Thursday, May 23, 2013

MTWARA : GESI GESI WAR UPDATE

 •  Mizinga baridi ipatayo sita yapigwa kuwatia joto wananchi majira ya saa nne na nusu usiku (UPDATE IJUMAA)
 •  Mjadala wa mama mjamzito aliyeuawa kwa kupigwa risasi waibuka baina ya Polisi na Waganga walioufanyia uchunguzi. Polisi wanataka kuupotosha umma. Polisi wanadai hajafa kwa kupigwa risasi mpaka waione risasi, madaktari wanasema ameuawa kwa risasi kwani  vipimo vya X-Ray na vipimo vingine vya uchunguzi wa kitabibu vinasema hivyo. Hatua hiyo imesababisha taratibu zote za maziko za mama huyo zisimame kwa muda.(UPDATE IJUMAA)
 •  Jengo la Marine Park- Msimbati lateketezwa .(UPDATE IJUMAA)
 •  Majeruhi wawili waliopigwa risasi miguuni wawasili Hospitali ya Mkoa wakitokea Zahanati ya Imekua. Walipigwa risasi tarehe 23/05/2013 siku ya alhamis. (UPDATE-IJUMAA)
 • Waziri Mkuu kuwasili muda wowote kuanzia tarehe 24/05/2013 Ijumaa. Atakutana pia na wadau wa habari maeneo ya mkoani siku ya Ijumaa.
 • Hali ya mji yarejea kwenye utulivu.
 •  Msimbati nako kuna vurugu
 • Dege kubwa la jeshi latua Mtwara.
 • Waziri wa Mambo ya Ndani,Waziri wa Ulinzi na viongozi waandamizi wizara ya Mambo ya ndani wawasili chini ya ulinzi wa FFU na Jeshi.
 • Kuna madai ambayo hayajathibitishwa kwamba wanawake wanabakwa na maaskari, wanapigwa risasi kutokana na vijana wote kukimbia maporini.
 • Mwanamke anayekadiriwa miaka 25 mjamzito auawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.
 •  Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali  Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
 • Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.
 • Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
 • Mabomu yanaendelea kupigwa tofauti kwa sasa hayapigw mfululizo.
 •  Mabomu yametulia. Hali ya ukimya imetawala.
 • Mabasi 5 ya Champion yamebeba Wanajeshi yako njiani yanakuja.
 •  Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
 • Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
 •  Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani  maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao.  Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
 • RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
 • Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
 • Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
 • Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.
 • Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.
 • Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.

 • Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote
Barabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita.  

MTWARA LEO
PICHA NA FARID HEMED
 SHUJAA WA GESI ALIYEPIGWA RISASI 
 RIP Kaka Karim(Picha Mpasta, JAMII FORUMS)

No comments: