Saturday, May 25, 2013

SIASA ZA MTWARA, SIASA ZA TANZANIA................


Uchafu wa Waziri Ghasia na dharau zake kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kifua cha JK(Habari hii haijathibitishwa rasmi) Na EX SPY,
Kwa kawaida ofisi ya Waziri Mkuu ndio yenye dhamana na mamlaka ya Serikali za Mitaa chini ya Waziri Mkuu mwenyewe. Lakini hali sasa sivyo kwa Mhe. Hawa Ghasia kujiamulia atakayo kinyume cha maelekezo ya Waziri Mkuu huku akitamba kuwa karibu sana na Rais na Mke wa Rais na mtoto wa Rais.

Hawa huyuhuyu ndiye anayenuka kwenye ufisadi wa korosho Mtwara kwa makampuni yake kusambaza pembejeo dhaifu, chache na nje ya muda huku ikilipwa mabilioni ya pesa za wakulima.

Ni Hawa huyuhuyu ambaye alipata kashfa ya kujipatia takriban dola milioni 3 toka kwa moja ya makampuni ya mafuta na kashfa hii TAKUKURU waliizima kwa kuogopa nyumba kubwa ambayo anatamba inamlinda.

Ni Hawa huyuhuyu kwa miaka yake nane ya Uwaziri amenunua nyumba lukuki Mtwara ambazo nyingine amegeuza hostel, kupangisha, kuishi mwenyewe na nyingine kuziacha tu, ndio maana katika vurugu zote nyumba zake ndio za kwanza kuchomwa.

Hawa kwa kipindi kifupi amekuwa akitengeneza mitandao ya wizi kwenye Halmashauri akishirikiana na mumewe ambaye amekuwa mwekahazina wa muda kwenye Halmashauri na alimalizia Manispaa ya Temeke kabla ya kupelekwa ubalozini India aliko mpaka sasa.

Amekuwa akiwahamisha, kuwasimamisha na kuwatisha wakurugenzi wote wanaombania kutimiza matakwa yake ya wizi.

Hawa amekuwa akilinda watumishi wezi wanaomsaidia kwenye mambo yake ya wizi, inasemekana anatumika na kambi moja ya urais inayoongoza kwa matumizi ya fedha kuwakusanyia fedha kwa mipango yao ya kuingia Ikulu 2015 kitendo ambacho wapo wanaohisi JK ameshtuka na wapo wanaohisi bado hasa ikizingatiwa kuwa Ghasia amesikika kwenye moja ya mikutano yake jimboni Mtwara akibeza jitihada za mama Salma kutwaa jimbo la Lindi mjini.

Mfano, mwekahazina Kabilinge Stima ambaye amehamishiwa Ilala toka Mvomero alikokula shilingi bilioni 1.3 na Baraza la Madiwani kutaka arudishwe kujibu tuhuma bado Waziri amemkingia kifua. Baada ya moto kuzidi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, aliunda Tume ambayo kumbukumbu zinaonyesha Ghasia na Waziri mwingine mmoja kupiga simu lukuki kukwamisha zoezi hilo. Baada ya tume kuwasilisha taarifa ya siri kwa Mkuu wa Mkoa ambayo Stima anayo kabla hata ya Mkuu wa Mkoa, imeelekeza achukuliwe hatua lakini mpaka leo kimya.

Katibu mkuu wa CCM A. Kianana na Katibu wa Siasa na uenezi Nape Nnauye kwenye ziara yao ya mkoa wa Morogoro walielezwa upotevu wa fedha hizo za miradi nao wakatoa maagizo ya kisiasa ambayo mpaka leo hayajatekelezwa. Aidha, yawezekana Stima amewahonga; maana anasifika kwa kuhonga hela nyingi, akitumia utajiri wa kutisha aloupata kwenye Halmashauri za Moshi, Geita na Mvomero na anamiliki Hotel mbili za ghorofa 6 maeneo ya Sinza na Kijitonyama au Kinana amemwogopa Ghasia kupitia kwa JK.

Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Bw. Kidaka amemwandikia Stima barua ya kurudi Mvomero na akaishia kutukanwa matusi ya nguoni na ndugu Hawa Ghasia, kitendo ambacho kilimfanya asuse ziara ya Kampala alokuwa aende na Waziri Ghasia.

Huko Ilala alikohamia Stima, kwa kushirikiana na Ghasia amekwamisha mradi wa kukusanya mapato kupitia Benki kitendo ambacho kingekwamisha wizi wao kwenye Halmashauri hiyo tajiri kuliko zote.

Baada ya kuona Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo hakubali kushiriki wizi, Ghasia kwa kumtumia swahiba wake kwenye kambi ya urais kuandika barua kumtuhumu mkurugenzi na Meya kwa ubadhirifu na kupelekea Waziri Ghasia kumpumzisha Mkurugenzi Gabriel Fuime 24/1/2013 kinyume na kanuni za Utumishi na maagizo ya Waziri Mkuu kwa barua yake ya 7/12/2013. Mpaka sasa inakaribia miezi 6 kwa taratibu za utumishi wa umma Fuime yuko nyumbani akitumia kodi za umma bila mashtaka yoyote.

Stima anasifika kuwa karibu na kila kiongozi wa kamati ya bunge ya LAAC kwa kuwahonga pesa nyingi sana. Inasemekana hata Dr. Slaa akiwa mkiti wa LAAC alikuwa karibu sana na Stima anayejiita 'Rais wa waweka hazina wote nchini' na ndiye aliyekuwa anamkusanyia Dr. Slaa migawo yake. Stima alifikia kufadhili harusi ya moja wa kada wa CHADEMA aliyefahamika kwa jina moja tu la Mrema kwenye hoteli yake kwa heshma ya Dk.Slaa (najua wengi hamtaamini ninachoeleza hapa, subiri karibuni mtaelewa na kwakuwa wote hawa ni members wa JF, waje wapinge tutashuka na viambatanisho ambavyo vimeshasambazwa kwa vyombo kadhaa vya habari).

Hawa Ghasia anatajwa kuhusika na maelekezo ya kuvunja mkataba wa uendelezaji wa kiwanja na. 288 Toure Drive baina ya Halmashauri ya Jiji na mwekezaji Silverstine kinyume na utaratibu, ili ampe kiwanja hicho mali ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam mfanyabiashara wa Kiasia aliyempa rushwa za wazi wazi. Mfanyabiashara huyo anadai alitoa kiwanja anachoishi Rais mstaafu Mzee Mwinyi Mikocheni chenye ukubwa wa mita za mraba 1,900 na akapewa kiwanja cha mita za mraba 900 Msasani na hivyo anataka aongezwe hiki 288 chenye mita za mraba 3800. Ukweli ni kwamba alipewa kiwanja chole rd cha mita za mraba 1,800 na amemwuzia mfanyabiashara Mohamed Dewji.

Baada ya Swahiba yake Ghasia Dr. Masaburi ambaye ameuza UDA kitapeli na madiwani wake kushiba hela za mhindi wakaazimia kwenye baraza la madiwani kuvunja mkataba huo. Mkurugenzi Mussa Singiza aliyehamia Dar mwaka jana kumshauri waziri kufata taratibu za sheria amehamishiwa Jiji la Mbeya kupisha wakubwa wafanye yao.

Hivi tunavyozungumza wakurugenzi nchini wamemwomba Waziri Mkuu wakutane naye faragha kumteta Ghasia na wako waloapa wakisimamia uchaguzi 2015 wataiangusha CCM.

Wiki mbili zilizopita, kwenye kipindi cha jahazi cha Clouds FM, alisikika Meya wa Halmashauri hiyo Jerry Silaa akifoka kuingiliwa na TAMISEMI kinyume cha sheria namba 8 ya 1982 ya mamlaka za miji hasa kwenye eneo la ukusanyaji wa mapato kwa kukwamisha utumiaji wa benki ya NMB ambayo kwenye mkutano wa Arusha walimsifu Meya Silaa kwa kubuni mfumo huu lakini wakaogopa kusema haujaanza licha ya mikataba kusainiwa.

Ghasia anamtuhumu Meya Silaa kumiliki makampuni 6 yanayofanya kazi ndani ya Halmashauri na amemlisha maneno Mh. Pinda na amesikika akisema hadharani. Viongozi hawa wawili hawazungumzii umiliki huo unapingana vipi na sheria na.4 ya 1979, na.8,9,10 za 1982. Vilevile hawaelezi kampuni hizo kama zilifata utaratibu wa kupata zabuni na hawaelezi utendaji wake wa kazi walizopewa.

Maneno ya kampuni ndio yanatumika kuziba midomo viongozi wengi wanaopingana na Ghasia na hivi karibuni Mh. Kigwangwalla ameshughulikiwa kwa staili hiyo hiyo. Tofauti yao ya Kigwangwala imeonyesha wana hisa na majina ya wamiliki.

Edward Hosea ameshindwa kumchukulia hatua Stima kwa maagizo ya Mkuchika ambaye wako karibu sana na Ghasia.

Hii ni part 1, tutaendelea kutoa ufafanuzi zaidi kadiri muda utakavyoruhusu
CHANZO: JAMII FORUMS

2 comments:

Chinang'o mwiro said...

Ndugu mwanablog Mwenzangu, napenda sana kukusihi kutoshiriki katika ushabiki wa kisiasa kwani mara kadhaa blog za aina hii huishia kuwa za mtu binafsi na ndio maana hupati michango ya maoni humu ndani.

Mimi binafsi nashukuru kwamba ni msomaji niliyepevuka na mwelewa wa siasa za africa na Tanzania pia dunia. Najua kwa kiasi gani watu wanaweza kukutumia kumuandika mtu, but jua ikitokea watu wakajua kwamba habari zako ni tetesi tu na hazina ushahidi jua kwamba unatufanya tupuuze kuja hapa. Naomba usidhani kwamba watu wote hatuna upeo wa kutafakari mambo. so nakushauri jifunze kuandika habari za ukweli, nakumbuka Tanzania daima liliandika baadhi ya aneneo haya but hawakuweza kutoa uthibitisho wowote na hata waziri mkuu hakukubaliana na fikra zao.

so nakushauri kuwa makini na mkweli katika blog yako.

wabillahi tawfiq,
Mwenyezi Mungu akusamehe kwa makosa yako kwani wote sisi ni wakosaji.

Mtwara kwetu said...

HATA MIMI NIMESOMA HII HABARI NDUGU YANGU NIMEJIFUNZA KWAMBA WATU WA MTWARA HAWAJUI NI KWA KIASI GANI WENZAO WA KASKAZINI WANASHUKURU KUPATA MBUNGE AMBAYE ANAUZALENDO WA KUJENGA NA KUWEKEZA KWAO. KUMBUKA WATU KAMA KINA MSUYA NA SUMAYE AMBAO KWAO WANAPENDWA KWA KUFANYA MAMBO YA MAENDELEO. NINGESTUKA KAMA HAWA ANGEKUWA AMEDHULUMU HAYO MAJUMBA, BUT MUANDISHI KASEMA AMENUNUA NA WAUZAJI WAMEUZA WENYEWE. PIA AMA AMEFANYA HOSTEL NA HOTEL NA MENGINE ANGALAU AMECHANGIA KUTATUA MATATIZO YA KWAO. WENZENU TUNAWALALAMIKIA WATU WETU WALIOLOWEA DAR ES SALAAM NA KUJENGA HUKO.
NATAKA KUJUA HIVI NI KWELI KWAMBA TANGU MTWARA MJINI NA VIJIJINI ZIANZE HAZIJAWAHI KUTOA WAZIRI? NAHISI WATU HAMJAJUA KWA KIASI GANI KWAKUWA NA HUYO MAMA MMEWEZA KUITANGAZA MTWARA KWA KUWEZESHA CHUO CHA UTUMISHI NAKADHALIKA.

KWAKWELI NAWASHANGAENI WAMAKONDE MPOJE? AU WABUNGE WA KABLA YAKE WALIFANYA MAKUBWA SAANA KWAMBA YEYE HAJAYAFIKIA? IKIWA HIVYO NITAWASAPORT BUT KIUKWELI KAMA ANAWEKEZA KWAKE HIYO NI BIG UP. WAAMBIENI KINA MEMBE NA MKUCHIKA NA WENGINE WAIGE MFANO HUO.