Wednesday, May 15, 2013

BABA ASKOFU NORBERT MTEGA ASTAAFU

Baba Askofu Norbert Wendalin Mtega amestaafu wadhifa wake kutokana na sababu za kiafya hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Maaskofu-TEC  iliyotolewa leo saa saba na robo mchana. Baba Mtega atakumbukwa kwa ubunifu wake wa kuleta maendeleo katika Jimbo lake na mikoa ya Kusini kwa ujumla. Kimsingi Baba Mtega alikuwa mchapa kazi mzuri na hodari katika weledi, utaalam kwa masuala mbalimbali ya uongozi ndani na nje ya Jimbo lake.Moja ya mafanikio yake ni kuwezesha kuanzishwa kwa matawi ya Chuo cha St. Augustine -Mtwara na Ruvuma. Blogu hii inamtakia mapumziko mema na asisite kusaidia jamii ya Watanzania bila kujali rangi, itikadi ama dini pale atakapo hitajika.

No comments: