Monday, May 13, 2013

MKAKATI WA UJENZI WA BOMBA LA GESI KUTOKA MTWARA KWENDA DAR

Kufuatia sintofahamu ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar hoja inayosimamiwa na serikali huku wananchi wakidai gesi haitoki mpaka iwafaidishe wao, na kupelekea uvunjifu wa amani Serikali imekuja na mkakati mpya. Zifuatazo ni baadhi ya dondoo ambazo Serikali imejipanga kwa ajili ya kuhakikisha ujenzi wa bomba la gesi unaendelea "by all means necessary"


  • Kamanda wa Polisi wa mkoa kuondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kamanda mwingine
  • Kamanda mpya kutumia mkakati wa kuonana na kila kundi kujadiliana nao na kupata muafaka wa ushirikiano na utii wa sheria bila shuruti pindi mradi huo utakapoanza. Mathalan wafanyabiashara, viongozi wa dini, viongozi wa asasi za kisiasa, viongozi wa serikali n.k
  • Kuongezeka kwa Kamishna mwingine wa Polisi atakayekuwa akisimamia operesheni ya ujenzi wa bomba la gesi kwa kuhakikisha usalama wa wanaojenga. Hii ina maana kwamba kutakuwa na kikosi maalum kinachojitegemea chini ya usimamizi wa kamanda mwenye jukumu hilo nje ya polisi wa kawaida. Huu ni mkakati kama ule wa kule Tarime.
  • Askari maalum, wakiwamo Makomandoo wa kikosi cha JWTZ kuwasili tayari kwa kazi hiyo
  • Makachero kadhaa wa vikosi vyote vya usalama wapo tayari kwa ajili ya zoezi la kutathmini athari zozote za kiusalama wakati zoezi la ujenzi wa gesi likiendelea.
  • Serikali kutenga kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya operesheni hiyo.
  • Hii ina maana kwamba nguvu kubwa itatumika na endapo kutakuwa na pingamizi kutoka kwa wananchi maafa, ikiwamo vifo, upotevu wa mali vitatokea.
  • Zoezi la mafunzo juu ya gesi kwa wadau mbalimbali  mkoani Mtwara linaendelea kwa ufadhili wa serikali. Nia na madhumuni ni kujitoa lawama endapo maafa yatajitokeza. 

No comments: