cha muhimu Bi dada badilisha Life Style la sivyo utakufa kwa msongo wa mawazo, kama si ajali ya gari basi unaweza hata kujiua, au presha


May 1, 2013 at 4:27 PM   WARAKA/WOSIA WA DADA  LADY JAY DEE

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa. Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria. Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia. Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao. Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu. Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge. Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia.. Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??. Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili. Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri. Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu. Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE

No comments: