Thursday, May 16, 2013

HOFU TENA MTWARANa Baraka Mfunguo,
Hali ya hofu imetanda  tena maeneo ya Manispaa ya Mtwara Mikindani baada ya kusambazwa kwa vipeperushi vyenye ujumbe wa kuwataka watu kutofanya shughuli zao siku ya Ijumaa ambapo Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itakaposomwa Bungeni. 

Dondoo muhimu katika vipeperushi hivyo


 • Huduma za vyakula sokoni zitafungwa
 • Huduma za Usafiri kama vile bodaboda , Bajaji na Hiace zisimame
 • Maduka yote yafungwe
 • Ofisi zote zikiwamo za serikali na zisizokuwa za serikali zifungwe.
 • Shughuli zote zisimame mpaka bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini isomwe na mbivu ijulikane na mbichi ijulikane. Hatma ipatikane ya nini kifanyike.
Hii inatokana na sintofahamu pamoja na ahadi ya serikali kujenga kiwanda cha kuchakata gesi ndipo gesi ingine itolewe kwa matumizi na kuanza kubaini ahadi hizo hazikuwa za kweli na kuanza kuamsha hisia miongoni mwao. Hali hii ikiendelea itasababisha maafa makubwa na hasara kubwa.
Baadhi ya wadadisi wanasema
Wananchi wamejiandaa kwa silaha za jadi, mabomu ya samaki na kuwa na mitandao mingine mikubwa.
  
Nini kinasababisha?
 Kubwa linalosababisha ni kiwango cha walionacho na wasionacho kuongezeka
 • Ukosefu wa ajira.
 • Umasikini 
 • Kudorora kwa Elimu.
 • Hali ya kisiasa mkoani Mtwara.
 • Zao la Korosho. 
 • Ahadi na ngonjera zisizotekelezeka za CCM na watu wake.
 • Gesi ni rasilimali ya pekee baada ya Korosho na wananchi wamesema hawakubali gesi yao itoke hivi hivi bila ya kuwafaidisha wao. Kuwepo na " Economic Profit" itakayofaidisha pande zote badala ya "Accounting Profit" itakayoifaidisha Serikali. 
 • Kushuka kwa maadili ya Utumishi wa umma
 • Maeneo mengi yenye rasilimali hayapewi vipaumbele na wanaofaidika sio wenyeji wa maeneo yale. Mfano Geita, Mwadui na maeneo mengine ambayo yamebakia mashimo na wananchi wake kubakia na umaskini mara mbili hata kabla ya madini kuchimbwa.
 • Watumishi wa Serikali ambao wanajulikana kwa ufisadi lakini serikali haijawachukulia hatua.
Maeneo ambayo ni target 
 • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
 • Ikulu ya Serikali
 • Ofisi zote za Serikali
 • Vituo vya Polisi
 • Eneo la ujenzi wa Bomba la gesi
 • Hospitali ya mkoa
 • Ofisi zote za chama Tawala pamoja na viongozi wake
 • Wale wote wanaoshabikia ujenzi wa bomba la gesi liende Dar
 • Mtu yeyote atakayeonekana kama ni msaliti kwenye nia "cause".
 • Nyumba za Wabunge wanaoshabikia bomba la gesi liende Dar.
 • Maeneo yenye miundombinu muhimu mf Daraja la Mtambaswala na Daraja la Mkapa(Update)
Kufuatia hali hiyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa  ,akiongea katika kituo cha PRIDE FM cha Mtwara amewatoa hofu wananchi na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida kwani wao kama Jeshi wamejipanga kuhakikisha usalama wa wananchi unakuwepo na amani inadumishwa.

Endapo serikali itayapuuza madai ya watu wa Mtwara, madhara ambayo yatajitokeza yatakuwa ni mabaya zaidi kwa kipindi kirefu na yatakuwa ni doa lingine katika historia ya Tanzania ukiacha ile ya Udini. Serikali inatakiwa iyazingatie madai ya watu wa Mtwara pamoja na wananchi wote ili pato la  taifa litolewe kwa usawa na liwe na tija. Isiwe tafsiri ya pato la taifa linatumika kuwafaidisha viongozi. Serikali iwe na vipaumbele vyenye manufaa kwa wananchi sio mashangingi na kujilundikia mishahara mikubwa na uheshimiwa kwani mwisho wa siku wote tutamezwa na ardhi ya dunia. 


Update:
 RPC Mtwara: ''Wananchi kaeni mkijua ya kwamba hizo vurugu mnazozipanga kesho sisi tumejipanga vilivyo''
 Kupitia safari redio mtwara,RPC huyo alisikika akitoa tahadhari kwa wananchi wenye hasira kali dhidi ya mustakabali wa suala la gesi na nia ya serikali kwa maeendeleo ya watu wa kusini,

Licha ya serikali kutumia gharama nyingi kuendesha kipindi cha BARAGUMU LA MSIMBATI kupitia kituo chake cha habari cha TBCCM ambacho katika kipindi hiki ni kama nyenzo ya kutoa elimu kwa wananchi wa tanzania hususani KUSINI wananchi hao wameonekana kutoelewa na kutokubaliana moja kwa moja na serikali....

Wananchi manispaa ya Mtwara Mikindani wameaswa kununua mahitaji yao ya umuhim na kuweka ndani kwa siku ya leo kwani kwa siku ya kesho huduma za kijamii zitasimama ama zisipatikane moja kwa moja,kuna uwezekano mkubwa wa maduka mbali mbali ya vyakula,masoko,usafiri wa umma kama dala dala,boda boda na bajaji zikasitisha huduma kutokana na TAMKO la wanaharakati na wakereketwa wa gesi na mustakabali wa mtwara na kusini ya kwamba huduma hizo kesho zisimame na watu wawe macho kufuatilia mjadala wa hotuba ya waziri wa nishati na madini BUNGENI na iwapo hawataona la maana kwenye hotuba hiyo basi wataamua lao la kufanya...

Wanamshangaa RPC kukimbilia SAFARI RADIO kutoa tamko hilo kwani wao hawajapanga kufanya vurugu za aina yoyote zaid ya kuonesha tuh passive resistance...

Wanasema kwa kuwa serikali ya CCM imeamua kutumia ubabe basi na wao wataonesha ya upande wao kwa MASLAHI YA VIZAZI VYAO VIJAVYO...


JAMII FORUMS 

 KIPEPERUSHI CHENYE UJUMBE


 

No comments: