Thursday, April 4, 2013

TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIAJUKWAA LA WA WAKRISTO TANZANIA (TCF)

 “ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI, NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA” (Lk.2:14)

TAMKO LA PAMOJA LA MKUTANO MKUU WA DHARURA WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA
   
1.Utangulizi    

Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) linajumuisha Taasisi Kuu za Makanisa nchini kama ifuatavyo:- Jumuiya ya Kikristo Tanzania – CCT Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania – TEC Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania – PCT Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA (Watazamaji) Katika Mkutano wake Mkuu wa Dharura uliofanyika katika Kituo cha Mikutano na Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini, Jijini Dar es Salaam, tarehe 8 Machi, 2013;   Wajumbe walitafakari kwa undani juu ya kuzorota kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini Tanzania, pamoja na mauaji na mashambulizi ya viongozi wa dini; na hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya uhalifu huo unaotekelezwa na Waislamu wachache.    

Katika taswira hiyo, Kanisa lilitathmini juu ya wajibu, utume, na sauti yake ya kinabii kwa taifa letu kuhusiana na mambo hayo.    

2. Hali halisi ilivyo hivi sasa hapa nchini kwa mtazamo wa Kanisa Ushahidi wa kihistoria na kimazingira unaonyesha wazi kuwa kwa sasa Kanisa nchini Tanzania limo katika kipindi cha mateso ya kimfumo (systematic persecution), kama vipindi vingine 10 vya mateso katika Historia ya Kanisa hapa duniani. Pamoja na mateso haya ya kimfumo, tunatambua wazi kuwa wanaotekeleza haya ni kikundi kidogo tu cha Waislamu wa Tanzania, kama wale wengine wa Barani Afrika (k.m. Boko Haram kule Nigeria).   Waislamu walio wengi hawafurahii mambo yanayotokea. Wao pia wanaitazamia Serikali kuthibiti hawa wachache wanaochafua dini ya Kiislamu na kuwafanya Waislamu wote waonekane kuwa maadui wa Ukristo, jambo ambalo siyo kweli. Kutokana na hali hiyo, mkutano mkuu wa dharura wa Jukwaa la Wakristo umeyaangalia maeneo makuu yenye migogoro ikiwa ni pamoja na:  

 2.1. Mgororo wa nani anastahili kuchinja kitoweo Hivi karibuni hapa nchini tumeshuhuduia mgogoro juu ya uchinjaji wa mifugo ambayo nyama yake inapaswa kuuzwa kwa watu wa imani mbalimbali wakiwemo Wakristo na Waislamu. Tunafahamu kwamba sheria ya nchi yetu inaweka bayana juu ya usalama wa nyama hizo kiafya, lakini sheria haielekezi kuwa dini fulani ndiyo waumini wake wanapaswa kuchinja mifugo hiyo.    

Kwa misingi hiyo Kanisa linatamka kuwa:-    

a) Hoja ya dini moja kudai kuhodhi (exclusive right) uchinjaji wa mifugo kwa misingi ya imani yake ni kinyume cha haki ya uhuru wa kuabudu ambayo amepewa kila mtu ndani ya nchi hii kikatiba katika Ibara 19.  

 b) Kwa kuwa kuchinja wanyama na ndege ni Ibada kwa Waislamu, Kanisa litambue na kuheshimu jambo hilo.   Lakini pamoja na kutambua haki ya Waislamu kujichinjia wanyama na ndege kama Ibada kwao, Wakristo wasilazimishwe kula nyama zilizochinjwa kwa misingi ya Ibada za Kiislamu.   Kwa kuwa wananchi wa Tanzania ni wa dini mbalimbali na mila za makabila mbalimbali, tunaitaka Serikali itamke wazi kuwa kila raia ana uhuru wa kufuata imani yake katika suala la uchinjaji.    

c) Kuhusiana na jambo hili tunashindwa kabisa kuelewa msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali.   Wakati wa Serikali ya awamu ya pili chini ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Muislamu, ulipotokea ugomvi wa mabucha ya nyama ya nguruwe Dar es Salaam, Rais huyu Mstaafu kwa kulinda Katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda, alisema mwenyewe kwa nguvu zote kuwa kila mtu ana uhuru wa kula anachotaka na mtu wa dini moja asimhukumu mtu wa dini nyingine kwa kile anachokula. 

Baada ya Rais Mstaafu kukemea jambo hili, hali ikawa ya amani na utulivu.   Kwa nini Serikali yetu ya sasa inapata kigugumizi kuhusiana na suala zima la nani achinje? 

d) Kwa mantiki hiyo hapo juu katika kipengele cha a-c, Wakristo wanaitaka Serikali iweke utaratibu wa kugawana machinjio na mabucha kati ya Wakristo na Waislamu ili kila Mtanzania awe huru kujinunulia kitoweo mahali anapotaka.   Sambamba na kuitaka Serikali kufanya hivyo, tunawakumbusha Wakristo wote Tanzania kuelewa kuwa watakuwa hawajavunja sheria yoyote ya nchi wakiamua kujichinjia kitoweo chao wenyewe. Kuhusiana na tangazo hili kwa Wakristo wote, tunaitaka mihimili ya dola (Serikali na Mahakama) kuheshimu Katiba ya Nchi yetu, na kipekee kuhusiana na jambo hili Ibara ile ya 19. 

e)   Kwa upande mwingine, kwa kuwa tayari zipo bidhaa za vyakula katika nchi hii ambazo zina nembo ya ‘halal’ na nyingine hazina nembo hiyo, huu ni uthibitisho kuwa vyakula hivyo vimegawanywa kwa kufuata misingi ya imani za kidini. Kwa hiyo, madai ya kugawanya machinjio na mabucha kwa kufuata misingi ya dini sio jambo jipya kwa sasa katika nchi hii.   

 2.2 Uchomaji wa Makanisa ulioambatana na vitisho na mauaji ya viongozi wa KanisaKanisa linalaani vikali mauaji ya kidini yanayoendelea kufanywa pamoja na vitisho (systematic persecution) kwa viongozi wa Kanisa na Wakristo wote kwa ujumla. Mtiririko wa matukio mbali mbali ya nyuma yanatudhihirishia kuwa kumekuwepo na mpango wa muda mrefu wa haya yanayotokea sasa hivi.    

Tarehe 15 Januari 2011, kundi la Waumini wa Kiislamu walipokutana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, miongoni mwao walikuwamo mashehe, walijadili hali ya nchi ya Tanzania kuongozwa kwa mfumo wa kidini.    

Mkutano huo ulihitimishwa kwa kutoa tamko dhidi ya kile kilichoitwa mfumo Kristo katika nchi yetu! Japo Serikali na vyombo vyake vya usalama wa Taifa vimekuwa vikipata taarifa za vitisho dhidi ya viongozi wa Kanisa, mauaji, kuchomwa kwa nyumba za ibada, pamoja na maneno ya uchochezi kupitia mihadhara, vipeperushi, CD na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taasisi zinazofahamika, hata hivyo Serikali kwa kiasi kikubwa imeshindwa kuchukua hatua kwa wakati muafaka na wanasubiri hadi maovu yatendeke ndipo ati waanze kufanya uchunguzi.  

 Kwa Serikali yetu inaonekana wazi kuwa katika hili ile methali kwamba “Kinga ni bora kuliko tiba” haina maana yoyote.    

Hii ni kuonyesha udhaifu mkubwa wa vyombo vya usalama wa Taifa au pia kwamba vyombo hivi vinafurahia kutoweka kwa amani nchini mwetu, jambo ambalo linalifanya Kanisa nchini Tanzania liamini kwamba matukio haya yanayoendelea kutokea ni dalili kuwa Serikali ina agenda ya siri dhidi ya Ukristo.    

Kutokana na hayo Jukwaa la Wakristo Tanzania linatamka kama ifuatavyo:    

a) Tunatambua kwamba ni jukumu la Serikali kuwatendea raia wake kwa usawa na bila ya ubaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 12 na 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.   Viongozi wa Kanisa wanatamka kwamba Serikali imeshindwa kuheshimu Katiba juu ya hizi haki za raia wake na kupelekea waamini wa dini ya Kikristo kukosa imani na Serikali iliyoko madarakani, hasa kuhusu ulinzi na usalama wao na mali zao kama inavyoagizwa kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.   Kama Serikali inaona haiwezi kuwahakikishia wananchi usalama wa uhai wao na mali zao, na hivyo kuwafanya waishi maisha ya hofu inayotokana na vitisho, basi kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, hakuna sababu ya Serikali iliyoko madarakani kung’ang’ania kuongoza nchi.    

b) Kwa kuwa ulinzi wa raia ni haki ya kikatiba na kisheria, Serikali inatakiwa iwalinde raia wake.    Kama Serikali imeshindwa kuwalinda raia wake, Kanisa linataka Serikali ikiri hivyo ili Kanisa liwaambie wananchi waiwajibishe Serikali na Viongozi wanaoifanya Serikali ishindwe kutimiza wajibu wake.   Jukwaa la Wakristo linasema: Kama Serikali haitachukua hatua za makusudi dhidi ya mambo haya yaliyoainishwa hapo juu, Kanisa litachukua hatua ya kuwaambia waamini wake kwamba Serikali iliyoko madarakani inaibeba dini moja, na hivyo Kanisa litatafakari upya uhusiano wake na Serikali.  

 3. Wakristo walioko Zanzibar Wakristo walioko Zanzibar wanatishiwa maisha yao na mali zao zinaharibiwa mara kwa mara, kiasi cha wengine kuamua kuhamia Tanzania Bara. Kigezo cha unyanyasaji huo ni suala la udini na muungano. Inaonekana ni kama vile Watanzania waliozaliwa Bara hawana haki ya kuishi Visiwani. Na kumbe wale waliozaliwa Visiwani wafikapo Barani wana haki zote. Kanisa linaitaka Serikali iwahakikishie Wakristo walioko Zanzibar usalama wao na wa mali zao maana hiyo ni haki yao ya Kikatiba.    

4. Vitisho na mauaji ya Wanakanisa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ichukue hatua za makusudi za kuzuia vitisho na mauaji kwa Viongozi wa Kanisa na Wakristo kwa ujumla. Vinginevyo Kanisa litautangazia ulimwengu kuwa Tanzania ni nchi mojawapo inayovunja haki za binadamu kwa ubaguzi wa kidini na kulitesa Kanisa kimfumo.    

5. Matumizi ya Vyombo vya Habari: Kwa kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimeruhusu vitumiwe kuwatukana Viongozi wa Kanisa, tunatoa nafasi kwa vyombo hivyo kuomba radhi; vinginevyo tutaitaka dunia ivielewe kuwa navyo ni sehemu ya chanzo cha migogoro. Pia tunachukua nafasi hii kuvitahadharisha vyombo mbalimbali vya habari kupima kwa kina ni nini kinachosemwa na viongozi wa kidini ili kuviepusha vyombo hivyo kutumika kwa nia ya uchochezi; yasije yakatukuta kama yale yaliyotokea kule Rwanda 1994.  

 6. Hitimisho: 

Kanisa linaendelea kusisitiza kuwa silaha kuu ya Mkristo katika nyakati hizi ni maombi na kufunga. Kwa mantiki hiyo, Kanisa linawataka Wakristo wote nchini Tanzania kuungana kwa pamoja katika maombi na kufunga kwa muda wa siku saba kwa ajili ya hali hii iliyojitokeza hapa nchini. Maombi hayo na mfungo vifanyike kabla ya Pasaka, yaani kuanzia, tarehe 24/3/2013 hadi 30/3/2013.    

Kwa niaba ya Maaskofu 177 walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Dharura wa Jukwaa la Wakristo na kutoa maazimio hayo.  

 1. Askofu Peter Kitula – Mwenyekiti CCT

 2. Askofu Tarcisius J. M. Ngalalekumtwa Rais TEC  

3. Askofu David Batenzi Mwenyekiti PCT DAR ES SALAAM,        MITAZAMO YA WANAMAONI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA MZALENDO.NET   Makame silima 22/03/2013 at 3:52

Wazanzibar Taget ya Tamko hili la wakristo mazumuni hasa ni Zanzibar kwa kuliwa Padri Mushi, Hii ndio chachu zaidi ya kikao hichi utazani Tanganyika hakuliwi Mapadri au vitendo vya mauaji kama hayo ya Maskofu.
Hili la Padri Mushi linawasi wasi kuwa inawezekana ni vile watu wanavyo sema kuwa mtandao wa kundi la Maskofu kuingiza Madawa ya kulevya umehamia Zanzibar bada ya kule Bara kustukiwa na kukamatwa maskofu wengi.

Lakini kwa upande wa Zanzibar hili limekuzwa kwa sababu kuna agenda ya siri kutumilia mwanya huu ili kuwazibidi/kuzibitiwa wananchi wa Zanzibar kwa vitisho vya udini au Ugaidi kwa vile wananchi wa Zanzibar %99 ni waumii wa dini ya Kislamu na Mapadri wameshindwa kuwazibiti kutokana n wingi wao Wazanzibar .

Wazanzibar tutahazari na chokochoko na sumu wanazo zimwaga ndani na nje ya Zanzibar wakristo kuipaka matope Zanzibar na watu wake ili ionekane Zanzibar wananchi wake wanawapiga vita Wakristo wa Zanzibar hali yakuwa ni chuki zenye kupandikizwa na Mapadri wa Tanganyika.

Tahadharani viongozi wetu wa Smz na mbinuza Maskou kuipaka matope na kupandikiza fitna za udini , Wananchi wa Zanzibar inajulikana kuwa ni waumini wa dini ya Kislamu %99 n wana haki kwa wingi wao kuweka mbele dini yao ambayo ndioyenye utamaduni wa kizanzibar.

Kwa hio viongozi wa Smz mukikubali kulichwa mawazo na kupokea sumu za % 0 ya Mapadri walkuja Zanzibar na mukaacha 599 ya wenyeji wa Zanzibar basi Zanzibar na watu wake mudakuwa hamukuitendea haki na Allah hato wacha kwa hilo.

Huwezi kusema kama kigezo cha Maskofu wakitumiacho kuwa Tanzania haina dinina unaweza kuichi na kuhubiri dini yako popote pale ndani ya Tanznia? hii kwa Zanzibar isiruhusiwe kwani Tanzania ni nchi ya Muungano wa nchi mbili yani ilokuwa Tanganyika na Zanzibar .

Kwa upande wa Zanzibar inayo dini kwa vile utamaduni wa Zanzibar unatokana na dini yao na mila zao zinatokana na dini yao sasa ukisema Tanzania haina dini nikuwanyima haki ma-jourty ya Zanzibar ambao wakazi wake ni waumini wa dini ya kislamu.

Tunawanasihi viongozi wetu wa Smz wasiangalie siasa tu , wajaribu kuzinduka kwa kuangalia mbinu na mipanga ya makafiri kwa kutaka kuinakamiza Zanzibr na kizazi chake, hili ni jukumu kubwa kwao mbele ya Allah.

Hii leo niaibu kuskia familia ya kizanzibar inauza dini yao kwa $100 dolla (innalillahiwainnailaihirojiun) M/mungu wazinduwe viongozi wetu wa Smz na uiokowe Zanzibar yetu, hal ni yakutiha na ni aibu na fedheha.


Fidoski 21/03/2013 at 5:46


Habari hii sio kwa wanamzalendo bosi wangu, hii habari ni kwa serikali ya Kikwete, hayo ni madai yao kwa serikali, ila mimi naona wamekosa hekima viongozi hawa wa dini, maana kama kweli nyinyi ni watu wazuri na malengo yeni mazuri basi wangetumia busa na hekima ktk kudai hili suala lao. kuna taratibu nyingi tu

1. wangeomba wakutane na raisi moja kwa moja ili waweze kumuelezea a to z au

2. kama kumuona ni ngumu wangemuandikia barua raisi wakafikisha madai yao kwa njia ya barua halafu wakasubiri majibu kutoka kwa raisi baada ya hapo wakiona hawajaridhika na maji hayo ndio watoe tamko sio kutoa tamko kwanza tna kwa vitisho eti wanaitishia serikali isipofanya hivyo wanavyotaka basi watawatangazia wananchi waitoe madarakani serikali iliopo, wawatangazie wakristo wezao na sio wananchi wote maana kwa mananchi anejitambua hawezi kusikiliza utumbo huu na aka take action eti tu kwasababu ya kuchinja, ivi unaakili wewe? sala la kuchinja unalishadidia kiasi cha kuitishia serikali, huko ni kukosa hekma na busara tena hawa ni viongozi wa juu wa dini, sijui hao wanaowaongoza wanajifunza nini kupitia viongozi hawa? eti jamani hebu nisaidieni.

Kama ni kudai na sisi tutadai siku ya mapumziko iwe alhamisi ( kwa ajili ya maandalizi) na ijumaa ( kwa kufanya ibada na mapumziko) kwa waislamu, maana tumeshakuwa wajinga sisi waislam tunaokubali kupumzika jumamosi na jumapili ambapo wakristo wote wanakwenda kufanya ibada katika makanisani. au vipi jamani?

Ashakh (Kiongozi) 21/03/2013 at 7:55
MMMhhhh

Kweli kazi kwetu! Hao ndio Wakiristo.

Ndio walioiweka serikali hii madarakani kwa makubaliano wautumikie, ikiwa wamekhalifu miadi hapo watakuwa wamekwenda kinyume namakubaliano yao na hivyokutoamwanya wa kukuadhibu.

Inaonekana kama vile na wao wameogopa kitu fulani hivi, kwani hawana kawaida ya kuripuka kama hivi. Wao huenda na strategies tu, iweje leo waje na msimamo dhahiri shahiri?

Moja katui ya haya; wameona mambo hayawaendei vizuri au wamejiona sasa wameshapata power ya kusema na kufanya chochote wananchotaka.

Mwisho nasema “WAKOME” kuihusisha Zanzibar na fitna zao.Hala abdalla 21/03/2013 at 6:21
Kweli haya ni maneno ya kusemwa na watu wa Mungu?huu si uchochezi tu na uongo wa wazi?toka lini Zanzibar kunyaynyaswa wa bara?bali tumeshuhudi wao kupewa fursa zaidi,tunao makatibu wa kuu na maofisa kibao,pia hata ktk uchaguzi wapemba wangapi wanoishi Unguja zaidi ya miaka 10 wamekataliwa kupiga kura lkn wao hukusanywa kwa gari na kupewa priority,nna mfano mmoja tulikua na mfanyakazi wa nyumbani hapo mpendae ambae alifika znz chini ya mwaka ikawa uchaguzi tayari basi alitwambia mwenyewe wameekewa gari na sheha na wabara wenzake ili wapelekwe kujiandikisha, na huo udini udini gani ?

kwa sababu Waislam wamechoka maonevu wamepaza sauti kidogo tu ndio imekua mwao?Waislam mara kibao wamenyanyaswa kwa mavazi yao kuna waliotolewa madarasani na maofisini kwa kuvaa hijabu au kofia lkn hatujawahi kusikia sister kakatazwa kuvaa nguo yake juu ya kua kuna uniform ikiwa ni chuo au schoo au kazini nlikua nafanya degree tulikua na masister wakisoma nurse lkn wakivaa nguo zao na scurf zao,rangi ya blue na wenzao wakivishwa vimini pink na kikofia hata uwe muislam hapana ruhusa.

kama wao ni waadilifu mbona hatujasikia wakitaja mauaji ya sheikh?au roho ya mkristo tuu ndio tamu ya sheikh halali kutoka kikatili?

na kama wao ni watu wa amani mbona pale wakereketwa wakikatoloki na wengine wanapoanzisha fujo hawakemei au ni safi tu kwao ni halali kuwadhulumu waislam maana kwao wao si binaadam maana hawajamuamini Yesu.

basi yasiishie kuchinja tu wajue kua na holiday iwe na friday,na kwaya marufuku ofisini na redio za kikristo, la sivyo na Quraani na mawaidha yapigwe,pia hatuishii kuchinja tu itabidi shughuli za makafir ( =watu waliokataa tauhidi) marufuku kushiriki kwani kuna nyama haramu pia kununua mishikaiki na vitu vyote vya nyama,na hii inamaana hata kama ndugu yako wa damu usiende hii ndio chuki wanayotaka kuipandikiza hali hapa bara utaona mtu ana mtoto au ndugu wa damu au wazazi ambao ni muislam.

lkn mm naona wanafanya dhulma wakijua bcos wanajua wanamtumikia Mungu asie sahihi kama kweli ni watu wa Mungu wa haki wasingesema haya.

Na hizi chokchoko za znz ni ajenda yao mahsusi lkn na sisi tunasema ALLAH atawashinda

“wanataka kuizima nuru ya ALLAH kwa vinywa vyao na ALLAH ni mwenye kuitimila”

wataondoka tu patupuINSHAALLAH na dhulma zao zina mwisho wao hawana hati miliki ya nchi.


Ghalib 21/03/2013 at 10:13
ipo nasi kupigania siju ya alhamis na ijumaa kuwa ni siku ya mapumziko kislamu kwa waislamu, leo hi kazini tuende na msikitini tuende au ukose kazi !

Wao jumapili wanafanya ibada zao wakiwa free kabisa ! Nani anaupendeleo katika hili taifa ?

Sisi zanzibar asilimia 99 waislamu kwa nini alhamis na ijumaa haiwi ni mapumziko ? Wakati umefika kudai haki zetu

wakiristo wanaonesha wazi wazi nia zao zilivyo kuwa mbaya zidi ya wazanzibari waislamu hasa ndiko waliko lenga hoja yao.

Kuuliwa kwa padri mushi wana ushahidi gani kwamba haya ni mapigano zidi yao na waislamu ? Huu ni uchochezi, hapa wameenda mchomo,kwa vile hi habari wameandika kanisa sheria zitapuuzwa, tusubiri baada ya siku tatu watatoa tamko sio wao walioandika huo utumbo ju.

No comments: