Tuesday, May 21, 2013

NUKUU ZA LEO"Najua kuwa watu wa aina ya Rashid Kawawa ni adimu sana duniani, hawazaliwi kila siku; lakini hata hivyo ni jambo la kushangaza kidogo kwamba viongozi wetu wa mageuzi, hata bado hatujafa, wanaona kuwa ni kosa kuwakumbusha kuwa vyeo walivyo navyo ni dhamana. Wanadhani Uwaziri ni Usultani: Ukisha kuwa Sultani utakufa Sultani! Nadhani wamekosea. Nchi hii imewahi kuwang'oa Masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia Masultani wa kuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa."  


Nyerere, J.K (1994) UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA -uk 45


" Kwani mbona tumeona
Dhahabu imetoka Geita hawajafaidi,
Almasi imetoka Shinyanga hawajafaidi,
Tanzanite imetoka arusha hawajafaidi,
Chumvi inatoka uvinza hawajafaidi,
Tumbaku inatoka tabora hawajafaidi.
Hili la gesi munataka kuwadanganya wana mtwara kama ije Dar kwa manufaa ya taifa na wao watanufaika huo ni uongo.
Naungana na wanamtwara GESI ISITOKE"


DJANGO, JAMII FORUMS.

No comments: