Monday, May 20, 2013

HUDUMA KUSIMAMA TENA MTWARA SIKU YA JUMATANO TAREHE 22/05/2013- ALERT

 Update:
Huduma zitasimama kwa siku mbili mfululizo. Jumatano na Alhamisi
Waziri Mkuu kuwasili tarehe 24 na atakuwepo mpaka tarehe 26.
Tarehe 24 na 25 uzinduzi wa viwanda Slumberger na Dangote.
Tarehe 26 kushiriki katika kuwekwa wakfu kwa Askofu wa K.K.K.T la Mtwara.

Maafisa Usalama wametanda wengi wao wakiwa wamepaki magari yenye namba binafsi barabarani. (Magari usiyoyadhania). Wengine wakiwa kwenye maeneo mbalimbali. 

Siku ya Jumatano huduma zitasimama tena ili kusikiliza bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo huduma za mabasi yaendayo mikoani na Dar es Salaam nazo zitasimama. Kikubwa ni wananchi kutaka kujua mustakabali wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar na Msimamo wa Serikali ni upi.

No comments: