Monday, May 27, 2013

NG'ANYA LA GESI LINAENDELEA

Kwa wale ambao walikuwa wanadhani hali ni shwari na mambo yanaenda sawa, watakuwa wanajidanganya. Ng'anya hili bado linaendelea na bado watu wananung'unika katika mioyo yao. Hatua inayoendelea sasa hivi ni mkakati wa kukusanya kadi zote za CCM na kuwarudishia wenyewe, huku mambo mengine yakiendelea. Tarehe 29/05/2013 ingawa taarifa sio rasmi kunaweza kukawa kusiwe na shughuli yoyote.

Wakati huo huo vifaru vya jeshi vimeripotiwa kuwasili leo mchana, na maiti ya kijana wa kiume ikiwa imetobolewa utumbo na polisi imewasili Ligula. Hili sio jambo la kushabikia kwa hatua iliyofikia hili ni suala la maisha na kifo.
 Watuhumiwa wa vurugu (wengi wao vibarua wa ujenzi wa bara bara na wanafunzi wa vyuo pamoja na vijana wa mtaani) wamefikishwa mahakamani kwa shitaka la uchochezi na wamenyimwa dhamana. Wamerudi rumande mpaka kesi yao itakapotajwa tena.
 Serikali inachukulia hili swala kama mzaha mzaha lakini matokeo yake yatakuwa mabaya sana.
Tutazidi kujuzana kila kinachoendelea....... GESI HAITOKI

No comments: